Mpenzi msomaji wa blog hii leo napenda nikuletee kitu kingine tofauti
kidogo na ambacho blog nyingi za kilimo, ntapenda kukuletea baadhi ya
vifaa ambavyo hutumika shambani hivyo wewe kama mkulima, mdau wa kilimo
au mtu yoyote na ungependa kufahamu zaidi kuhusu mashine na vifaa
vinavyo tumika shambani usisite kuwasiliana na mimi kwa kubofya hapa.
TRACTOR |
Tractor ni moja kati ya mashine ambazo ni maalufu sana, bila shaka
kila mmoja ameshawahi kuliona, wengi wanaweza wakawa hawafahamu nini
hasa kazi za tractor.pia tractor hutofautiana kwa umbile, wats na hata
ubora.
- hutumika kama usafiri kwa mizigo na watu pia
- hutumika kama chanzo cha umeme sambani mfano mashine za kusaga zinaweza kuunganishwa na kufanya kazi
- hutumika kuunganisha vifaa tofauti tofauti vinavo tumiwa shambani mfano plough.
jifunze zaidi kwa kubofya hapa
𝐓
HALLOW |
hiki kinaweza kua kifaa kigeni kwa watu ambao hawafahamu mambo ya shamba
hasa, lakini ni kifaa maarufu kwa wakulima. hallow hua na disc ya
maumbo tofauti na hutumika baada ya disc plough. kazi yake hasa ni
- kusawazisha shamba.
- kuchanganya udongo na mbolea
- kuruhusu udongo kua katika hali nzuri inayo ruhusu, maji na hewa kupenya ndani ya udongo.
|
corn seeder nikifaa ambacho hutumika kupandia mahindi, kifaa hiki hua
hakitumii umeme au mafuta ili hufanya kazi kwa kuunganishwa katika power
tiller. hua si kukubwa sana kwa umbo na nirahisi kuhamishika na hata
kusafisha.
FARM TRAILER |
Hiki ni kifaa ambacho ni maalufu sana, farm trailer ni tela kama
inavofahamika na wengi. kazi yake kubwa ni kubeba mizigo, mazao na hata
watu. na hua maalumu kwaajili ya matumizi ya shamba na hata shuguri
zingine za kiuchumi na kijamii pia. na huvutwa kwa kutumia tractor.
jifunze mambo mengi zaidi kwa kubofya HAPA
MAIZE DRYER |
Maize dryer kama inavo itwa hua nikifaa maalumu ambacho kimetengenezwa ili kukausha maindi baada ya kuvunwa.
BOOM SPLAYER |
Boom sprayer hua ni kifaa ambacho kimetengenezwa maalumu kwa ajili ya
kupulizia viuagugu au viua dudu shambani. na hua na mfano kama splayer
zinazo tumika kiupulizia dawa za kuua kupe kwa wanyama, ila tofauti yake
ni kwamba boom sprayer hua ni kubwa sana na huvutwa kwa kutumia
tractor. hivyo utumika kupulizia dawa katika mashamba. boom spalayer hua
na ukubwa tofauti tofauti mfano zingine huchukua 300 liters, 600 liter
n.k
COMBINE HARVESTER |
Hii ni mashine ya shamba na hua na umbo kubwa mfano wa scaveter na
hutumika katika kuvuna mazao mbali mbali mfano mpunga na ngano.
DISC PLOUGH |
Disc plough pia hufanya kazi kwa kuunganishwa katika trekta, hutumika katika kuvunjavunja udongo ulio katika hali ngumu.
POWER TILLER |
Hii pia nimashine maalufu sana, imekua ikitumika katika maeneo mengi tofauti tofauti na hua nakazi nyingi kama ilivyo trekta
- usafirishaji
- hutumika kulima
- chanzo cha umeme pia
Bila shaka umeza kufahamu baadhi ya vifaa vinavyo tumika shambani
na kazi zake, nitumaini kangu umeapata uelewa na ufahamu wa kutosha juu
ya vifaa hivyo.
japo imekua nichangamoto sana kwa wakulima jinsi ya kupata vifaa hivyo kutokana na upatikanaji mdogo wa vifaa hivyo.
hivyo wewe kama muuzaji au msambazaji wa vifaaa mbalimbali ni fursa
kwako sasa kuweza kuweza kuonesha au kujulisha wa kulima jinsi ya
kuvipata vifaa hivyo kupitia kwako.
WASILIANA NA MIMI MOJA KWA MOJA ili tuweze kulisukuma gurudumu la maendeleo ya kilimo.
Thy
ReplyDelete