Image result for MAGUNIA YA MAINDI

 irika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limeripoti kuwa dunia nzima imepata mavuno makubwa, lakini limetahadharisha kuwa upatikanaji wa chakula umepungua kutokana na mapambano na ukame katika baadhi ya nchi ikiwemo Afghanistan, Burundi, Sudan Kusini na Yemen.

Ripoti imesema ingawa utoaji wa chakula umeimarika, ukame unahatarisha usalama wa chakula katika nchi za Afrika Mashariki, huku upatikanaji wa chakula ukipungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo yanayokumbwa na mapigano ya ndani.
Ripoti pia imesema, nchi 28 miongoni mwa 37 zinazohitaji msaada wa chakula kutoka nje, ziko barani Afrika.

Comments

Popular Posts