Hali ya chakula nchini kuelekea mwaka 2017


1.            Hali ya Chakula
Hali ya chakula mwaka 2016/2017 ni ya kuridhisha kutokana na mavuno yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2015/2016. Tathmini ya awali (Preliminary Forecast) ya uzalishaji wa mazao ya chakula iliyofanyika mwezi Julai 2016, nchi inajitosheleza kwa chakula kwa viwango vya utoshelevu vya asilimia 123. Kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara Mikoa 11 ilibainika kuwa na viwango vya ziada vya chakula mikoa 12 ina hali ya utoshelevu na mikoa 2 ina uhaba wa chakula.  Katika mikoa 15 ilibainika kuwa na maeneo yenye uhaba wa chakula katika Halmashauri 43 hatahivyo mkoa wa Kagera na lamashauri 3 za mkoa huo zimekuwa na maeneo tete baadaye kutokana na athari za tetemeko la ardhi pamoja na ukame ulioathiri mazao kwa kiasi kikubwa.Kwa ujumla hali ya chakula inaridhisha ukilinganishwa na mwaka uliopita kwa kuwa kulikuwa na jumla ya Halmashauri 69 zilizokuwa zimebainika kuwa na maeneo yenye uhaba wa chakula katika mwaka uliopita.
2.            Uzalishaji wa Chakula
Taarifa ya Tathmini ya awali (Preliminary Forecast) na uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2015/16 inaonesha kuwa kitaifa, uzalishaji wa chakula utafikia tani 16,172,841 za chakula (kwa mlinganisho wa nafaka – Grain Equivalent), ambapo tani 9,457,108 ni za mazao ya nafaka na tani 6,715,733 ni za mazao yasiyo nafaka. Mahitaji ya chakula kwa mwaka 2016/17, tunahitaji tani 13,159,326 ambapo tani 8,355,767 ni za mazao ya nafaka na tani 4,803,560 ni za mazao yasiyo nafaka.
Uzalishaji wa zao la mahindi katika mwaka 2015/2016 ulikuwa tani 6,148,699 ambapo mahitaji kwa mwaka 2016/2017 ni tani 5,202,415. Hivyo, kulikuwa na ziada ya tani 946,284 za mahindi kwa kiwango cha utoshelevu wa asilimia 118. Kwa upande wa uzalishaji wa mchele, jumla ya tani 2,229,071 zilizalishwa kwa mwaka 2015/2016 ambapo mahitaji ya zao hilo kwa mwaka 2016/2017 ni tani 976,925. Hivyo, kulikuwa na ziada ya tani 1,252,146 za mchele kwa kiwango cha utoshelevu wa asilimia 228.
3.            Hifadhi ya Chakula ya Taifa
Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa mwaka wa fedha 2016/2017 umepanga kununua jumla ya tani 100,000 za chakula. Hadi kufikia tarehe 24 Novemba 2016, Wakala umenunua jumla ya tani 61,145.245 za chakula sawa na asilimia 61 ya lengo ililojiwekea. Kati ya kiasi hicho, tani 38,132.389 zimenunuliwa kupitia vituo vya ununuzi na tani 23,012.906 kupitia vikundi vya wakulima. Hata hivyo, hadi kufikia tarehe 24 Novemba, 2016 Wakala umetoa jumla ya tani 20,048.521 za chakula. Aidha, hadi kufikia tarehe 26 Disemba, 2016 Wakala una akiba ya tani 90,716.798 za chakula.
4.  Matarajio ya Hali ya Chakula
Tanapoanza mwaka 2017, tunatarajia hali ya chakula kuendelea kuwa ya kuridhisha kutokana na mavuno ya msimu uliopita wa 2015/2016. Bei ya chakula husuani mahindi katika kipindi hiki imepanda kidogo ukilinganisha na bei za mwaka jana mwezi kama huu. Mwenendo wa kupanda kwa bei ya mazao unatokana na kupungua kwa uingizaji wa mazao sokoni ambayo ni hali ya kawaida kila mwaka. Bei ya mchele sokoni bado ni ya kuridhisha.
Mvua za vuli zilichelewa kuanza  na zimenyesha chini ya kiwango na kwa mtawanyiko usioridhisha  katika maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka. Uzalishaji unaotokana na mvua za vuli huwa unachangia takribani  kati ya asilimia 17 hadi 20 ya chakula nchini. Aidha, maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka (mvua za msimu) mvua zimeanza pia kwa kuchelewa na za chini ya kiwango. Hali hiyo, kwa kiasi fulani inazidi kuathiri uingizaji mazao ya chakula kwa wingi  sokoni na hasa mahindi kutokana na wafanyabiashara kuhodhi mazao hayo wakiwa na mategemeo ya bei kupanda baada ya taarifa za hali ya unyeshaji mvua kuonyesha kuwa mvua zitakuwa chini ya kiwango na hivyo uzalishaji unategemewa kutokuwa wa kuridhisha.Mabadiliko ya tabia nchi kwa kiasi kikubwa yamechangia mvua kunyesha chini ya kiwango na kwa mtawanyiko mbaya.
Wizara inaendelea kuwasiliana na mikoa ili kufuatilia  kwa karibu  hali ya upatikanaji wa  chakula pamoja na bei, mwenendo wa mvua na hali ya mazao mashambani.Taarifa  zinazopatikana zitaisaidia  Serikali na kuchukua hatua stahiki  kulingana na hali itakayojitokeza. Aidha, tathmini ya kina ya hali ya chakula na Lishe inatarajiwa kufanyika katika maeneo yenye hali tete mwanzoni mwa mwezi Januari 2017 ili kubaini idadi ya watu walioathirika na mahitaji ya chakula na mbegu.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     
5. Ushauri
  • Wafanyabiashara watumie fursa ya kuwa na bei nzuri ya mazao kutoa akiba ya mazao waliyoyahifadhikatika maghaliaa yao na kuyaingiza katika soko.
  • Wakulimawatumie mvua zinazonyesha kupanda mazao yanastahimili mvua kidogo na yanayokomaa mapema.
  • Wataalam wa kilimo wanatakiwa kuendelea kutoa ushauri kwa wakulima juu ya mazao yanayofaa katika maeneo yao ili kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha.
  • , Wananchi kote nchini wanatahadharishwa juu ya kuzingatia hifadhi ya mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaathiri kwa kiwango kikubwa mzunguko na upatikanaji wa mvua zinazotosheleza uzalishaji wa mazao hapa nchini.


Kiambatisho 1a: Mwenendo wa bei za mazao ya chakula, kwa miaka ya 2002 hadi 2016
      (Bei (TSh) kwa Gunia la Kilo 100)

MWEZI










ZAO

JAN
FEB
MAR
APR
MEI
JUN
 JUL
AUG
SEP
OKT
NOV
DEC
Mahindi
2002
14,363
14,716
15,267
14,055
10,987
9,035
9,190
9,237
10,005
11,262
11,446
11,586

2003
13,471
12,413
13,028
14,089
14,333
15,025
16,347
17,215
17,323
17,713
18,678
21,804

2004
25,260
25,957
25,816
21,154
15,855
13,400
13,997
16,069
16,239
16,440
16,652
16,467

2005
16,221
14,298
14,656
15,500
16,020
17,072
16,839
16,372
16,402
16,364
18,763
22,099

2006
29,945
30,594
32,046
33,139
30,406
25,973
22,112
20,554
19,679
19,460
18,789
18,095

2007
19,104
18,283
17,815
17,026
17,371
16,882
18,241
19,528
21,802
24,394
25,468
28,281

2008
32,065
31,181
35,458
32,798
30,090
28,194
28,628
28,867
28,792
30,927
32,391
35,029

2009
36,612
39,314
38,022
35,959
35,005
35,245
34,128
32,481
36,801
38,439
40,930
43,841

2010
46,111
46,472
41,426
33,864
29,542
27,530
27,745
28,259
28,988
30,217
32,050
33,695

2011
35,133
37,531
40,740
43,666
42,265
43,326
44,524
42,246
42,227
41,492
42,242
42,976

2012
44,437
42,388
43,270
46,751
51,185
50,378
50,165
50,487
54,291
58,120
65,498
56,318

2013

77,416
73,192
64,842
65,431
49,096
49,967
52,554
53,539
53,686
53,826
55,674

2014

54,547
51,855
49,876
47,583
47,681
44,642
41,313
40,602
39,510
38,243
38,470

2015
38,232
37,355
39,491
47,702
47,042
48,025
52,219
56,318
57,717
57,756
63,774
65,104

2016
67,048
67,326
63,912
57,431
55,976
53,986
57,011
55,571
56,312
63,133
72,133





Kiambatisho 1b: Mwenendo wa bei ya mahindi



Comments

Popular Posts