Sunday, February 26, 2017

KILIMO NI MAPINDUZI MAKUBWA YA UCHUMI,HABARI PICHA

Image result for kilimo cha greenhouseImage result for kilimo cha greenhouse


Image result for kilimo cha greenhouse

KILIMO CHA KISASA CHA GREENHOUSE (BANDA KITALU) NA FAIDA ZAKE​


[​IMG]

Green Agriculture

Ndugu Msomaji karibu tena leo tujuzane kuhusu banda kitalu yaani Green house 
Nini Maana ya Green House?
Green house ni hali nuai(artificial environment) ya kimazingira iliyotengenezwa kwa ajili ya uhitaji fulani wa kitu(zao) ambacho hakiwezi/kinaathirika kikiishi katika mazingira halisia au hakiendani na mazingira halisia na ningependa ujue ya kuwa green house sio ile nyumba bali ni ile hali ya ndani inayotengezwa na ile nyumba.Hali mbali mbali zinaweza kutengenezwa na green house kama maeneo ni ya joto sana na unataka kulima mazao yanayostawi sehemu za baridi unaweza kutengeneza green house ambayo italeta hali ya baridi na pia kama upo maeneo ya joto na unataka kulima mazao mazao yanayostawi sehemu za baridi unaweza kutengeneza green house kwa ajili ya kuleta hali ya baridi na ukafanya kilimo chako bila shida yoyote tena kwa ufanisi mkubwa
NOTE: katika ununuzi wa materials hakikisha ununua kwa mtu mwenye uelewa ili akupe material inayoendana na eneo lako ili upate matokeo mazuri hasa nylon cover kwa nchi za tropical ni ile yenye standard ya 200micron

Greenhouse(Banda Kitalu)
Hii ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa. Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.

Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi za baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse lilipoibuka. Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kitalu ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi. Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti kati yake na zile za nchi za ukanda wa baridi na tofauti yake ni kwenye materilas zinazotumika kutengengenezea hasa polycover tujue kuwa katika dunia yetu kila ukanda una kiwango chake cha mionzi ya jua inayofika eneo husika kwa hiyo green house materilas zinazotumika katika nchi za baridi zina microyn tofauti na zile zinazotumika ukanda wa tropiki mfano kwa tanzania tunatumia polycver yenye 200 micron kuendana na hali ya hewa yetu na usipotumia material ya aina hyo mimea yako itaungua au kutokukua vizuri ndio maana tunashauri ufanye kazi na wataalamu ili upate uhakika wa kile kitu unachokifanya kwa manufaa yetu sote

FAIDA ZA GREENHOUSE

1.Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi,ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.

2.Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya uharibifu wa mazao kama wadudu waharibifu na wale waletao magonjwa kwa mimea.

3.Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.

4.Uwezo wa kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu, ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei za mazao ziko juu na unapata faida kubwa

5.Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti kwani wakati mwingne dawa hazitumiki kabisa kwenye green house.

6.Matumizi bora ya maji kwani drip irrigation system ndio hutumika kwenye green house na ina ufanisi mkubwa katika ufikishaji wa maji kwa mimea na hupunguza upotevu wa maji

7.Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili ya kuzoea mazingira ya nje kwanza. wataalamu wa SUA wanafanya sana hii

8.Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (Hydroponic). Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuzi wa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea

MFUMO WA UMWAGILIAJI KWENYE GH
[​IMG]

mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone yaani drip irrigation system ndio unatumika sana katika green house kwani ndio mfumo rahisi na wenye ufanisi mkubwa sio tuu katika kuhakikisha mmea wako unapata maji shahiki bado katika kubana matumizi ya maji pia, katika mfumo huu tunaweza kuweka mbolea moja kwa moja kwenye mfumo wako na mimea ikapata mbolea kwa njia hii (fertigation) mbolea inawekwa kwenye tank la maji lakini hii ni vizuri ukapata ushauri wa kitaalamu ili tukuambie namna ya uwekaji wa mbolea na kiwango cha kuweka 

ARDHI, UDONGO KWENYE GH
[​IMG]

Ni muhimu kapima udongo kabla ya kuwaza kulima pia hata kwenye kilimo hiki cha kutumia green house ni vizuri kupata data za udongo katika mambo yafuatayao kwanza kabisa data za udongo husaidia katika kufanya design ya mfumo wa umwagiliaji ili mimi mtaalamu niweze kukuambia utamwagilia kwa muda gani na baada ya siku ngapi ( irrigaton time and irrigation intervval mfano . mwagilia masaa matatu kila baada ya siku mbili) na calculation zinafanywa kuendana na uhitaji wa maji katika zao lako na uwezo wa udongo wako kubeba maji .

katika green house kuna kitu tunakiita soil develpment yaani ni kuuandaa na kuuongezea udongo rutuba kwa kutumia mbolea asilia na mchanganyiko wa madini mengine ili udongo uweze kuwa na uwezo wa kuupa mmea mahitaji yake lakini ni vizuri kupima udongo ili mtaalamu aweze kujua ni kiwango gani za mbolea na samadi na vitu vingine vinahitajika katika udongo wako ili mazao yaweze kustawi vzr kwa wateja wetu huwa tunawapa offer ya soil test bure ili waweze kumudu gharama katika uwekezaji huu 

[​IMG]


Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha Greenhouse.
Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii.

Tuanze na Marekani, Marekani ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua, Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka.

Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000 hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga, pamoja na nyanya Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo hazilimwi kwingine. Mazao maarufu yanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.

Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse. Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)

Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa nchi ya Israel eneo lake ni kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse.


Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao yanya na tango yanalimwa kwenye green house. Misri 10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote duniani. Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse. Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama Japan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).

AINA ZA GREENHOUSE
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:

1. Aina za Greenhouse kwa kigezo cha sura/umbile (shape)


Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu




kwa hapa kwetu mara nyingi tunatengeneza gh za iana tatu ambazo zinafanya vizuri sana kama slant roof green house kama ilivyo kwenye picha hapa tunatumia mbao(miti) au chuma

[​IMG]a)Quonset Greenhouse

[​IMG]

b) Saw tooth type

[​IMG]


iii. c)Even span type greenhouse


iv. d)Uneven span type greenhouse


2.Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi


a)Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)


i b)Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)


3.Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)

a)Greenhouse za miti (Wooden framed structure)

i b)Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)

Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma

4. Aina za Greenhouse kwa kigezo aina ya zana za ufunikaji (covering types)

a)Greenhouse zinazofunikwa kwa zana za Vioo (glass)- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndani greenhouse

b)Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya nylon (polycover)

5. Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa

Katika green house unaweza kulima mazao mengi hasa ya mbogamboga na matunda ambayo yana soko zuri na uapatikanaji wake ni adimu sana , kwa kuwa kilimo cha gh ni uwekezaji bora kwenye kilimo 

ORGANIC FARMING(KILIMO HAI)
hiki ni kilimo ambacho huhiji kutumia kemikali zozote wala mbolea za viwandani yaani ni kilimo asili, kwa nchi za wenzetu mazao ya kilimo hai yana bei mara kumi zaidi ya mazao ya kilimo cha kawaida kwani kukua kwa teknolojia na uharibifu wa mazingira bidhaa za kilimo zimekuwa zikitumia kemikali nyingi sana ambazo huathiri afya ya binadamu moja kwa moja au madhara huonekana baadaye sasa ukiwa na green house utaweza kufanya kilimo hiki na familia yako ikatumia chakula safi ambacho hakijawekwa chemikali

kwa mahitaji ya kutengenezewa green house ya kisasa kwa bei nafuu wasiliana na mimi pia baada ya kukutengenezea structure yako hatutakuacha hivi hivi ila tutakupa mtaaalamu wetu ambae ni Agronomist Boniphace Mwanje(0719880905) aliebobea kwenye utaalamu mbegu,mbolea,madawa na utunzaji wa mimea na huduma nyingne za aina zote za umwagiliaji, kupima udongo, kuchora na kupanga ramani za mashamba na taasisi au kampuni

MKULIMA JEMBE HILI NI KITEGA UCHUMI CHAKO KILIMO NI BIASHARA

                                             LIMA   SASA 

KILIMO BORA CHA VITUNGUU SAUMU

  UTANGULIZI 

Vitunguu saumu ni jamii ya vitunguu maji asili yake ni nchi za Asia lakin pia usitawi katika nchi za kitropik kwa hapa tanzania ustawi katika mikoa ya singida,Arusha,Iringa na Mbeya. pia utumika kama kiungo cha chakula dawa kwa binadamu na wanyama pia na pia utumika kutengeneza mafuta pia harufu yake kali ufukuza wadudu waalibifiu shambani.
hivyo shamba la vitunguu swaumu haliwi na wadudu wa halibifu sana ukiringanisha na mazao mengine.

  AINA YA VITUNGUU SAUMU
Kitaalam bado aijafahamika kunaaina ngapi za vitunguu saumu lakini kuna aina mbili ambazo zinalimwa hapa nchini ni Kienyeji na kisasa.
Aina ya kisasa uzaa vitunguu vikubwa venye ngozi nyeupe napia aina ya kienyeji uzaa vitunguu vyekundu vyenye harufu kali sana na pia havia haribiki mapema ukilinganisha na vya kisasa
vitunguu saumu havizai mbegu halisi kwa hyo uzalishwa kwa kutumia vikonyo vyake
  
     TABIA YA MMEA
Tunguu la vitunguu saumu utokana na vikonyo na hiv vikonyo ndo vinatumika kama mbegu

HALI YA HEWA
Vitunguu saumu ulimwa kiasi cha mita 1800 au zaidi kutoka usawa wa bahari na mvua kiasi cha mm 1000 au zaidi na joto kiasi udongo tifutifu na mnyevunyevu na usio tuamisha maji ndio unafaa kulima vitunguu saumu.
KUANDAA SHAMBA
Andaa shamba mapema lima na akikisha udongo ni tifutifu na pia  unaweza kutuengeneza matuta kwaajili ya kupanda weka samadi shambani wiki 2 kabla ya kupanda au wakati wa kupanda pandia TSP kilo 40 kwa eka au kilo 100 kwa hekta
KUPANDA
 Panda vikonyo vilivo anza kuchipua vilivo safi na visivyo na dalili ya ugonjwa kwa nafasi ya sm 5 kikonyo hadi kikonyo na sm 15 mstari hadi mstari.

PALIZI NA MATUMIZI YA MBOLEA
Palizi ya kwanza ifanyike mapema mara tu magugu yanapo tokeza wakati vikonyo vimesha chipua  na baada ya palizi ya kwanza weka mbolea ya kukuzia CAN au UREA. CAN kiasi cha kilo 75 kwa eka au 190 kwa Hekta au UREA kiasi cha kilo 40 kwa eka na 100 kwa hekta na palilia mara mbili au zaidi ili kuweka shamba katika hali ya usafi
unaweza kupulizia dawa ya kuua magugu endapo vitunguu vimeshaota  kama vile Bromoxynil ambayo uua majani mapana na fusilade uua nyasi.

MAGONJWA
  • fusari muozo-unasababishwa na ukungu katika majani au miziz na pia unaweza kudhibiti kwa kuchoma masalia ya mimea baada ya kuvuna
  • kutu ya majani-mmea unakua na vinundu vya ukngu vyenye rangi ya kahawia kama kutu katika majani tumia dawa ya ukungu  kama fungaran nabayfidan na nordox ili kuzuia
  • kuoza kwa vitunguu-ukungu wa rangi ya blue ufunika vitunguu na usabibisha vitunguu kuoza na utokea gharan vuna kwa uangalifu ili kuepusha michubuko  na hakikisha store ni safi
  • baka jani-vidonda vidogo hutokeza katika majani na badae vinakua vikubwa epuka kumwagilia maji mengi kupita kiasi na tumia mzunguko wa mazao
  • muozo shingo-shingo kuonyesha dalili ya majimaji weka mbolea ya ntrogen kama CAN,UREA na mwagilia maji ya kutosha hasa vinapo elekea kuvunwa
 WADUDU
Wadudu kama chawa wekundu nondo na funza  wanakata miche na mizizi tumia dawa ya karate,selecron,novthin,dursban hutumika kuuwa wadudu

KUVUNA
Vitunguu uvunwa vikifika miezi 6-7 baada ya kupanda majani na mashina unyesha dalii ya kukauka viache vitunguu shambani mpaka majani yanap kauka kabisa  ngoa kwa mkono au jembe na pia kua muangalifu ili kuepusha kuchubua vitunguu
  

KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO

                                                             UTANGULIZI

Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. viazi husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300 hadi 2700 juu ya usawa wa bahari. hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano.
viazi mviringo vina virutubisho  vingi mfano vitamin, protin,madini na maji


           SIFA ZA MBEGU BORA ZA VIAZI
  • Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja
  • ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi zaidi ya manne
  • zisiwe na wadudu pamoja na magonjwa
  • zitoke katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ukungu na mnyauko
  • zenye ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la kuku
  
 mfano wa viazi mviringo

AINA BORA YA VIAZI MVIRINGO
Kuna aina nyingi sana ya viazi mviringo lakini hapa nitataja aina ambazo nazifahamu na ni bora
kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo uyole
  • baraka 
  • sasamua
  • tana
  • subira(EAI 2329)
  • Bulongwa
  • kikondo(CIP 720050)

      MUDA WA KUPANDA
Viazi mviringo mara nyingi katika maeneo mengi vinapandwa agost hadi september na november hadi december
  Natumia sentimita 60 hadi 75 kutoka mstari hadi mstari na nafasi kati ya kiazi na kiazi ni sentimita 30.

   MBOLEA
Ili kupata mazao mengi kutoka shambani mkulima anashauriwa kutumia mbolea aina ya samadi, mboji, maan mabichi  na za viwandani

kwa mbolea za viwandani tumia kilo 300 au mifuko 6 za mbolea ya TSP kwa hekta moja, ns kilo 300 mifuko 6 za mbolea ya CAN au kilo 400 mifuko 8 ya SA au kilo 175 mifuko 3.5 za UREA.

  PALIZI
Palilia viazi wiki mbili au tatu baada ya kuchomoza. inulia udongo kufanya tuta zuri ili pawepo na unyevu wa kutosha na kufunika viazi kutokana na mwanga wa jua

MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
Ili kuzuia ugonjwa wa ukungu tumia Ridomil.
changanya gram 100 za dawa  katika lita 20 za maji na nyunyuzia mara baada kila wiki mbili au tatu kutegemea na hali ya hewa.
nyunyuzia dawa ya karate kiasi cha mililita 20 mpaka 40 za dawa katika lita 20 za maji ili kuzuia wadudu kama inzi weupe na wengine. Tumia mbinu bora za kilimo kama usafi wa shamba au kilimo mzunguko kama mbinu ya kuzuia magonjwa na wadudu.

KUVUNA NA MAVUNO

Viazi huwa tayari kuvunwa baada ya miezi 3 hadi 5 kutoka kupandamda wa kuvuna unategemea na mda wa kupanda na dhumuni la zao
usiache viazi shamban bila kufunika  kwa nyasi au udongo  kwa mda mrefu

KUHIFADHI
Viazi vya chakula viiafadhiwe kwenye ghara hewa ya kutosha pasiwe na unyevunyevu na joto kali


  
                                         mfano wa chakula kinachotokana na viazi mviringo

NJIA ZA KUZUIA MAGUGU SHAMBAN

Wakulima wengi  hua wanashindwa jinsi ya kupambana na magugu hasa kwneye mashamba makubwa sana. hiyo inapelekea wakulima kulima sana lakini mavuno wanayo pata hayaendani na jinsi walivo lima .

Kuna njia kuu tatu za kuzuia magugu shambani
  •   kutumia kemikal (chemical control method)
  • kibaologia(biological control method)
  • kwa njia ya kawaida( physical control method )


                      KUTUMIA CHEMICAL
hii ni njia kuu ambayo inatumika sana kwa watu wenye mashamba Makubwa na hii njia nitaielezea sana kwa sababu ndo njia nzuri sana kwa watu wenye maeneo makubwa na inawachanganya wakulima wengi sana hivo nitaiweke wazi

kuna aina  mbili za viua gugu(herbicides)
  • viua gugu kabla ya kupanda(pre emergency herbicides)
  • via gugu baada ya kupanda (post emergency herbicides)

           VIUA GUGU  KABLA YA KUPANDA (PRE EMERGENCY HERBICIDES)
hivi ni viua gugu ambavyo vinawekwa shambani ili kuua magugu ya aina yote  hvo ni kua makini sana wakati wa kutumia
kwa sababu unapo weka shamban inaua kila jani ambalo litaonekana shambani
mara nyingi kwa Tanzani hua tunatumia ROUND UP
     Unatakiwa uweke siku 10-14 kabla ya kuanza kutifua shamba

na baada ya hapo masaa 48 baada ya kupanda ni muhimu sana kutumia dawa  hizi kwa mazao ya fuatayo ili kuzuia wadudu waalibifu
mahindi- premagram
maharage -trichlor

  VIUA GUGU BAADA YA KUPANDA (POST EMERGENCY HERBICIDES)
Hivi ni  viuagugu ambavo vinatumika mazao ambapo yamesha kua makubwa
mahindi- grammaxone
maharage- amazon, sabea na bean clean


                                  NJIA YA KAWAIDA YA KUZUIA MAGUGU

hii ni njia ambayo kila mkulima anaifaham japo kua inatumika sana lkn ni njia ngumu sana.
na pia inachukua nguvu na mda mwingi.
  • kung'orea
  • kupalilia kwa jembe la mkono
  • kupalilia kwa trekta
  • na kupalilia kwa kutumia wanyama






  0756 483 174 kwa maelezo zaidi kwa vipindi vya Radio na tv

JINSI YA KUONGEZA RUTUBA KWENYE SHAMBA LAKO

Ili kuvuna mazao mengi lazma udingo unao lima uwe na rutuba ya kutosha ili kusababisha mazao yako kupata virutubisho muhimu kwa ukuaji

zifuatazo ni njia ambazo zitakusaidia mkulima kuongeza rutuba kwenye shamba lako
  usipande mazao ya aina moja kwa mfululizo, hautakiwi kupanda mazao ya aina moja mfano mahindi na mtama kwa kufuliuliza ili kuepusha virutibisho kupotea vyote  na itasababisha magonjwa na wadudu kuwa wengi shambani

usitumie mbolea za kemikali mara kwa mara,hii pia haitakiwi, mbolea za kemikali mfano UREA hua hazitajkiwi kutumika mara kwa mara husababisha alzi kupunguza rutuba mbolea hizi utumika mara moja moja zinapo itajika.

 usipende sana kuchoma shamba, unapo choma shamba unasababisha kuuwa wadudud wanao sababisha kuongeza rutuba kwenye udongo na pia huua uoto asiri.

 zika mabaki ya mazao baada ya kuvuna, unapo vuna mabaki ya mazao mfano mabua yanapo zikwa na kuoza husababisha kuongeza rutuba kwenye udongo husika.

panda mazao ya jamii ya mikunde, pia mazao ya mikunde mfano kunde na maharage husaidia kuongeza naitrogen ambayo inatakiwa sana na mimea hivo rutuba huongezeka

weka mbolea ya samadi ,hii ni mbolea hasiri inayo yani ni kinyesi cha ng'ombe hivo ili kuongeza rutuba inabidi uweke sana samadi kwenye shamba lako hii itasaidia sana kurudisha rutuba kwenye shamba lako.

pumzisha shamba, Wakulima wengi hua hawapendi kupumzisha shamba hivo wanashauliuwa kupumzisha shamba kwa mda hii usaidia shamba kuongeza rutuba iliyo kua imepotea.

usitumie sana viuagugu,hii pia ni mbaya kutumia ke mikali za viuagugu badala yake palilia kwa jembe na badae yazike magugu ili rutuba iendelee kubaki kwenye shamba lako.

usitifue kupita kipimo, hii husababisha mmomonyoko wa udongo na pia rututba nyingi hupote kwa huo mmomonyoko

KILIMO BORA CHA MAHARAGE

       UTANGULIZI

Maharage ni moja kati ya mazao ambayo yanalimwa sana na ni moja kati ya mazao yanayo waongezea kipato wakulima wengi sana nchini Tanzania lakn kwa kufuata kanuni za kilimo bora

     MAHALI PA KUPANDA
Maharage hupandwa mahari kwenye muiniko wa mita 400-2000 kutopka usawa wa bahari kwenye udongo usio tuamisha maji 


    WAKATI WA KUPANDA
Sehem za umwagiliaji panda wakati wa kiangazi na sehem zenye mvua nyingi zinazo anza mwezi november hadi disemba april na may panda mwezi februali na machi.

    MAANDALIZI 
  1. Shamba; lima shamba vizuri na kufukia yale magugu na lima kufuatana na mwinuko wa ardhi
  2. mbegu; Andaa mbegu bora mapema kulingana na chaguo lako
  3. mbolea;andaa mbolea kilo 75 DAP au 150 mijingu kilo 50 TSP na CAN  kwa ekari 
     KUPANDA

Maharage yanatakiwa kupandwa eneo lenye unyevu wa kutosha weka ulefu wa sentimita 2.5 hadi 3 na fukia vizuri na hakikisha mbolea aigusani na mbegu kuepusha kuunguza mbegu.

na kwa maharage madogo ni kilo 25 had 30 kwa hekari na maharage makubwa ni kilo 40 48
  • kwa maharage pekee panda sm50 kati ya mstari na mstari na sm10 kati ya shina na shina 
kwa kilimo mseto panda mahindi  sm75  mstari na mstari na sm60 shina na shina weka mbegu 3 kwa maharage yanayo tambaa na  6 kwa maharage mafupi

  PALIZI
Palizi inatakiwa kufanyika siku 14 baada ya maharage kuota na rudia tena kabla ya kuchanua. unaweza kutumia madawa ya kuuwa magugu kama galex,stomp, dual gold,sateca

 WADUDU WAHARIBIFU
FUNZA WA MAHARAGE
ni wadudu wadogo wanao shambulia mimea michanga ya maharage wanaweza kusabisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100
njia nzuri ya kuwazibiti ni kuwanynyuzia dawa mfano karate 5EC au actelic50 EC ndani ya sku nne hadi 5 baada ya maharage kuota

wadudu wengine ni wanao kula maua kutoboa vitumba na mbegu pamoja na wale wanao bungua ghalani

MAGONJWA
Magonjwa makubwa ni
  • ndui ya maharage
  • madoa pembe
  • kutu
  • magonjwa yanayo sababishwa na bakteria na virusi
punguza magonjwa hayo kwa kupanda mbegu safi, aina znazo vumilia na kutunza shamba na unaweza kutumia madawa kama
kocide,fugulani,Bayleton  kwa kuzuia magonjwa yanayosababishwa na ukungu na bakteria

  UVUNAJI
Maharage yanatakiwa kuvunwa pale yanapo kauka kuepusha kuoza na kupasuka  na yanapo kauka piga vizuri mbegu zisipasuka au kuruka mbali
pepeta na chambua kuondoa uchafu anika yakauke vizuri kabla ya kuifadhi

 HIFADHI
Ghara au chombo cha kuifadhia lazima kiwe safi  na zuia wadudu kwa kutumia dawa asili na zaviwandani


NOTE; Maharage yanaweza kuzaa gunia 6 hadi 10 ukifuata kanuni bora za kilimo cha maharage



RC DKT. KEBWE STEPHEN KEBWE AMUAGIZA MKUU WA WILAYA YA KILOMBERO JAMES IHUNYO KUKAA NA VIONGOZI WA HALMASHAURI ZA KILOMBERO KUTAFUTA NJIA YA KUKITUMIA KITUO CHA UTAFITI NA MAFUNZO YA KILIMO

Image result for shamba la mpunga
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo kukaa na viongozi wa Halmashauri za Kilombero na Mji wa Ifakara ili kutafuta njia ya kukitumia vema Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Kilimo KATRIN kilichopo Wilayani humo ili kuleta mapinduzi ya Kilimo kwa Halmashauri zake.
Dkt. Kebwe ametoa agizo hilo Februari 21 mwaka huu, wakati wa ziara yake Wilayani Kilombero baada ya kutembelea Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Kilimo KATRIN na kuongea na Uongozi wa kituo hicho.
Amesema, uwepo wa Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Kilimo Wilayani humo ni fursa kubwa katika masuala ya kilimo na hivyo Halmashauri zilizopo katika Wilaya hiyo zinatakiwa kufanya kila jitihada na kutafuta njia za kufaidi matunda ya chuo hicho hasa katika kilimo na hivyo kuonesha utofauti na maeneo mengine ambayo hayana vituo vinavyojishughulisha na kilimo.
Kwa sababu hiyo, amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo kuitisha Kongamano la wadau wa kilimo ngazi ya Wilaya na kuona ni kwa namna gani kituo hicho kinaweza kuboresha kilimo katika Halmashauri zake mbili za Kilombero na Halmashauri ya Mji wa Ifakara.
 “DC mimi nakupa maagizo leo, fuatilia huyo Mkurugezi ili kuona ni kwa vipi anatumia vyuo tulivyo navyo hapa katika kuleta mapinduzi ya kilimo” Dkt. Kebwe alisema.
Aliongeza kuwa, Kongamano la wadau wa Kilimo ngazi ya Mkoa limeshafanyika  wiki moja iliyopita na kwamba katika kongamano hilo aliagiza kila Wilaya ifanye Kongamano la wadau wa Kilimo ngazi ya Wilaya, kwa lengo la kujadili namna ya kuinua uzalishaji katika Sekta ya Kilimo. Hivyo amemtaka Mkuu huyo wa Wilaya atumie fursa hiyo kujadili pia suala la chuo hicho kitakavyoleta mapinduzi ya kilimo Wilayani humo.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa alimuagiza Kaimu Mkuu wa Kituo hicho Bw. Jerome Mgase, kuwa anataka chuo hicho kujipanga katika kusaidia Halmashauri za Kilombero na Mji wa Ifakara na kujielekeza katika eneo la kuinua uzalishaji katika sekta ya Kilimo.
Ameshauri kuwa wanafunzi wa mwaka wa pili wanapokaribia kuhitimu na kufanya mazoezi yao wapangiwe Vijiji au Vitongoji mbalimbali katika Halmashauri hizo ili kulea mashamba darasa yaliyopo na kuwafundisha wananchi kilimo bora kwa Vitendo.
Dkt. Kebwe amesema, wananchi kwa sasa wanataka kufundishwa kilimo bora kwa vitendo ili kuona utofauti wa kilimo cha mazoea walichokuwa wanakitumia siku zote na kilimo bora kwa kuona uzalishaji wake unaongezeka wakilinganisha na hapo awali.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo amesema, anayapokea maagizo ya Mhe. Mkuu wa Mkoa, hata hivyo aefafanua kuwa  alishawaagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili kuangalia maeneo ambayo chuo hicho kingeweza kuwasaidia  katika kupata mbegu bora za Mpunga au  kuongeza zaidi uzalishaji wa mazao.
Pamoja na kutekeleza agizo hilo anasema pia atajikita katika kutatua mgogoro wa muda mrefu uliopo baina ya chuo hicho na Wananchi zaidi ya 200 ambao inasemekana wengine wamevamia maeneo ya chuo katika maana ya makazi na wengine  kwenye mashamba ya chuo ili kukaa katika meza moja na kupata suluhisho la kudumu.
Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Kilimo KATRIN (Kilombero Agricultural Training and Reseach Institute) ambacho kipo chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na maendeleo ya Uvuvi, kipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Wilayani Kilombero, kilianzishwa mwaka 1963 kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanganyika (kwa wakati huo) na Ujerumani.
Kituo kilikuwa na jukumu la kufanya tafiti za mazao mbalimbali yakiwemo ya mahindi, mtama, ulezi, ufuta, alizeti, minazi na pamba. Mazao mengine ni  mikunde, mazao ya mafuta, mbogamboga na matunda. Mwanzoni mwa miaka ya themanini kituo kilipewa jukumu la kuratibu utafiti wa mpunga Kitaifa.
Kwa matokeo mazuri yaliyotokana na kituo hicho, mnamo mwaka 2010, KATRIN ilichaguliwa kuwa kituo mahiri cha mpunga kwa nchi za ukanda wa Mashariki mwa Afrika (Regional Rice Centre of Excellence – RRCoE) na hadi sasa Kituo kimefanikiwa kufanya utafiti na kupitishwa kwa mbegu kumi kitaifa.

Saturday, February 25, 2017

Magonjwa hatari ya nyanya na dawa zake

Nyanya
Pamoja na umuhimu wa zao la nyanya, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Sasa ili mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato lake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili la nyanya.

Utangulizi

Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili. 

Katika makala hii tutaangalia namna ya kudhibiti baadhi ya magonjwa na wadudu muhimu wa zao la Nyanya.

1. Ugonjwa wa Ukungu

(i) Bakajani tangulia au ukungu mapema: Early blight (Alternaria solani)

Dalili

Dalili za ukungu mapema hutokea kwenye matunda, shina, na majani ya nyanya. Majani huonesha madoa ya kahawia iliyokoza na yenye mfumo wa duara zenye kati moja. Madoa kwanza hujitokeza kwenye majani yaliyokomaa na kuendelea juu ya mmea. Majani yenye madoa huweza kufa kabla ya wakati wake na kusababisha kupukutika mapema kwa majani, matunda huungua kwa jua na kuwa na rangi isiyopendeza.

Madoa ya kwenye matunda hujitokeza kwa juu kwenye ncha ya shina. Kwa kawaida madoa huwa na rangi ya kahawia iliyokoza mpaka nyeusi, yaliyozama ndani, magumu na yenye duara za kipekee zenye mfumo wa kati moja. Kuoza kwa chini ya shina huweza kutokea kwenye miche michanga. Hali hii hujionyesha kwa kuzunguka shina sehemu ya chini. Miche iliyoathirika hudumaa na huweza kunyauka na kufa. Miche mikubwa iliyoathirika huwa na makovu ambayo kawaida huwa upande mmoja tu wa shina na hurefuka na kudidimia kwenye mashina na vikonyo.
 
Jani-la-nyanya-lenye-dalili-za-ukungu-tangulia
Dalili za ugonjwa wa ukungu tangulia

Dalili za ugonjwa wa ukungu mapema mara nyingi hudhaniwa kuwa ni ukungu chelewa, lakini kwenye ukungu chelewa makovu yamefifia, madogo na hayana alama za duara zilizonyanyuka.

Njia za kudhibiti

Ukungu mapema unaweza kubainika shambani kwa kutafuta madoa ya kahawia iliyokoza ya kiasi cha 1.2 sm kwa upana. Ni vigumu sana kuzuia ukungu mapema ukishaanza shambani. Njia muhimu ya kudhibiti ukungu mapema ni kuzuia kuingia kwake na kusambaa.

Mbinu bora za kilimo

•Zungusha mazao ya nyanya na nafaka ndogo ndogo, mahindi au jamii za kunde
•Panda aina zenye kustahimili ‘early blight’. (Km. Floradade, Hytec 36, Julius F1 na Zest F1)
•Tumia mbegu safi
•Limia na kufukia mabaki ya mazao baada ya mavuno na choma moto mazao yaliyoathirika na takataka zote za mazao
•Epuka kumwagilia kwa juu
•Ongezea mbolea ya samadi
•Tumia matandazo kuzuia kurukia kwa maji
•Hakikisha kupanda kwa nafasi sahihi na kufunga vijiti
•Toa majani ya chini yaliyoathirika ili kuboresha mzunguko wa hewa
•Epuka kutumia ardhi kwa angalau miaka 2 baada ya uzalishaji wa nyanya


Dawa (chemical control)

‘Early blight’ inaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa za ukungu Boscalid ( Endura Captan, Captan 4F, Captan 50), dawa za ukungu zenye shaba (Champ Dry Prill, Champ Formula 2, Copper-Count-N, Kocide 101, Kocide DF, Kocide 4.5LF, Kocide 3000, Nordox Tri Basic), Chlorothalonil na Chlorothalonil Mixtures (Bravo 720/Echo, Bravo Ultrex/Echo 90DF, Bravo Weather Stik, Echo Zn, Ridomil Gold/Bravo), EBDC, Copper FBDC na EBDC/Zaxamide (Cuaprofix Disperss M2, Dithane/Gavel, Maneb 75, Manex, Mankocide, Manzate F1, Penncozeb 80W, Penncozeb 75DF), Famoxadone+Cymoxanil (Tanos, Fenamidone, Reason 500SC, Penthiopyrad, Fontelis, Pyrimethanil, Scala), Strobilurin na Strobilurin Mixtures (Cabrio, Flint, Quadris)

Kibaiolojia (Biological control)

Kuna mazao mengi yatokanayo na mimea ambayo husemekana kuwa na sifa za sumu kwa aina nyingi za ukungu. Haya ni mazao asilia ambayo hupoteza nguvu zake haraka juu ya majani na kwenye udongo. Juu ya hivyo, taarifa kidogo sana zinajulikana kuhusu viwango vyao vya matumizi, athari zao juu ya viumbe marafiki, na binadamu.


(ii) Bakajani Chelewa au Ukungu chelewa: Late blight (Phytophthora infestans)

Dalili

Dalili za ukungu chelewa hujitokeza kwenye matunda, majani, shina na matawi. Kwenye majani madoa ya kijani kibichi/kahawia hujitokeza upande wa juu wa majani, na pembezoni mwa majani huwa kijani kibichi na huwa kama iliyotota, kwa kawaida madoa hutanuka ghafla hadi majani yote yanapokufa. Nyakati za hewa ya unyevu, ukungu mweupe/kijivujivu hujitokeza kwenye kingo za madoa katika sehemu za chini za majani. Wakati wa joto, sehemu zilizoathirika huonesha kukauka. Madoa ya kahawia na yaliyorefuka hujitokeza kwenye mashina.

Kwenye matunda, madoa ya kijivujivu/kijani yaliyotota hujitokeza kwenye nusu ya tunda upande wa juu. Madoa haya baadae husambaa na kugeuka kahawia, yaliyokunjamana na magumu. Wakati wa hali ya unyevu ukungu mweupe hujitokeza kwenye sehemu za matunda yaliyoathirika. Dalili za ukungu chelewa mara nyingi hudhaniwa ni ukungu mapema (Alternaria solani), lakini dalili za ukungu mapema mara nyingi huwa za duara zaidi, kubwa, na zilizokoza na za duara zenye kati moja. Ukungu chelewa hauna duara hizi.

Matunda-ya-nyanya-yaliyoathiriwa-na-ukungu-chelewa
Ukungu chelewa kwenye nyanya

Njia za kudhibiti

Nyanya zilizoambukizwa huweza kushambuliwa kwa haraka na kuteketezwa na ukungu chelewa. Kuzuia ugonjwa huu ni shida sana ukishajiimarisha shambani. Njia muhimu sana ya kuzuia ukungu chelewa ni kuhakikisha haijajiimarisha na kusambaa. Hii inaweza kufanyika kwa kutumia mbinu zifuatazo:

Mbinu bora za kilimo

•Crop rotation: Zungusha mazao mengine kwa miaka 3 hadi 4
•Tumia aina zenye kustahamili ugonjwa huu (km. Meru, Tengeru 97 na Shengena)
•Tumia mbegu safi
•Ondoa mabaki ya mazao na choma moto mimea iliyoathirika na mabaki ya mimea
•Tumia moto au mvuke kuua vimelea katika maeneo yaliyoathirika
•Weka matandazo ya nyasi kuzuia kurukia kwa maji
•Tumia zana safi baina ya mashamba
•Hakikisha maji hayatuami na kuwe na mzunguko mzuri wa hewa
•Toa majani ya chini yaliyoathirika kusaidia mzunguko mzuri wa hewa
•Hakikisha kupanda kwa nafasi inayotakiwa


Dawa (Chemical control)

Ukungu chelewa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa za ukungu za aina ya mrututu (Champ Dry Prill, Champ Formula 2, Copper-Count-N, Kocide 101, kocide DF, Kocide 4.5LF, Kocide 3000, Kocide 6000), Cholorothalolin na Cholorothalonil Mixtures (Bravo 720/Echo 720, Bravo Ultrex/Echo 90DF, Bravo Weather Stik, Echo Zn, Ridomil gold/Bravo), EBDC, Copper EBDC/ Zoxamide (Cuprofix MZ Disperss, Dithane, Gavel, Maneb 75 DF, Manex, Mankocide, Manzate F1, Penncozeb 80W, Penncozeb 75DF), Famoxadone + Cymoxanil (Tanos, Fenamidone, eason 500SC) Strobilurin na Strobilurin Mixtures ( Cabrio Flint Quadris).

Kibaiolojia (Biological control)

Mpaka hivi sasa hakuna dawa ya kibaiolojia inayo weza kudhibiti/kuzuia ukungu chelewa.


2. Bakadoa: Bacterial spot >Madoa ya majani kutokana na bakteria< (Xanthomonas spp.)

Dalili

Dalili bayana zaidi huonekana kwenye majani, ndio maana ya hilo jina ‘Madoa ya majani kutokana na bakteria’. Makovu madogo ya rangi ya manjano-kijani hujitokeza kwenye majani machanga na matokeo yake ni majani yaliyopindapinda, yaliyokoza, yaliyotota na yenye kuonesha ishara kama yenye mafuta kwenye majani yaliyokomaa.

Makovu hukua haraka na yanaweza kufikia ukubwa wa 0.25-0.5 sm, huwa na rangi ya kahawia/nyekundu. Umbo la makovu kwa kawaida huwa na pembe kwa vile hufuata umbile la mishipa midogo ya majani. Makovu mara nyingi hutokea kwenye ncha na pembezoni mwa jani ambamo unyevu huhifadhiwa. Katika hali ya ujoto/ukavu, majani huonekana yamechanika chanika kutokana na maeneo ya pembezoni mwa majani na kati ya makovu hukauka na kukatika. Ukubwa wa makovu huongezeka kutokana na muda ambao majani yanakuwa na maji. 

nyanya-iliyoathiriwa-na-ugonjwa-wa-bakadoa
Athari za ugonjwa wa bakadoa

Kwenye matunda, madoa huanza kwa kuwa na rangi ya kijani kibichi na kuonyesha sehemu kama zilizotota maji. Kwa kawaida hufikia ukubwa wa 0.5 sm. Madoa haya hatimaye huwa yenye mnyanyuko, rangi ya kahawia na yenye kukwaruza kwenye tunda la nyanya. Madoa haya kawaida hufanya njia za kupenya aina nyengine za ukungu na bakteria wavamizi na kusababisha kuoza kwa matunda.

Njia za kudhibiti

Madoa ya majani yanayosababishwa na bakteria yakishaingia tu shambani au kwenye jengo la kuoteshea mimea ni vigumu kuyadhibiti. Mbinu zifuatazo zinaweza kuchukuliwa kudhibiti ugonjwa huu:

Mbinu bora za kilimo

•Mbegu zisizo na vimelea vya magonjwa
•Miche isiyo na magonjwa
•Mzunguko wa mazao
•Epuka maeneo yaliyopandwa nyanya kwa muda wa mwaka mmoja
•Tumia miche iliyopasishwa
•Ondosha shambani na choma moto mabaki ya mimea iliyoathirika na masalio
•Safisha na kuua vimelea vya magonjwa katika vitalu kabla ya kusia mbegu

Matumizi ya kemikali

Madoa yanayosababishwa na bakteria yanaweza kudhibitiwa kwa kutumia kemikali zifuatazo; Acibenzolar (Actigard 50WG) Copper fungicides (Champ Dry prill, Champ Formula 2, Copper-Count-N, Cuprofix MZ Disperss, Kocide, Kocide DF, Nordox, Tofix Dispress Basic Copper) Copper/ EBDC/Zoxamide Mixtures, Cuprof ix Dispress MZ, Gavel, Mankocide) Famoxadone/Cymoxanil (Tanos) na Streptomycin (Agri-strep).

Kibaiolojia (Biological control)

Virusi vinavyoshambulia bakteria hudhibiti magonjwa haya, lakini ni lazima viwekwe shambani wakati wa jioni angalau mara mbili kwa wiki. Bakteria wa jamii ya Xanthomonas ambao hawasababishi magonjwa hutoa udhibiti wa kiasi wa madoa yanayosababishwa na bakteria.


3. Mnyauko bakteria: Bacterial wilt 

(Ralstonia solanacearum, Pseudomonas solanacearum)

Dalili

Dalili za awali ni kunyauka kwa majani ya kwenye ncha. Baada ya siku mbili dalili hii huwa ni ya kudumu, na mti wote hunyauka na kufa kutokana na kuendelea kwa ugonjwa. Matawi yote hunyauka kwa wakati mmoja. Shina la mti ulionyauka likikatwa shehemu ya kati huwa na rangi nyeusi na huonekana kama iliyotota maji. Shina linapokamuliwa, hutoa maji ya utelezi kijivujivu unaotiririka. 

Hatua zinazofuata za ugonjwa huu ni kuoza kwa sehemu ya kati ya shina na hii husababisha uwazi katika sehemu hiyo. Mzizi ulioathirika huoza na kuwa na rangi ya kahawia mpaka nyeusi. 

Mmea-umenyauka-kwa-sababu-ya-ugonjwa-wa-mnyauko-bakteria

Mnyauko wa bakteria hausasababishi madoa kwenye matunda. Mmea hunyauka ukiwa na rangi ya kijani, (majani hayawi ya njano au kuwa na madoa) na inaweza kutokea ghafla. Katika hali ya ugonjwa kusambaa taratibu, mti hutoa mizizi mingi juu ya shina na mmea hudumaa. Kuanguka kabisa kwa mmea hutokea wakati nyuzi joto zinapofikia 320C au juu ya hapo.

Njia za kudhibiti

Mnyauko unaosababishwa na bakteria unaweza kutambuliwa shambani kwa kukata sehemu ya chini ya shina urefu wa 2-3 sm na kuisimamisha kwenye glasi ya maji. Ikiwa ugonjwa upo, basi michirizi ya bakteria kama nyuzi hutoka kwenye kipande hicho cha shina sekunde chache tu baada ya kukisimamisha kwenye maji.

Mbinu bora za kilimo

•Mzunguko wa mazao na yale ambayo hayaathiriki
•Usipande nyanya katika udongo ambao ugonjwa huu uliwahi kuwemo
•Tumia aina za mbegu zenye kustahimili/zisizopata ugonjwa wa mnyauko bakteria. (Kama vile Fortune Maker, Kenton na Taiwan F1)
•Toa na angamiza mimea iliyonyauka kutoka shambani kupunguza usambaaji wa maradhi
•Ruhusu mafuriko yenye kuenea
•Ongezea mbolea ya samadi
•Panda katika msimu ambao si rafiki kwa ugonjwa huu
•Zuia minyoo fundo (root-knot nematodes) kwani husaidia uingiaji wa ugonjwa
•Changanya na mazao jamii ya kunde
•Epuka kutumia ardhi kwa miaka 3-4 baada ya uzalishaji wa nyanya

Dawa (Chemical control)

Mnyauko wa Bacteria unaweza kudhibitiwa kwa kutumia Chlorothalonil (Bravo 720/Ensign, Bravo Ultrex, Bravo Weather Stik, Echo 720, Echo 90DF, Echo Zn, Ridomil/Bravo). Juu ya hivyo, tahadhari inapaswa ichukuliwe kuepuka usugu wa vimelea vya ugonjwa, hivyo mbinu ya matumizi ya kemikali katika kuzuia ugonjwa inabidi ichanganye na mbinu nyinginezo.

Kibaiolojia (Biological control)

Kuzuia kunyauka kunakosababishwa na bakteria kunajumuisha matumizi ya ardhi zenye kuzuia ugonjwa na ardhi zenye vimelea wapinzani (km. Candida ethanolica, Pythium oligandrum).


4. Makovu bakteria (Bacterial canker)

Ugonjwa huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu na hewani. Hutokea zaidi wakati wa masika. Majani hukauka nchani na makovu yaliyodidimia hutokea kwenye shina. Matunda huwa na makovu yenye rangi ya kahawia sehemu ya katikati.


Njia za kudhibiti

· Tumia mbegu bora na safi
· Teketeza masalia ya mazao
· Tumia mzunguko wa mazao


5. Mnyauko Fusari: Fusium wilt

(Fusarium oxysporum)

Dalili

Dalili zinajumuisha majani ya chini kuwa na rangi ya njano. Majani yaliyoathirika hukatika kwa urahisi kutoka kwenye shina na wakati mwingine hukauka kabla ya kubainika mnyauko. Tawi moja au mawili huonesha ishara. Majani machanga ya upande mmoja wa tawi huonesha dalili za kuathirika wakati upande wa pili hauneshi dalili zozote. Matawi na vipande vya matawi vikikatwa katikati huonesha rangi ya kahawia katika sehemu za kusafirishia maji.

Majani-ya-nyanya-yaliyogeuka-rangi-kutokana-na-mnyauko-fusari


6. Mnyauko Vetisili: Verticillium wilt 

(Verticillium spp.)

Dalili

Dalili hujitokeza kwenye majani yaliyokomaa na baadaye kwenye majani machanga. Majani yaliyoathirika hugeuka manjano, hukatika kwa urahisi kutoka kwenye tawi na wakati mwingine hukauka kabla kunyauka hakujajionesha. Ncha za matawi hunyauka wakati wa mchana. Wakati kupukutika kwa majani kukiendelea, majani ya juu hujikunja kwa kuelekea juu lakini hubaki hai.

Nyanya-zilivyokauka-kutokana-na-mnyauko-vetisili
Mnyauko vetisili kwenye nyanya

Njia za kudhibiti

Vyote, mnyauko ‘Fusari’ na ‘Vetisili’ hubaki kwenye udongo kwa miaka mingi. Njia za kudhibiti magonjwa haya hujumuisha yafuatayo:


Mbinu bora za kilimo

•Crop rotation: Mzunguko mrefu wa mazao (miaka 4-5) na mazao yanayostahimili magonjwa haya
•Tumia mbegu safi na zenye afya
•Lima kwa kuchimba zaidi
•Pandisha PH kwa kutumia chokaa au samadi katika ardhi zenye kiwango kikubwa cha tindikali
•Usipande nyanya katika ardhi ambayo mnyauko kutokana na Ukungu ulikuwepo
•Tumia mbegu zinazostahimili mnyauko unaotokana na Ukungu (km. Diego, Duke, Floridade, Fanny, Fortune Maker, Napoli, Radja, Roma VF, Roma VFN na Tengeru 97)
•Ondoa na teketeza mimea iliyoathirika, kuzuia usambaaji wa maradhi
•Mwagilia
•Dhibiti minyoo fundo, kwani hawa wanarahisisha na kuruhusu uingiaji wa maradhi haya ya kunyauka

Dawa (chemical control)

Mnyauko Fusari unaweza kudhibitiwa kwa kutumia Methyl bromide, Methyl bromide/Chloropicrin. Thiophanate-methyl, Streptomyces griseoviridis and Iprodione. Mnyauko Vetisili unaweza kudhibitiwa kwa kutumia Methyl bromide/Chrolopicrin.

Kibaiolojia (Biological control)

Dawa itokanayo na ukungu Mycostop husaidia kudhibiti mnyauko unaosababishwa ‘Fusarium’.


7. Rasta: Yellow leaf curl

Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Hutokea zaidi wakati wa kiangazi. Mimea hudumaa na majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya manjano na pengine rangi ya zambarau. Nyanya hupasuka.

Jinsi ya kudhibiti

· Nyunyiza dawa za sumu za kuua wadudu (Selecron, Dursburn, Actelic)
· Ng’oa mimea yenye ugonjwa
· Tumia mzunguko wa mazao
· Weka shamba katika hali ya usafi


8. Batobato: Tomato mosaic virus (ToMV)

Ugonjwa husababishwa na virusi na hueezwa na mbegu na kugusana. Majani huwa na mchanganyiko wa rangi hasa kijani kibichi na kijani kilichofifia (majano). Majani hujikunja na manjani machanga huwa na maumbile yasiyo kawaida. Ukifikisha jani huwa linavinjikavunjika.

Majani-ya-nyanya-yalivyojikunja-kutokana-na-ugonjwa-wa-batobato
Ugonjwa wa batobato 


Jinsi ya kudhibiti

· Tumia mbegu bora na safi
· Ng’oa mimea iliyoshambuliwa
· Teketeza masalia ya mazao
· Weka shamba katika hali ya usafi


9. Virusi mosaic vya tumbaku, matango na Virus jani vya nyanya

Dalili

Dalili zinajumuisha rangi rangi, kuwa manjano, vichungu, mabaka, rangi za kahawia, kudumaa, kukunjika kwa majani, nafasi fupi baina ya vifundo, majani membamba. Mazao duni, kuchelewa kuiva kwa matunda, rangi isiyo sawasawa ya matunda ni matokeo ya mashambulizi. Dalili zinategemea sana umri wa mmea ulioshambuliwa, hali ya mazingira, aina au jamii ya virusi na jamii ya virusi vyote vilivyopo. Aina ya nyanya pia inachangia aina za dalili zinazojitokeza.

Njia za kudhibiti

‘Tobacco mosaic virus’ na ‘tomato leaf curl virus’ huendelea kuwepo sana na husambaa kirahisi na kwa haraka, wakati ‘cucumber mosaic virus’ haiendelei kuwepo sana na usambaaji wake ni mdogo kuliko ‘tobacco mosaic virus’. Virusi husambazwa kutoka mimea iliyoathirika na kwenda kwenye mimea yenye afya kupitia kufyonza kwa nzi weupe na ‘thrips’.

Mbinu bora za kilimo

•Panda aina asilia zenye kuzuia.
•Hifadhi miche isigusane na wadudu kwa kutumia chandarua.
•Epuka kupandikiza kwenye ardhi zenye mimea iliyoathirika.
•Ng’oa mimea iliyoathirika na choma moto mabaki ya mazao.
•Fanya mzunguko wa mazao na mimea yenye kustahimili.
•Epuka kuvuta sigara wakati wa kuhudumia nyanya.
•Safisha mikono na zana kwa kutumia dawa za kuua vimelea vya magonjwa.
•Epuka kwenda kwenye mashamba safi baada ya kutoka kwenye mashamba yaliyoathirika.
•Virusi husitishwa kasi ya mashambulizi yake kwa wafanyakazi shambani kutia mikono yao ndani ya maziwa kabla ya kupanda.

Dawa (Chemical control)

Mpaka hivi sasa hakuna kemikali inayozuia mimea isipate mashambulizi ya virusi. Dawa za kuulia wadudu zinadhibiti wadudu lakini thrips ni taabu kuwadhibiti.

Kibaiolojia (Biological control)

Mpaka hivi sasa hakuna viumbe vinavyoweza kudhibiti virusi kwenye sehemu za mimea. Viumbe vya kudhibiti nzi weupe na vidukari kanda mbili vinafanyiwa uchunguzi.


10. Ugonjwa wa ukoma wa nyanya

Huu ni ugonjwa wa virus unao enezwa na nzi mweupe. Inzi hawa hushambulia zaidi nyanya wakati wa kiangazi, hasa kipindi cha joto kali.


Dalili

• Majani machanga hujikunja na baadaye majani yote.
• Kupungua kwa utoaji maua na matunda na hata yakitokea matunda huwa ni madogo.
• Mmea kudumaa na kutozaa kabisa.


Njia za kudhibiti

Mbinu madhubuti ni kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu kwenye shamba kwa kudhibiti kuzaana na kuenea kwa mdudu (inzi mweupe) kama tulivyo ona katika kupambana na mdudu huyo, yaani:
• Kuondoa mimea michache iliyo shikwa na ugonjwa maana wadudu hawa wanachukua ugonjwa huu kutoka mimea hii.
• Kutumia mbegu zilizo hakikishwa kuwa zinaweza kuvumilia ugonjwa huu na kutoa mavuno mazuri.
• Usilime nyanya karibu na eneo lililo na mazao kama bamia, mipapai maana mimea hii huhifadhi inzi mweupe
• Kuua inzi weupe wanaofyonza nyanya na kusambaza virusi kwa kutumia madawa. Tumia madawa kama vile Selecron, Decis, Karate n.k.
• Epuka kuchanganya zao la nyanya na mazao mengine yanayohifadhi hawa nzi kama vile mipapai na bamia.
• Ng'oa na kuchoma moto mimea yote iliyougua ugonjwa huu.


11. Ugonjwa wa mmea wa nyanya kuoza sehemu ya shina inayogusa udongo na mmea kunyauka kama vile umekosa maji

• Wadudu wanaosabisha ugonjwa huu hupatikana ardhini.
• Hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huu baada ya dalili kujitokeza.
• Kupiga madawa za viwandani ardhini kabla ya kupanda nyanya husaidia kupungu wadudu wa ugonjwa.
• Epuka kupanda nyanya au mazao jamii ya nyanya katika eneo moja kwa muda mrefu mfulilizo. Baadhi ya mazao yanayohusiana na nyanya ni bilinganya, pilipili, ngogwe, mnavu, n.k.


12. Ugonjwa wa miche michanga ya nyanya kuoza sehemu ya shina inayogusa udongo na kufa ghafla

Ugonjwa huu hushambulia miche kitaluni na husabishwa na wadudu waishio ardhini. Mara baada ya dalili, ugonjwa huu hauna dawa ila unaweza kukingwa kwa kutumia njia zifuatazo:
• Choma moto udongo wa kutengezea kitalu kabla ya kupanda mbegu zako. Kutumia mboji husaidia kukinga miche dhidi ya ugonjwa huu.
• Epuka kumwagilia maji kupita kiasi na kutumia kuvuli kizito.


13. Matunda ya nyanya kuoza kitako

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na:
• Umwagiliaji wa nyanya bustanini usio na mpangilio maalumu. Mfano, kumwagilia mimea maji mengi kasha kuiacha bila maji kwa siku kadhaa.
• Upungufu wa virutubisho aina ya chokaa. Dalili zake ni matunda ya nyanya kuoza sehemu ya kitako na kuonyesha rangi nyeusi.

Njia za kudhibiti

Kuzuia ugonjwa huu, zingatia kuwa na utaratibu mzuri wa kumwagilia maji ambao haubadiliki ovyo kiratiba na kiasi cha maji yanayowekwa. Rutubisha mimea kwa madini ya chokaa kwa kutumia mbolea aina ya CAN zenye madini haya.

Haya ni baadhi tu magonjwa ambayo kwa kiasi kikubwa yanahatarisha mavuno ya nyanya, je kuna ugonjwa mwingine umekutana nao shambani kwako na hatuja ueleza hapa? je unafahamu njia nyingine ya kudhibiti ugonjwa wowote uliotajwa hapa? Tafadhali tufahamishe kwa kuweka comment yako hapa chini.

Fahamu mbinu za kuongeza thamani nyama

  Safari ya kuongeza thamani nyama ya mifugo huanzia shambani kwa usimamizi wa ufugaji na uzalishaji. Lishe bora ni muhimu kwa wa ufugaji ...