UJUE MTI WA MAAJABU DUNIANI, UNA ZAIDI YA VIRUTUBISHO 96 KWA AFYA

Moringa Oleifera tree Dar es Salaam


UJUE MTI WA MAAJABU DUNIANI, UNA ZAIDI YA VIRUTUBISHO 96 KWA AFYA

 Mlonge ni mti ambao umeiteka dunia na kuwa mti wa maajabu duniani kutokana na ubora wa hali ya juu na kuwa na virutubisho(nutrients) zaidi ya 96, madini zaidi ya 46 na si hivyo tu bali na kutumika kama zao la chakula, Dawa, lishe, mboga za majani, juisi, chai na mambo mengine kadha wa kadha. Mti huu umepewa kipaumbele sana na nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani, ufilipino, na hata barani Afrika  kama Afrika kusini, Senegal, Kenya n.k kutokana na faida zake ambazo zinapatikana katika majani yake, mizizi na hata mbegu zake.

Mlonge unasifika na kupendwa kama zao la chakula, dawa na hata kibiashara ambalo ni zao la kudumu(permanent) na husitawi na kuota katika ardhi yoyote ile na katika kila aina ya vipindi vya majira kutokana na desturi yake ya kuchipua shina juu ya shina na na kukua ndani ya wiki mbili ambapo mlimaji huanza kuvuna mazao(chakula) na pia huongezeka kimo wiki, mwezi, mwaka na miaka kutokana kiwango chake kizuri cha uhifadhi wa maji hali ambayo imewafanya watu mbalimbali  duniani kuuita mti huu kuwa ni mti wa maajabu na jina lingine liliozoeleka ni Moringa Oleifera. Licha ya mlonge kuwa bora kwa chakula pia unatoa vitamin A, C, B, E, pamoja na madini ya Protini, chuma, Magniziam, Nitrojen na mengine mengi pia mti huu unasaidia kuondoa vitambi, kusafisha macho, dawa ya kusafishia nywele, kukomaza mifupa na kurekebisha mzunguko wa damu ikiwa ni pamoja na kusaidia zaidi katika tatizo la shinikizo la damu (BP), Wataalamu wanasema ukitumia mlonge unakuwa umepata mlo kamili na kupata virutubisho vyote ambavyo ungepata katika vyakula na matunda mfano Karoti, Mayai, nyama, mahindi n.k

Kumekuwepo na hali ya sisi binadamu kupuuza baadhi ya miti hata kuikata ili kutengenezea kuni na hata wengine pia kuchoma mkaa huku tukisahau umuhimu wa kuwa na miti hii, pia tunashuhudia baadhi ya watoto wachanga huzaliwa wakiwa na tatizo la utapia mlo, mama pia kukosa maziwa kumnyonyesha mtoto bila kujua nini tatizo! Wahenga walisema “Kuzaa mwana si kazi bali kazi ni kumlea huyo mwana” hii inajidhihirisha bayana kutokana na mti huu wa Mlonge kuwa na madini ya nitrojeni na chuma ambayo yatamsaidia mama Mjamzito kujenga mifupa ya mtoto tumboni na pia hata mtoto atakapo zaliwa ataweza kupata maziwa ya kutosha kutoka kwa mama ili kumnyonyesha vyema na kuwa na afya njema. Mlonge pia hutibu Bacteria na fangasi, unaweza pia kutengeneza chai ya mlonge ambao uko katika hali ya unga, pia kupata mafuta kutokana na mbegu zake pia sabuni kutokana na mlonge kwani hauna kemikali zozote.

Watu mbalimbali  duniani wamenufaika na kufanikiwa kiuchumi kwa kutumia mlonge kulima kama zao la biashara pamoja na chakula na kuyaendesha maisha yao vyema kama utakavyoona katika vidokezo(links) hapo chini. Sisi watanzania tunaweza hebu tujiokokoe katika janga la njaa na umasikini  kwa kulithamini zao hili la mlonge kama utajiri wetu na daktari wa afya yetu hususani katika Maisha yetu hasa kwenye kipaumbele cha kilimo kwanza. Nina imani mpaka hapo umeufahamu na kuujua mti wa maajabu duniani na faida zake. Huu ndio mti wa maajabu (Miracle tree)

Unitaji mlonge 0756 483 174

Comments

Popular Posts