KILIMO CHA KISASA CHA GREENHOUSE (BANDA KITALU) NA FAIDA ZAKE​


[​IMG]

Green Agriculture

Ndugu Msomaji karibu tena leo tujuzane kuhusu banda kitalu yaani Green house 
Nini Maana ya Green House?
Green house ni hali nuai(artificial environment) ya kimazingira iliyotengenezwa kwa ajili ya uhitaji fulani wa kitu(zao) ambacho hakiwezi/kinaathirika kikiishi katika mazingira halisia au hakiendani na mazingira halisia na ningependa ujue ya kuwa green house sio ile nyumba bali ni ile hali ya ndani inayotengezwa na ile nyumba.Hali mbali mbali zinaweza kutengenezwa na green house kama maeneo ni ya joto sana na unataka kulima mazao yanayostawi sehemu za baridi unaweza kutengeneza green house ambayo italeta hali ya baridi na pia kama upo maeneo ya joto na unataka kulima mazao mazao yanayostawi sehemu za baridi unaweza kutengeneza green house kwa ajili ya kuleta hali ya baridi na ukafanya kilimo chako bila shida yoyote tena kwa ufanisi mkubwa
NOTE: katika ununuzi wa materials hakikisha ununua kwa mtu mwenye uelewa ili akupe material inayoendana na eneo lako ili upate matokeo mazuri hasa nylon cover kwa nchi za tropical ni ile yenye standard ya 200micron

Greenhouse(Banda Kitalu)
Hii ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa. Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.

Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi za baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse lilipoibuka. Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kitalu ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi. Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti kati yake na zile za nchi za ukanda wa baridi na tofauti yake ni kwenye materilas zinazotumika kutengengenezea hasa polycover tujue kuwa katika dunia yetu kila ukanda una kiwango chake cha mionzi ya jua inayofika eneo husika kwa hiyo green house materilas zinazotumika katika nchi za baridi zina microyn tofauti na zile zinazotumika ukanda wa tropiki mfano kwa tanzania tunatumia polycver yenye 200 micron kuendana na hali ya hewa yetu na usipotumia material ya aina hyo mimea yako itaungua au kutokukua vizuri ndio maana tunashauri ufanye kazi na wataalamu ili upate uhakika wa kile kitu unachokifanya kwa manufaa yetu sote

FAIDA ZA GREENHOUSE

1.Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi,ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.

2.Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya uharibifu wa mazao kama wadudu waharibifu na wale waletao magonjwa kwa mimea.

3.Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.

4.Uwezo wa kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu, ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei za mazao ziko juu na unapata faida kubwa

5.Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti kwani wakati mwingne dawa hazitumiki kabisa kwenye green house.

6.Matumizi bora ya maji kwani drip irrigation system ndio hutumika kwenye green house na ina ufanisi mkubwa katika ufikishaji wa maji kwa mimea na hupunguza upotevu wa maji

7.Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili ya kuzoea mazingira ya nje kwanza. wataalamu wa SUA wanafanya sana hii

8.Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (Hydroponic). Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuzi wa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea

MFUMO WA UMWAGILIAJI KWENYE GH
[​IMG]

mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone yaani drip irrigation system ndio unatumika sana katika green house kwani ndio mfumo rahisi na wenye ufanisi mkubwa sio tuu katika kuhakikisha mmea wako unapata maji shahiki bado katika kubana matumizi ya maji pia, katika mfumo huu tunaweza kuweka mbolea moja kwa moja kwenye mfumo wako na mimea ikapata mbolea kwa njia hii (fertigation) mbolea inawekwa kwenye tank la maji lakini hii ni vizuri ukapata ushauri wa kitaalamu ili tukuambie namna ya uwekaji wa mbolea na kiwango cha kuweka 

ARDHI, UDONGO KWENYE GH
[​IMG]

Ni muhimu kapima udongo kabla ya kuwaza kulima pia hata kwenye kilimo hiki cha kutumia green house ni vizuri kupata data za udongo katika mambo yafuatayao kwanza kabisa data za udongo husaidia katika kufanya design ya mfumo wa umwagiliaji ili mimi mtaalamu niweze kukuambia utamwagilia kwa muda gani na baada ya siku ngapi ( irrigaton time and irrigation intervval mfano . mwagilia masaa matatu kila baada ya siku mbili) na calculation zinafanywa kuendana na uhitaji wa maji katika zao lako na uwezo wa udongo wako kubeba maji .

katika green house kuna kitu tunakiita soil develpment yaani ni kuuandaa na kuuongezea udongo rutuba kwa kutumia mbolea asilia na mchanganyiko wa madini mengine ili udongo uweze kuwa na uwezo wa kuupa mmea mahitaji yake lakini ni vizuri kupima udongo ili mtaalamu aweze kujua ni kiwango gani za mbolea na samadi na vitu vingine vinahitajika katika udongo wako ili mazao yaweze kustawi vzr kwa wateja wetu huwa tunawapa offer ya soil test bure ili waweze kumudu gharama katika uwekezaji huu 

[​IMG]


Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha Greenhouse.
Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii.

Tuanze na Marekani, Marekani ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua, Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka.

Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000 hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga, pamoja na nyanya Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo hazilimwi kwingine. Mazao maarufu yanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.

Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse. Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)

Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa nchi ya Israel eneo lake ni kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse.


Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao yanya na tango yanalimwa kwenye green house. Misri 10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote duniani. Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse. Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama Japan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).

AINA ZA GREENHOUSE
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:

1. Aina za Greenhouse kwa kigezo cha sura/umbile (shape)


Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu




kwa hapa kwetu mara nyingi tunatengeneza gh za iana tatu ambazo zinafanya vizuri sana kama slant roof green house kama ilivyo kwenye picha hapa tunatumia mbao(miti) au chuma

[​IMG]a)Quonset Greenhouse

[​IMG]

b) Saw tooth type

[​IMG]


iii. c)Even span type greenhouse


iv. d)Uneven span type greenhouse


2.Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi


a)Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)


i b)Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)


3.Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)

a)Greenhouse za miti (Wooden framed structure)

i b)Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)

Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma

4. Aina za Greenhouse kwa kigezo aina ya zana za ufunikaji (covering types)

a)Greenhouse zinazofunikwa kwa zana za Vioo (glass)- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndani greenhouse

b)Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya nylon (polycover)

5. Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa

Katika green house unaweza kulima mazao mengi hasa ya mbogamboga na matunda ambayo yana soko zuri na uapatikanaji wake ni adimu sana , kwa kuwa kilimo cha gh ni uwekezaji bora kwenye kilimo 

ORGANIC FARMING(KILIMO HAI)
hiki ni kilimo ambacho huhiji kutumia kemikali zozote wala mbolea za viwandani yaani ni kilimo asili, kwa nchi za wenzetu mazao ya kilimo hai yana bei mara kumi zaidi ya mazao ya kilimo cha kawaida kwani kukua kwa teknolojia na uharibifu wa mazingira bidhaa za kilimo zimekuwa zikitumia kemikali nyingi sana ambazo huathiri afya ya binadamu moja kwa moja au madhara huonekana baadaye sasa ukiwa na green house utaweza kufanya kilimo hiki na familia yako ikatumia chakula safi ambacho hakijawekwa chemikali

kwa mahitaji ya kutengenezewa green house ya kisasa kwa bei nafuu wasiliana na mimi pia baada ya kukutengenezea structure yako hatutakuacha hivi hivi ila tutakupa mtaaalamu wetu ambae ni Agronomist Boniphace Mwanje(0719880905) aliebobea kwenye utaalamu mbegu,mbolea,madawa na utunzaji wa mimea na huduma nyingne za aina zote za umwagiliaji, kupima udongo, kuchora na kupanga ramani za mashamba na taasisi au kampuni

Comments

Post a Comment

Popular Posts