Sunday, April 30, 2017

BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA-TADB YAKOPESHA WAKULIMA WADOGO SHILINGI BILIONI 6.5

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji

                                                                                 Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma

Mikoa mitatu ya Tanga, Morogoro na Iringa, imenufaika na kiasi cha shilingi bilioni 6.5 zilizotolewa kama mkopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) tangu benki hiyo ianzishwe mwaka 2015.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu swali na msingi lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Felister Aloyce Bura, aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanza kutoa huduma kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Dodoma.

Dkt. Kijaji ameeleza kuwa hadi kufikia mwezi Desemba, 2016, TADB imetoa mikopo ya jumla ya shilingi 6,489,521,120 kwa ajili ya kutekeleza miradi ishirini (20) ya kilimo katika mikoa hiyo mitatu ya Iringa, Morogoro na Tanga.

“Sambama na utoaji mikopo, Benki inatoa mafunzo kwa wakulima ambapo hadi sasa vikundi 336 vya wakulima wadogowadogo vyenye jumla ya wanachama 44,400 wamepatiwa mafunzo hayo katika mikoa hiyo mitatu” aliongeza Dkt. Kijaji

Amesema kuwa Benki hiyo inatarajia kuanza kutoa huduma hiyo kwa wakulima wadogowadogo wa Mkoa wa Dodoma na mikoa mingine jirani wenye sifa.

“Benki imepata nafasi kwa ajili ya kufungua ofisi katika jengo la PSPF mjini Dodoma na itakabidhiwa ofisi hiyo mwezi Julai, 2017, baada ya mkandarasi kukamilisha ujenzi wa jengo hilo” Alisisitiza Dkt. Kijaji

Dkt. Kijaji amesema kuwa tayari Benki hiyo imemwandikia barua Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma ili kuomba aipatie miradi mizuri ya kilimo ambayo mkoa unapendekeza Benki iifikirie katika zoezi la kutoa mikopo itakayoanza kutolewa mwishoni mwa mwaka 2017.

Saturday, April 29, 2017

KILIMO BORA CHA MAHIND

KILIMO BORA CHA MAHINDI

KILIMO BORA CHA MAHINDI

MAHINDI-MAIZE ( Zea mays)

www.kilimofaida.blogspot.com

 Image result for picture of maize plantImage result for picture of maize cob

1.UTANGULIZI
www.kilimofaida.blogspot.com
Mahindi ni zao la nafaka ambalo lina kiasi kikubwa cha wanga.Kwa kiasi kikubwa mahindi hulimwa kama zao la chakula,lakini pia likilimwa vizuri linaweza kutumika kama zao la biashara kutokana na mavuno yake mazuri,Ekari moja hutoa Kg 2000 hadi 4000 kutegemea na matunzo na aina ya mbegu.www.kilimofaida.blogspot.com

2.HALI YA HEWA IFAAYO
Mahindi huwezwa kulimwa na kustawi vizuri katika uwanda wa chini kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 2500 kutoka usawa wa bahari.Mahindi mengine hukubari vizuri katika ukanda wa chini na mengine katika ukanda wa juu.hukua vizuri katika maeneo yapatayo mvua za kutosha kiasi cha milimita 750 na kuendelea kwa mwaka hustawi katika nyuzi joto 22 -33 C.

3.ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA MAHINDI

Hustawi vizuri katika udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye pH ya 6 hadi 7.hukubari katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji.unaweza kulima katika udongo wa kichanga au mfinyanzi japokuwa katika udongo wa mfinyazi kama mvua itakuwa kubwa na maji yakatuama kwa muda mrefu huzuia ukuaji mzuri wa Mahindi.

4.MAANDALIZI YA SHAMBA LA MAHINDI

Shamba la mahindi inabidi liandaliwe mapema kwa kulisafisha na kuondoa uchafu na takataka zisizoweza kuoza kwa urahisi,Kisha shamba lilimwe vizuri kabla ya msimu wa kupanda kuanza.Shamba hilo linaweza kulimwa kwa kutumia trekta Jembe la mkono au kukokotwa na ng'ombe.

5.MBEGU BORA ZA MAHINDI

Kuna aina mbali mbali za mbegu bora za mahindi,na mbegu hizi hufaa zaidi kulingana na ukanda husika kutokana na utofauti wa hali ya hewa na urefu au ufupi wa msimu wa mvua
Maeneo ya nyanda za juu kusini hupata mvua nyingi na za muda mrefu katika msimu hivyo mbegu nyingi za hybrid hufaa katika kanda hizi mikoa ya nyanda za juuu inajumlisha Mbeya,Iringa ,Rukwa n,k na Mikoa ya nyanda za chini hupata mvua chache na za muda mfupi kama vile Dodoma,singida na mikoa mingi ya sehemu za pwani kama vile Lindi,Mtwara na Tanga.

AINA ZA MBEGU.
 Mbegu aina ya chotara(hybrid)-Hufaa katika maeneo yenye mvua nyingi mfano UYOLE, DK,SIDCO ,PANNAR, PIONEER, KITALE

 Aina ya ndugu moja(synthetic)
 Mbegu aina ya composite-Hufaa maeneo yenye mvua chache mfano TMV 1,TMV 2,staha,Kito.Katumbili n.k
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 20-40 kwa ekari.

6.UPANDAJI WA MAHINDI

Mahindi inapaswa yapandwe mwanzoni mwa msimu wa mvua,ili yaweze kukua vizuri na kutoa mavuno yaliyo bora.
Kiasi cha kilogram 7- 10 za mbegu ya mahindi huitajika katika ekari moja.

NAFASI YA UPANDAJI
Fukia mbegu yako katika kina cha sentimeta 2.5 hadi 5 ardhini.
kuna nafasi mbalimbali za upandaji wa mahindi kama vile
sentimeta 90 kwa 25- 30- mbegu moja moja
sentimeta 90 kwa 40- 50 Mbegu mbili
sentimeta 75 kwa 30 mbegu moja
sentimeta  75 kwa 50 Mbegu mbili au
sentimeta 80 kwa 40-50 kwa mbegu mbili.
www.kilimofaida.blogspot.com

MUDA WA KUPANDA

Maeneo mengi hupandwa mapema kuanzia mwezi wa  Novemba hadi Januari. kulingana na unyeshaji wa mvua za msimu.Kupnda mwanzoni mwa mvua ni bora zaidi.

FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA

Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
    Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.
Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.

Image result for picture of maize plant



7.PALIZI NA KUPUNGUZA MIMEA KATIKA MSTARI.

Kama shamba lako lina magugu mengi hakikisha unapalilia mapema kabla mimea haijazidiwa na magugu.katika kila shimo hakikisha unabakisha miche miwili ya mimea ya mahindi.hakikisha shamba lako linakuwa safi muda wote.

8.MBOLEA.

Mahindi hukubari vizuri katika maeneo yenye kiasi kikubwa cha rutuba katika udongo,hivyo ili upate mavuno mengi ya mahindi utahitajika upande katika shmba lenye mboji au samadi au shamba lako uwe unatumia mbolea katika upandaji na ukuaji wa mimea.
Unaweza kutumia mbolea za asili kama vile mboji,samadi au  mbolea ya majani ya miti.-Hizi zina kiwango kidogo cha virutubisho.

MBOLEA ZA KUPANDIA MAHINDI
Pia unawza kutumia mbolea za viwandani katika kupanda kwa kiasi cha kg 50 kwa ekari ,mbolea kama vile DAP,Minjingu mazao,NPK au DSP kulingana na upungufu wa virutubisho vya aina fulani katika udongo.Mbolea  za kupandia huwekwa katika shimo la kupandia kabla ya kuweka mbegu (baada ya kuchimba shimo unaweka mbolea gram 5 kisha unafukia kidogo na kupanda mbegu yako na kufukia Tena,

MBOLEA ZA KUKUZIA MAHINDI
Mbolea za kukuzia kama vile N.P.K,UREA ,CAN,SA www.kilimofaida.blogspot.com hutumika katika kukuzia mimea na kuzalishia mbegu kwa kiasi cha kg 50 kwa ekari.
Mbolea hizi huwekwa baada ya palizi ya kwanza  ambayo hufanyika kati ya wiki ya 3 hadi 4 tangu mahindi kupandwa shambani.Kwa maeneo ambayo mahindi au hupandwa mbegu ambayo huchukua muda mrefu zaidi kukomaa zaidi ya miezi 3 na 4 inashauriwa kuweka mbolea za kukuzia mara mbili.Mara ya kwanza mbolea huwekwa mwezi wa kwanza  baada ya kupanda na  mbolea hurudiwa tena kuwekwa yakifikia  mwezi 1 na nusu (siku 45) hadi Miezi 2 (siku 60). Pia kwa ziada unaweza ukaweka kwa Mara ya tatu Kg 12.5 kwa ekari mbolea ya kukuzia Mara baada ya mahindi kuanza kubeba,Lengo la uwekaji wa tatu wa mbolea ni kuhakikisha jani linalolisha hindi(flag leaf) linakuwa la kijani hivyo kupata mavuno zaidi.
Jinsi ya kuweka mbolea hizi-Kuzungusha shina kwa mbolea bila kugusa mmea,Kuweka mbolea kwa vifungu viwili au zaidi kuzunguka mmea. www.kilimofaida.blogspot.com

KUMBUKA-Haitakiwi kurundika mbolea sehemu moja,Haitakiwi mbolea hizi kugusa mmea wakati wa kuweka kwani zina kiasi cha chumvichumvi ambacho kinaweza kuathiri mmea kama hakuna unyevu wa kutosha.

PIA-MKULIMA lazima ajue kuwa mbolea hizi huwekwa wakati udongo una unyevu wa kutosha au kuna dalili za kunyesha kwa mvua ili kuwezesha mimea kuitumia kwa urahisi bila madhara na Pia kuzuia mbolea isipotee kwa jua kali.

9.UMWAGILIAJI

Kama mvua zitakuwa ni tatizo unaweza kuyamwagilia mhindi yako maji kwa kuangalia kutozidisha hali ya maji katika shamba lako

10.WADUDU www.kilimofaida.bologspot.com
WADUDU WAHARIBIFU WA MAHINDI

A) Viwavi Jeshi
 Ni wadudu aina ya funza ambao hutokana na Nondo.Hushambulia mahindi kwa kula majaniyake pamoja na shina.
Wadudu hawa huangamizwa/kudhibitiwa kwa njia zifuatazo;-
 Kuondoa vichaka karibu na shamba
Kunyunyizia sumu za asili kama vile Mwarobaini majuma mawili ya mwanzo.
Kunyunyizia sumu za viwandani endapo wadudu wameanza kuonekana kama vile Karate au DUDUALL au DUDUBA

B) Funza wa Mabua (Maize Stalk Borer).

Image result for picture of maize plant with maize stalk borer
    Funza wa mabua hutoboa shina la mahindi na kusababisha kudumaa kwa mahindi.
    Matundu, ungaunga kama wa msumeno huonekana kwenye majani yaliyoathiriwa.
    Mashambulizi huanza juma la pili hadi la tatu baada ya mahindi kuota.

Njia za kudhibiti zinazotumika
    Kuchanganya mahindi na mazao jamii ya mikunde kam vile maharagwe
    Kung oa mahindi yaliyoshambuliwa

TIBA
    Puliza Sumu za asili mwarobaini au
    Sumu za viwandani kama vile Karate au Duduall au duduba

KUMBUKA -Unapopuliza dawa hakikisha maji  maji ya dawa yameingia ya kutosha katika mirija ya majani ya katikati ya mahindi. www.kilimofaida.blogspot.com

10.UVUNAJI WA MAHINDI

Mahindi huvunwa .Mahindi huchukua siku  au miezi 4 hadi 6.Kupandwa na kukomaa.Mahindi yaliyokommaa mimea yake huanza kukauka  maganda ya nje .Mahindi huvunwa kwa kifaa maalum ya kuvunia au kuvunwa kwa mikono.Kisha hukaushwa vizuri na kupukuchuliwa kwa mashine au mikono ili kutenganisha na vigunzi/vibunzi vyake. Kisha yaweke katika magunia tayrai kwa kuhifadhiwa.

12.UHIFADHI WA MAHINDI

Baada ya kupukuchuliwa mahindi huwekwa katika mifuko kama vile viroba au magunia na kuwekwa gharani kuhifadhiwa.Mahindi huifadhiwa gharani baada ya kuyachanganya na dwa za kukinga na kuu wadudu kama vile actellic super Dust (SHUMBA) n.k Pia kuna mifuko maalum ya kuhifadhia mahindi ambayo huwezesha kulinda mahindi yasishambuliwe na wadudu. www.kilimofaida.blogspot.com


KILIMO BORA CHA MAHARAGE

       UTANGULIZI
Maharage ni moja kati ya mazao ambayo yanalimwa sana na ni moja kati ya mazao yanayo waongezea kipato wakulima wengi sana nchini Tanzania lakn kwa kufuata kanuni za kilimo bora

     MAHALI PA KUPANDA
Maharage hupandwa mahari kwenye muiniko wa mita 400-2000 kutopka usawa wa bahari kwenye udongo usio tuamisha maji


    WAKATI WA KUPANDA
Sehem za umwagiliaji panda wakati wa kiangazi na sehem zenye mvua nyingi zinazo anza mwezi november hadi disemba april na may panda mwezi februali na machi.

    MAANDALIZI
  1. Shamba; lima shamba vizuri na kufukia yale magugu na lima kufuatana na mwinuko wa ardhi
  2. mbegu; Andaa mbegu bora mapema kulingana na chaguo lako
  3. mbolea;andaa mbolea kilo 75 DAP au 150 mijingu kilo 50 TSP na CAN  kwa ekari 
     KUPANDA

Maharage yanatakiwa kupandwa eneo lenye unyevu wa kutosha weka ulefu wa sentimita 2.5 hadi 3 na fukia vizuri na hakikisha mbolea aigusani na mbegu kuepusha kuunguza mbegu.

na kwa maharage madogo ni kilo 25 had 30 kwa hekari na maharage makubwa ni kilo 40 48

  • kwa maharage pekee panda sm50 kati ya mstari na mstari na sm10 kati ya shina na shina 
kwa kilimo mseto panda mahindi  sm75  mstari na mstari na sm60 shina na shina weka mbegu 3 kwa maharage yanayo tambaa na  6 kwa maharage mafupi

  PALIZI
Palizi inatakiwa kufanyika siku 14 baada ya maharage kuota na rudia tena kabla ya kuchanua. unaweza kutumia madawa ya kuuwa magugu kama galex,stomp, dual gold,sateca

 WADUDU WAHARIBIFU
FUNZA WA MAHARAGE
ni wadudu wadogo wanao shambulia mimea michanga ya maharage wanaweza kusabisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100
njia nzuri ya kuwazibiti ni kuwanynyuzia dawa mfano karate 5EC au actelic50 EC ndani ya sku nne hadi 5 baada ya maharage kuota

wadudu wengine ni wanao kula maua kutoboa vitumba na mbegu pamoja na wale wanao bungua ghalani

MAGONJWA
Magonjwa makubwa ni
  • ndui ya maharage
  • madoa pembe
  • kutu
  • magonjwa yanayo sababishwa na bakteria na virusi
punguza magonjwa hayo kwa kupanda mbegu safi, aina znazo vumilia na kutunza shamba na unaweza kutumia madawa kama
kocide,fugulani,Bayleton  kwa kuzuia magonjwa yanayosababishwa na ukungu na bakteria

  UVUNAJI
Maharage yanatakiwa kuvunwa pale yanapo kauka kuepusha kuoza na kupasuka  na yanapo kauka piga vizuri mbegu zisipasuka au kuruka mbali
pepeta na chambua kuondoa uchafu anika yakauke vizuri kabla ya kuifadhi

 HIFADHI
Ghara au chombo cha kuifadhia lazima kiwe safi  na zuia wadudu kwa kutumia dawa asili na zaviwandani


NOTE; Maharage yanaweza kuzaa gunia 6 hadi 10 ukifuata kanuni bora za kilimo cha maharage

Kilimo Bora cha Nanasi


mmea-wa-Nanasi
Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C.


Utangulizi

Nanasi ni tunda la kitropiki, linapendwa na walaji wengi kwa sababu ya ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma.
Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi.
Hali ya hewa inayofaa kwa ukuaji wa nanasi
Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C.
Udongo unaofaa kwa kilimo cha nanasi
Kwa kilimo cha nanasi chachu (pH) ya udongo inayofaa ni 5.5 hadi 6.0, na hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga usiotuamisha maji. Ingawa nanasi huweza kustawi katika udongo wa aina yoyote ile, udongo wa mfinyanzi haufai kwa kilimo cha nanasi.
Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45. Shamba la nanasi unaweza kulilima kwa sesa (flat-bed) au kwa matuta (furrows).
Kwa sesa: chimba mashimo kwa nafasi ya sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya kila mistari miwili. Weka mbolea kianzio katika kila shimo na upande, hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda. Weka tani 10 hadi 15 za mbolea ya kuku, weka pia viganja 2 vya mbolea ya zizi katika kila shimo.
Upandaji wa mananasi
Zipo aina mbali mbali za ‘mbegu’ (machipukizi/maotea) lakini yale yanayochipua kutoka ardhini hufaa zaidi na hukomaa mapema. Chagua machipukizi mazuri yenye umri mdogo na yenye kulingana kwa ukubwa. Iweke miche kwenye kivuli kwa siku 3 kabla ya kuipandikiza iweze kutoa mizizi haraka. Pandikiza mwanzoni mwa mvua za masika. Nafasi iwe sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya mistari miwili. Pandikiza miche 50,000 katika hekta moja. Chovya miche kwenye dawa ya Diazinon au Fention kwa muda wa dakika 25 kabla ya kuipandikiza ili kuzuia mashambulizi ya wadudu.
Palizi
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu. Katika kilimo cha nanasi magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Matumizi ya viuagugu hurahisisha zaidi palizi ya nanasi ukizingatia kuwa nanasi huwa na miiba katika ncha za majani yake ambazo huchubua ngozi endapo palizi za jembe zitatumika. Njia nyingine ni matumizi ya matandazo (mulch) ya majani au plastiki (plastic mulch) maalum kuzuia magugu.
shamba-la-mananasi
Shamba la mananasi
Mahitaji ya mbolea ya mananasi
Weka mbolea ya NPK gramu 50 hadi 70 kwa kila mche wakati wa kupanda. Weka tena gramu 85 kwa kila mche baada ya miezi 3 na pia miezi 3 baadae.
Wadudu na Magonjwa yanayosumbua minanasi
Nanasi ni zao lisilosumbuliwa na wadudu ama magonjwa mara nyingi. Hii ni faida kubwa sna kwa wakulima wa nanasi! Hivyo endapo patatokea mashambulizi ya wadudu na magonjwa, ushauri zaidi wa kitaalam utafutwe kukabiliana na tatizo husika. Hakikisha unakagua shamba ili kuzuia wadudu kama wataonekana.
Uvunaji wa mananasi
Nanasi huanza kutoa maua miezi 12 hadi 15 baada ya kupanda kutegemeana na aina ya nanasi au maotea ya mbegu yaliyotumika, muda wa kupanda na joto la mahali husika. Kwa kawaida nanasi hukomaa miezi 5 baada ya kutoa maua, hivyo nanasi huchukua miezi 18 hadi 24 kukomaa/kuiva. Katika kilimo cha nanasi, mimea ikitoa maua kwa nyakati tofauti tofauti itasababisha kuvuna kidogo kidogo na kwa muda mrefu. Kwa sababu hiyo ndio maana ni muhimu kupanda kwa wakati mmoja mbegu zenye umri na ukubwa sawa.
Kwa wanaofanya kilimo cha nanasi kibiashara (commercial pinapples production) hutumia kemikali aina ya Ethrel (@ 100 ppm) mwezi mmoja kabla ya kuanza kutoa maua ili mimea mingi iweze kutoa maua kwa wakaii mmoja, angalau 80% ya mimea yote.
Vuna wakati kikonyo cha nanasi kimebadilika rangi kuwa njano ya dhahabu. Kata kikonyo cha nanasi chenye urefu wa sm. 30 kikiwa kimeshikana na nanasi na upunguzie majani ya kichungi chake.
Utunzaji wa mananasi
Hifadhi nanasi katika eneo lenye ubaridi huku kikonyo chake kikielekea juu. Hakikisha unauza nanasi mara tu au siku 2 hadi 3 baada ya kuvuna ili kutunza ubora wake.
mananasi-yaliyovunwa
Mananasi yaliyovunwa

KILIMO BORA CHA CHINESE CABBAGE


UTANGULIZI
Chinese cabbage ni moja kati ya mazao ya mbogamboga inayo limwa sana nchini Tanzania.asili yake ni china na badae likasambaa katika nchi za Ethipia,south africa,zimbabwe na Tanzania.


HALI YA HEWA
JOTOLIDI;Chinese cabbage linastawi na kukua vizuri kwenye maeneo yenye jotolidi 18 hadi 22oc
Unyevunyevu; chinese cabbage ni zao linalo tegemea umwagiliaji hivo  linaitaji maji mengi wakati wa ukuaji.
Udongo;chinese cabbage linakua vizuri kwenye udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha
PH; 5.5 hadi 7.6
KUANDAA SHAMBA
Udongo unatakiwa utifuliwe vizuri kabla ya kupanda unaweza kutumia jembe la mkono au machaku na chisel na andaa shamba wiki 6 kabla ya kupanda.
KUANDAA KITALU
Kitalu kinatakiwa kiwe na upana wa mita 1 yan sentimita 100 na urefu wa mita 5 yani sentimita 500. Kitalu kitifuliwe vizuri na kiwe na kingo ili kuzuia maji kutoka nje ya kitalu.kisha panda mbegu kwenye kitalu kwa sm 15 hadi 20 mstari hadi msitari na panda mbegu sm 2 kati ya mbegu na mbegu na fukia sm 1 hadi 2.
KUPANDA
Kwa kupanda moja kwa moja chimba udongo sm 2 hadi 3 kwa kutumia jembe la mkono na panda nafasi ya 30 mstari hadi mstari na 30 mbegu hadi mbegu na fukia sm1 hadi 2.

Na kwakupandikiza hamisha miche inapo fikia urefu was sm 5 na  chagua miche yenye afya na isiwe na magonjwa.
MBOLEA
Kama unatumia mbolea ya ng’ombe, kuku na nguruwe tumia ndoo katika kila kitalu chenye mita 5
Na pia weka mbolea ya kukuzia UREA gram 50 kwa kila kitalu chenye mita 5 pale mmea unapofikia majani matano.
PALIZI
Tumia jembe la mkono kupalilia magugu pale yanapo jitokeza.

MAGONJWA NA WADUDU WAALIBIFU
WADUDU
v  Sota (bagrada bugs)
v  Dudu mafuta(cabbage aphids)
v  Minyoo ya chini(cut worm)
Tumia chemicali za kuua wadudu kama vile ninja, supercorn, wilcron na perfecron  na pia kuondoa magugu pamoja na mimea yenye wadudu  na pia weka shamba safi wakati wote.
MAGONJWA
v  Ubuli unga(powdery meldew)
v  Kuoza kwa mizizi(black rot)
v  Rub root
Zuia kwa kupanda mbegu safi na kuondoa mazao yaliyo athilika na ugonjwa.
KUVUNA
Chinese ukomaa baada ya miezi 3 hadi 4 inategemea na aina
Vuna kwa kung’oa kwa mkono au unaweza kutumia kisu kukata.
 UTUNZAJI
Maisha ya chinese ni mafupi hivyo unatakiwa kusafisha kwa kuosha na pia baada ya hapo unaweza kutunza kwenye friji  ili kuzuia kukauka.

MVIWATA WAIOMBA SERIKALI KUUNDA SHERIA KUWABANA WAFANYABIASHARA WA UFUTA

ufuta  
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mtandao wa Vikundi vya Wakulima nchini (MVIWATA) umeiomba Serikali kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana wafanyabiashara wa zao la ufuta ili wakulima wapate faida ya uzalishaji wa zao hilo.
Maombi hayo yamebainishwa hivi karibuni na Afisa Masoko kutoka MVIWATA, Acquiline Wamba wakati wa warsha ya uboreshaji wa matumizi ya vipimo sahihi katika biashara ya mazao ya kilimo iliyofanyika mkoani Dodoma.
Bi. Acquiline amesema Serikali inatakiwa kuchukua hatua madhubuti kwa kuweka sheria kali dhidi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwani Sheria hizo  zitawasaidia kuwapa maelekezo ya namna ya kuweka vipimo sahihi kwenye mazao ili kuongeza ushindani kwenye biashara.
“Wafanyabiashara wasio waaminifu wamekua ni chanzo cha kukwamisha soko la nje kwa kupeleka mazao yenye uchafu nje ya nchi, hii sio sahihi ndio maana tunaomba Serikali itusaidie” alisema Bi. Acquiline.
Aliongeza kuwa ili kuboresha soko la nje la zao la ufuta Serikali inatakiwa kuhakikisha panakwepo na mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mazao yanayoenda nje ni masafi.
Aidha, Bi. Acquiline alifafanua kwamba kuwabana wafanyabiashara wa zao hilo kutumia vipimo sahihi vya mizani itasaidia kukomesha  wafanyabiashara wanaowaibia wazalishaji hao kwani lengo halisi la kuweka mizani ni kupunguza tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kuongeza mchanga kwenye zao la ufuta kwa lengo la kuongeza uzito.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Danford Chisomi alisema kuwa Halmashauri bado haijawa na mizani ya mazao kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo aliahidi kushiriki katika kutatua changamoto hizo.
“Halmashauri itatafuta nafasi ya kuweka mizani pamoja na kuunda sheria mpya ndogondogo za kuwadhibiti wafanyabiashara wa zao hilo”, alisema Chisomi.
Akiongea katika warsha hiyo, mzalishaji wa ufuta Wilayani Bahi, Fikiri Bernard, alisema kukosekana kwa mizani katika Halmashauri hiyo kunaathiri moja kwa moja jitihada za wazalishaji pamoja na kusababisha upotevu wa mapato kwa halmashauri hiyo.
“Vipimo vingi vinavyotumiwa na wafanyabiashara huwa haviko sahihi kwa sababu havijahakikiwa na Mamlaka husika kwa matumizi ya biashara hivyo wafanyabiashara wamekua wakitumia mwanya huo wa ukosefu wa mizani kuweka vipimo vyao wenyewe vya kununulia zao la ufuta,” alisema Bernard.
Ameongeza kuwa Halmashauri hiyo imekua ikipoteza mapato mengi kwa kushindwa kukusanya ushuru kutokana na kuwepo kwa wafanyabiashara wasio waaminifu wanaopenyeza mazao yao bila kulipa ushuru.
Vile vile, mkulima huyo ameiomba Halmashauri kutenga vituo mbalimbali vya kupimia mazao kwa ajili ya kupata vipimo sahihi vya mazao ili kuepuka kuwaibia wakulima.

KILIMO BORA CHA ALIZETI


Alizeti ni zao mojawapo kati ya mazao muhimu yanayotoa mbegu za mafuta. Hutoa mafuta kati ya asilimia
40 – 45 na mashudu yake ni chakula cha mifugo. Alizeti huvumilia ukame na hulimwa kwa ajili ya biashara
na matumizi ya nyumbani. Wakulima huvuna kiasi kidogo, kati ya gunia 3 – 5 kwa hekta. Hivyo kwa
mavuno mengi na bora, mkulima anashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
Kuandaa Shamba
Unashauriwa kutayarisha shamba lako mapema kwa kukatua ardhi na kulainisha vizuri. Samadi yaweza
kuchanganywa vizuri na udongo wakati wa kuandaa shamba.
www.ariuyole.go.tz
Wakati wa Kupanda
Upandaji wa alizeti hutegemea sana hali ya hewa ya eneo husika.
Maeneo yenye mvua nyingi alizeti huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Januari mpaka katikati ya
mwezi Februari.
Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa mwezi Desemba hadi Januari.
Kiasi cha mbegu na upandaji
Kiasi cha kilo 3 – 4 za mbegu zinatosha kupanda eneo la ekari moja.
Panda mbegu 3 – 4 katika kila shimo moja kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka mstari hadi mstari na sentimita
30 kutoka shimo hadi shimo. Shimo la mbegu liwe na kina cha sentimita 2.5 – 5.
Wiki mbili baada ya kuota, punguza miche katika kila shimo na kubakiza mche mmoja.
Kiasi cha mbolea
Mbolea zinazofaa kwa kilimo cha alizeti ni zile za kupandia na kukuzia hasa kwenye maeneo yasiyo na
rutuba.
Wakati wa kupanda tumia nusu mfuko kwa ekari moja ya mbolea ya kupandia na mfuko mmoja kwa ekari
moja ya mbolea ya kukuzia kwa kuigawa mbolea hiyo mara mbili. Nusu ya kwanza iwekwe wakati wa
kupanda na nusu ya pili iwekwe wiki mbili baadaye.
Wakati wa kuweka mbolea angalia isigusane na mbegu au mche wa alizeti kwani huunguza.
Palizi
Alizeti hukua taratibu katika wiki chache za mwanzo. Hivyo unashauriwa kupalilia mapema ili kupunguza
hasara. Katika maeneo yaliyo na magugu machache, palizi moja tu inatosha. Vile vile maeneo yenye upepo
mkali, wakati wa kupalilia inulia matuta ili kuzuia kuanguka.
Wanyama na wadudu
Ndege
Alizeti hushambuliwa sana na ndege ambao huweza kuteketeza hadi asilimia 50 ya mazao shambani.
Kuzuia
- Usipande alizeti karibu na msitu/pori
- Vuna mapema mazao yako mara tu kichwa kinapobadilika rangi na kuwa manjano
- Panda alizeti kwa wingi katika shamba moja
- Amia ndege kwa mutumia sanamu, makopo na ua kuweka watu ingawa ni gharama.
Funza wa vitumba (American bollworm)
Funza huyu hutoboa mbegu changa kuanzia mara tu vitumba vya maua vikifunguka mpaka karibu na
kukomaa kwa mbegu.
Kuzuia:
- Tumia dawa yo yote ya kuulia wadudu inayopatikana katika eneo lako.
Magonjwa
Alizeti hushambuliwa na magonjwa yakiwemo madoa ya majani, kutu, kuoza kwa mizizi, shina, kichwa na
kushambuliwa na virusi.
www.ariuyole.go.tz
Kuzuia:
- Tumia kilimo cha mzunguko wa mazao
- Panda mbegu safi zilizothibitishwa na wataalamu
- Choma masalia ya msimu uliopita
Uvunaji
Unashauriwa kuvuna alizeti mara tu inapokomaa ili kupunguza hasara ya kushambuliwa na ndege. Alizeti
iliyokomaa kichwa hubadilika rangi toka kijani kibichi na kuwa njano. Kata vichwa na kuvianika juani ili
vikauke vizuri.
Piga piga vichwa ili kutoa mbegu za alizeti, kisha upepete na kuendelea kuzianika ili zikauke vizuri.
Utafiti unaonyesha kuwa mkulima anaweza kupata magunia kati ya 10 -12 kutoka katika ekari moja.
Kwa Mawasiliano zaidi wasiliana na:
Taasisi ya Utafiti Uyole,
Kitengo cha mbegu za Mafuta
S.L.P. 400
MBEYA
Simu: 025 2510062
Fax: 025 2510065
Barua pepe; ariuyole@iwayafrica.com
website: www.ariuyole.go.tz
www.ariuyole.go.tz
Mkulima jembe 0756 483174

Matumizi ya Mbolea

Matumizi ya Mbolea
Matumizi ya rutuba kwenye udongo
}  Mimea huchukua /huondoa virutubisho kutoka kwenye udongo kupitia kwenye mizizi.
}  Virutubisho vinavyotumika na nafaka kama (ngano, mahindi, mpunga, n.k) inageuzwa kuwa punje na sehemu kwenye masalia ya mimea.
}  Kwa upande wa mahindi ,kwa kila kilogramu 1000 ya mazao yanayozalishwa ,Kilogramu 35 za virutubisho zinakuwepo kwenye mazao na kilogramu 37 kwenye masalia  ya mimea.Jumla ya kilogramu 72 za virutubisho zinakuwa zimetoweka.
}  Iwapo kwenye hekta moja umevuna tani 4 =kilogramu 4000, kiasi cha kilogramu 288 ya virutubisho itakuwa imeondolewa kutoka kwenye udongo.
}  Kama hivi virutubisho havitarudishwa, rutuba ya udongo itapungua .Kwa miaka kadha wa kadha, mavuno kutoka kwenye udongo wa aina hiyo inashuka.
}  Kwa udongo kubaki na rutuba, ni vizuri kurudisha virutubisho vilivyo potea wakati wa mavuno ya mazao.
Kutoka: IFDC: Estimated removal of nutrients from the soil by Grains (kg nutrients/ Mt grain harvested)
Mimea
Nitrojeni
(N) 
Fosforasi
(P2O5)
Potasiamu
(K2O)
Jumla 
Mahindi
18
10
7
35
Ngano
20
8
5
33
Mpunga
14
6
4
24
Kutoka: IFDC: Estimated removal of nutrients from the soil by          Residue (kg nutrients/ Mt straw harvested)
Mimea
Nitrojeni
(N) 
Fosforasi
(P2O5)
Potasiamu
(K2O)
Jumla 
Mahindi
10
6
21
37
Ngano
6
3
22
31
Mpunga
9
2
24
35
Virutubisho ni nini?
}  Mimea inahitaji virutubisho kumi na sita ili kukua na kutoa maua na mazao mazuri.
}  Virutubisho hutumika kama lishe ya mimea.
}  Virutubisho vitatu hutoka hewani mambavyo ni: kaboni, oxijeni na hydrojeni.—Ikichangia asilimia 93 ya mahitaji ya mmea.
}  Wakati virutubisho vitatu hutokana na hewa na maji .
}  vingine kumi na tatu hupatikani kupitia udongoni.Hupatikana kupitia mizizi na kutumika na mimea.
Madaraja ya virutubisho vya mimea
}  Kwa kuzingatia kazi zake na kiwango kinachohitajika na mimea kwa ukuaji kumetokea madaraja yafuatayo:
  1. Virutubisho vya msingi au vinavyohitajika kwa wingi
}  Nitrojeni (N), Fosforasi (P), Na potasiamu (K) ndivyo vinahitajika mno na mimea kwa ukuaji na kwa kiwango kikubwa.
  1. Virutubisho vinavyo hitajika kwa kiasi
}  Kalsiamu (Ca), salfa (S), and magnesiamu (Mg) huhitajika kwa kiasi kidogo na mimea lakini vinaumuhimu mkubwa.
3. Virutubisho vinavyo hitajika kwa kiwango kidogo
}  Virutubisho saba vilivyobaki ambavyo ni: Chuma (Fe), Kopa (Cu), zinki (Zn), boron (B), manganese (Mn), clorini (Cl), and molybdenum (Mo) huhitajika kwa kiwango kidogo sana.
Dalili kutokana na ukosekanaji wa vitutubisho Dalili kutokana na ukosekanaji wa vitutubisho
Virutubisho vya msingi
}  Nitrogen (N), phosphorus (P), and potassium (K) ni vya aina tatu.
 Kutokana na makubaliano ya vigezo vilivyowekwa na viwanda vya mbolea, virutubisho vya muhimu /msingi vimekubalika kama; N (nitrogen), P2O5 (or phosphorus pentoxide for phosphorus), and K2O (or potassium oxide for potassium
1.       Nitrogen
2.       Nitrojeni ndio kirutubisho cha muhimu kwa aina kubwa ya udongo unaonjesha mapungufu.
3.       Ijapokuwa Nitrojeni inahitajika katika ukuaji wa awali wa mimea ,inahitajika kwa kiwango kikubwa wiki ya 3-4 kutoka zao kuota haswa kwa mazao ya nafaka kama ngano,mahindi ,mpunga n.k.
4.       Nyongeza huwekwa baadae wakati mimea inapacha ,kutoa maua au karibu na kukomaa.
5.       Kwa hiyo Nitrojeni huwekwa kama mara 2-3 kwenye mimea
Dalili za mapungufu ya  Nitrojeni
}  Kama nitrojeni imekosekane kwenye udongo:
}  Ukuaji wa mmea huwa taratibu.
}  Mmea hudumaa na majani kuwa ya njano.
}  Mmea hukomaa haraka kupunguza mavuno.
}  Upungufu wa  Nitrojeni
}  Mapungufu ya nitrojeni hupatikana karibu kila eneo lakini zaidi kwenye udongo wa kichanga, udongo wenye kiwango kidogo cha mboji, au udongo uliolimwa mfululizo kwa miaka mingi.
}  Aina ya mbolea inayotumika sana kusambaza nitrojeni ni mbolea ya Urea,SA,CAN
Mbolea
Virutubisho %
N:P:K
Hutumika haswa
Urea
46:0:0
Kukuzia
Calcium Ammonium Nitrate(CAN)
27:0:0
Kukuzia
Sulphate of Ammonia(SA)
21:0:0
Kukuzia
Di -ammonia Phosphate (DAP)
18:46:0
Kukuzia
N:P:K
17:17:17,20:10:10
Kukuzia
2.  Fosforasi
}  Fosforasi hupitia kwa mmea kwa kutumia mbolea za fosfeti,mara nyingi hutumika kupandia.
}   Fosfati ni muhimu sana kipindi cha awali cha ukuaji wa mmea  kwa kuuwezesha mmea kuwa na mizizi mingi na kuwa na nguvu ya kuushikilia mmea kwenye udongo.
}  Mizizi yenye afya huufanya mmea kupata vitutubisho kwenye udongo.
Dalili za mapungufu ya fosforasi
}  Upungufu wa Fosforasi Huonekana haswa kwenye udongo wenye tindikali au ulio na kalsiuamu /chokaa kwa wingi.
}  Mapungufu ya fosforasi kwenye udongo huufanya mmea kuwa :
}  Dhaifu kutengeneza mizizi.
}  Kuanguka kwa mmea.                                                        
}  Kudumaa kwa mmea na mavuno kidogo.
}  Mfano wa mbolea zenye Fosforasi ni: SSP (0-16-0),TSP (0-46-0),DAP (18-46-0)
3.       Potasiamu
}  Potasiamu ni aina ya tatu ya kirutubisho cha msingi kinachohitajika na mimea.,barafu ,wadudu na magonjwa na kusaidia usafirishaji wa virutubisho vingine kuanzia kwenye mizizi hadi sehemu nyingine ya mimea.
}   Inasaidia kujaza punje,mbegu.
}  Mbolea zote zinazosambaza Potasiamu hutumika kupandia ila kwenye udongo wa kichanga inashauriwa kuwekwa mara mbili wakati wa kukuzia.
Dalili za mapungufu ya potasiamu
}  Majani huonjesha dalili ya kama kuungua kwenye njia ya jani na kuendelea.
}  Kwa lugha ya kitaalamu huitwa “chlorosis.”
}  Mimea inakuwa dhaifu kwa mashambulizi ya magonjwa.
}  Salfa inahusika kwenye protini ya mmea ,husaidia vimengĂ©nyo na vitamini vinavyohitajika kwenye kutengeneza ukijani unaosaidia kuakisi mwanga wa jua
.
}  Sulfur inapatikana kwenye vitu vingi Kama vile gypsum na mbolea kama ammonium sulfate, SSP and TSP.
Matumizi ya mbolea Asilia/Mboji
}  Mboji ni urutubishaji wa asili ambao hujirudia wenyewe kwa mtindo wa kuoza. Utengenezaji wa  mboji ni njia ya kurudisha rutuba ya asili kwenye udongo kwa njia ya kuozesha vitu.
}  Matokeo yake ya mwisho ni kutoa mbolea asili ambayo ni rahisi kutengeneza, na ambayo ina virutubisho vingi bila gharama
}  Mboji huwa ni faida kutokana na uozaji wa asili ambao hutokea kwenye vitu vyote vyenye uhai.
}  Vitu vyenye uhai ni kama vile majani, miti na mabaki ya vyakula.wakati wa uozaji vitu hivi hugeuka na kuwa rutuba inayorudia kwenye udongo
}  Udongo hupoteza virutubisho baada ya kutumika sana .
}  Matumizi ya mbolea za asili nayo ni mazuri katika kuendeleza udongo kwa ajili ya ukulima.
}  Pia mbolea za asili/mboji husaidia kuzuia mmomonyoko wa ardhi
}  Inaruhusu mmea kupata rutuba kwa urahisi kutoka kwenye udongo.
}  Pia hufanya mmea usiwe dhaifu kwahiyo huzuia wadudu waharibifu kushambulia mmea.
}  Mboji hutoa virutubisho kwa muda mrefu kwasababu ya uendeleaji wa kuoza polepole.
}  Madini yaliyopo katika mboji husaidia kuyeyusha madini mengine yaliyo kwenye udongo,
}  Hufanya madini yenye rutuba yapatikane zaidi kwa mimea. Madini hayo huimarisha sehemu laini za mizizi na hivyo kuipa mizizi uimara wa kuweza kupata maji na virutubisho kwa njia ya mizizi
Hitimisho
}  Mbolea ni kitu muhimu sana katika udongo kwa sababu mazao huitaji virutubisho katika udongo na baada ya udongo kutumika kwa muda mrefu , virutubisho hupotea.
}  Kuvirudisha virutubisho, mbolea inahitajika inaweza ikawa ya chumvichumvi au ya asili hii hutegemea na udongo uliopo katika sehemu hiyo.
}  Kila sehemu ina udongo wa aina yake na unahitaji virutubisho vya aina yake kwa wingi au kiwango kidogo.
}  Kwa hiyo uwekaji wa mbolea katika udongo lazima utumie utaalamu ambao mkulima amepata kutoka kwa wataalamu wa kilimo au uzoefu.

Fahamu mbinu za kuongeza thamani nyama

  Safari ya kuongeza thamani nyama ya mifugo huanzia shambani kwa usimamizi wa ufugaji na uzalishaji. Lishe bora ni muhimu kwa wa ufugaji ...