MTAALAMU APATIKANA KILIMO CHA VITALU (GREEN HOUSE), TANZANIA SASA NI NEEMA.

Sasa Tanzania imehamasika na kilimo cha vitalu bandani (Green house farming) baada ya Mtaalamu na Mshauri (Expert) wa masuala ya kilimo kupatikana na kusema yuko tayari sasa kushirikiana na watanzania katika kilimo hiki ikiwemo kutoa ushauri wa kitaalamu na elimu juu ya kilimo.
Akizungumza na tovuti hii, Bw.Daudi Ally Kambanyuma ambaye ni mwalimu, mshauri, Msomi na mtaalamu wa masuala ya kilimo ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika masuala ya kilimo na pia ni Mkuu wa shule ya Sekondari Chita iliyopo wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Katika mahojiano na tovuti hii Mwl. Kambanyumba aligusia masuala ya upandaji na matatizo ya wadudu kuharibu mazao kama changamoto inayo wakumba wakulima wengi wa vitalu na kuelezea kazi yake maalumu ya kutoa ushauri kwa wakulima huku akibainisha uzoefu wa utaalamu wake na maeneo mbalimbali aliyofanya kazi hiyo na jinsi wakulima wa mazao hayo walivyonufaika. “Sasa ni wakati wetu watanzania kuamka na kuwekeza katika kilimo cha vitalu bandani maana ardhi tunayo na yenye rutuba, Suala la Mazao ya baadhi ya wakulima kuharibika yanatokana na wakulima kutopata wataalamu ambao watafanya tafiti za uchambuzi wa udongo (Soil Analysis) wa eneo husika hatua ambayo ni ya kwanza kabisa inayokupa uhakika wa unacho panda, Nimefanya kazi hii kwa muda mrefu na changamoto zake siku zote ni hii ya wakulima kutozingatia hili” alisema Mwl. Kambanyuma.
Aidha Mwl. Kamba nyuma amekuwa akifanya kazi za kitaalamu na ushauri wa kilimo na taasisi na mashirika mbalimbali kama Rack Farm, Intermon oxfarm Msowero na Lupalilo Ventures Ruvu Farm. Pia aliwaomba watanzania kutilia mkazo na kuwekeza katika kilimo hiki kwa kusema kuwa kilimo ni uti wa Mgongo wa mtanzania na kubainisha kuwa si lazima mtu kuwa na eneo la hekari kubwa ndio afanye kilimo hiki, La hasha! bali hata eneo dogo lililoko katika nyumba yako unaweza kutumia kwa kilimo hiki bila bugudha na kupata mavuno mazuri na pesa nyingi bila kuhangaika kuwaza kupata eneo la shamba. “Baadhi ya Watu wanadhani na kuogopa kuwa wataingia gharama kununua eneo la shamba hekari nzima kwaajili ya kilimo hiki, sivyo kabisa ukiwa na kaeneo kako kadogo katika nyumba yako na unalima na kuvuna unapata pesa bila taabu yoyote, tugutuke watanzania maana kilimo ndicho uti wa mgongo kwani nchi nyingine kama Kenya wamewekeza zaidi katika kilimo hiki” aliongeza.
Hata hivyo pamoja na kumpata mtaalamu huyu wa kilimo hiki Njia mpya bado tunahitaji wataalamu wengi zaidi ili kufikia kila kona ya Tanzania ili kuweza kuwahudumia wakulima wote kwa karibu kutokana na hitaji kubwa la wataalamu wanaohitajika. Kama wewe au rafiki yako ni Mtaalamu au Mshauri wa kilimo hiki Tafadhali wasiliana nasi kupitia namba zetu au tovuti yetu hapo chini.

Comments

Popular Posts