Zao la vitunguu hulimwa duniani kote kwa ajili ya kutumika kama
kiungo cha chakula. Kila familia angalau hutumia kitunguu mara moja klia siku
katika chakula chao. Vitunguu hutumika kama dawa katika baadhi ya jamii na
wataalamu wanasema hupunguza shinikizo la juu la damu na kupunguza matatizo
mengine ya moyo.
Ili uweze kuzalisha
mazao ya jamii ya kabichi unahitaji vitu vifuatavyo:
i) Ardhi yenye rutuba.
ii) Mbegu bora ya vitunguu; k.m Red Creole kutoka ktk chanzo cha
kuaminika
iii) Uwezekano wa kupata maji.
iv) Dawa za kudhibiti magugu, wadudu na magonjwa.
Uchaguzi wa mbegu bora
Mbegu bora ichaguliwe kwa kuzingatia sifa zifuatazo:
1) Iwe na ustahimilivu
dhidi ya magonjwa na wadudu.
2) Yenye kutoa mavuno mengi.
3) Inayokomaa mapema ilu kuwahi soko.
4) Inayoendana na hali ya
hewa ya eneo shamba lilipo.
Udongo – vitunguu ni zao la
kina kifupi, udongo uwe laini na usio na mawe wala mabonge ili kuruhusu ukuaji
wa kitunguu. pH ya 6-7 na usiotuamisha maji.
Kupanda moja kwa moja shambani
Ingawa zipo baadhi ya faida za kupanda mbegu za vitunguu moja moja
kwa moja shambani (direct seeding) kama kuepuka usumbufu wa kutunza kitalu,
njia hii sio maarufu sana miongoni mwa wakulima ukilinganisha na ile ya kutumia
kitalu.
Miche ya vitunguu itakua tayari kwa
kupandikizwa kati ya wiki 6 hadi 8 baada ya kupanda kitalu. Wakati wa
kupandikiza, itawanye mizizi sawasawa kadri ilivyojipanga katika shina kabla ya
kufukia na kushindilia kiasi.
Muhimu; wiki mbili kabla ya kuhamisha miche
kutoka kwenye kitalu kwenda kuipandikiza shambani, unatakiwa kuipa miche
mazingira halisi ya shambani kwamfano kupunguza kiwango cha maji na kuiondolea
kivuli. Hii husaidia kupunguza uwezekano wa miche kufa pindi inapo amishiwa
kwenye mazingira mapya ya shamba.
Wadudu waharibifu wa vitunguu
Jina la mdudu
|
|
Thiripi (Thrips): Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na
shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha
majani kuwa na doti nyeupe. Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake
jambo ambalo huathiri mavuno pia.
Thrips huudhibitiwa kwa kunyunyuzia
dawa iitwayo Protrin 60 EC.
|
|
Kimamba:
Wadudu hawa hufyonza maji kwenye
vitunguu, na kusambaza ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu.
Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi
kwenye mbegu.
Wadudu hawa huthibitiwa kwa
kunynyuzia dawa Metakan super 350 SE
|
|
Sota (Cutworms): Sota au viwavi wa nondo wanasababisha uharibifu mkubwa. Viwavi
wanakata mashina ya miche michanga sehemu ya chini ya shina juu ya ardhi.
Sota wanapendelea kula wakati wa usiku na mchana kujificha kwenye ardhi
karibu sana na sehemu waliokata shina. Uharibifu huu unapunguza sana idadi ya
mimea shambani na kuleta upungufu wa mazao.
Wadudu hawa wanadhibitiwa kwa kupulizia dawa kama;
PROTRIN 60 EC, Agromectin 1.8 EC ambayo hutumika ndani ya wiki 0-7 na Metakan super 350 EC nayo hutumika
ndani ya wiki 8-20.
|
|
Utitiri wekundu (Red spider mites)
Hawa ni wadudu wadogo sana, ambao wanajificha upande
wa chini wa majani. Wanafyonza maji maji kwenye majani na kusababisha majani
kuwa na rangi nyeupe. Wadudu hawa wanatengeneza utando mweupe kuzunguka
majani na mashina. Mmea unashindwa kutengeneza chakula na baadaye inakufa.
Njia ya kudhibiti:
kupulizia dawa za wadudu
AGROMECTINE 1.8 EC.
|
|
Vipekecha majani (leaf miner)
Hawa ni aina ya inzi wadogo, ambao viwavi wake
wanashambulia majani, kwa kupekecha na kutengeneza mitandao wa mitaro kwenye
majani. Viwavi wanashambulia majani na kusababisha majani kukauka. Upungufu
mkubwa wa mazao hutokea.
Njia ya dhibiti:
kupulizia dawa ya wadudu kama AGROMETHRIN 10 EC
kuteketeza masalia ya mazao
kutumia mzunguko wa mazao
|
|
Magonjwa ya vitunguu
Ugonjwa
|
Dalili za
ugonjwa ni:-
|
Picha
|
Baka zambarau
(Puple Blotch)
Ungonjwa huu
unasababishwa na kuvu (fangasi). Chanzo kikubwa cha ugonjwa ni mbegu zenye
ugonjwa. Pia ugonjwa unajitokeza wakati kuna ukungu na unyevunyevu mwingi
hewani hasa wakati wa masika.
Kiasi cha
60-80 % ya mazao yanaweza kupotea kama ugonjwa hautadhibitiwa.
|
ü madoa meupe yaliyodidimia kwenye majani na mashina
ü rangi ya zambarau kuwepo katikati ya doa jeupe.
ü majani kuanguka
|
|
Kinyausi (Damping – off)
Ugonjwa huu unasababishwa na fangasi na kuenezwa na
udongo, mbegu na masalia ya mazao. Ugonjwa unajitokeza hasa kitaluni ikiwa
hali ya hewa ina unyevunyevu na udongo una maji maji.
Kudhibiti: mbegu ziwe safi na ziwekwe dawa ya AGROZEB
80WP
|
ü mbegu kuoza
kabla ya kuota na kunyauka kwa miche baada ya kuota
|
|
Virusi njano
vya vitunguu (Onion yellow Dwarf virus)
Ugonjwa huu
unasababishwa na virusi na kuenezwa na wadudu aina ya vidukari (wadudu
-mafuta).
Kudhibiti
ugonjwa huu ni:-
Kutumia mbegu
safi
Kuweka shamba
katika hali ya usafi
Tumia PROTRIN kuua Wadudu wanaosambaza
ugonjwa
|
Mistari ya
rangi ya manjano kwenye majani.
Kujikunja kwa
majani
Majani
kugeuka rangi ya manjano na kuanguka
Mimea mzima
kudumaa, kujikunja na kufa.
|
|
Ukungu mweusi
Onion
Black Mold
Kisababishi:
Aspergillus niger
Maranyingi
hutokea endapo joto litakua kali.
Kudhibiti:
mbegu ziwe safi na ziwekwe dawa ya AGROZEB 80WP
Agromenol
250EC
|
Utando mweusi
katika gamba la kitunguu.
|
|
Kuoza shingo na kirungu
Onion
Botrytis Neck and Bulb Rot
Kisababishi
: Botrytis allii
Japo
Ugonjwa huu huonekana wakati vitunguu vimehifadhiwa, maambukizi huanzia
shambani.
Tumia
Agromenol 250EC
|
Kudumaa
Sehemu
zilizoathirika hukauka na kufa.
Gamba gumu
katika shingo ya kitunguu.
|
|
Ubwiri unyoya
Onion Downy Mildew
Kisababishi: Peronospora destructor
Kudhibiti: Meronil 720 EC,
rudia kila baada ya siku 7
|
Manyoya ya
kijivu-meupe katika majani ya umri mkubwa.
|
|
Kutu
Kisababishi:
Puccinia
porri
Tumia Agromenol 250EC, Meronil 720 EC,
Sipron Star 330 EC
|
Majani yalioathirika huwa na madoa ya rangi ya
machungwa
Baadaye hugeuka na kuwa meusi
Majani yaliyoathirika sana huwa ya njano na
hatimaye hufa.
|
|
ü kutumia
mzunguko wa mazao
ü kusia mbegu kwa
nafasi za kutosha
ü kuepukana na
kubananisha miche kitaluni
ü Kuepukanana na
kumwagilia maji wakati wa jua kali au wakati kuna ukungu.
ü kupanda mbegu safi
ü kupanda vitunguu kwa kutumia mzunguko wa mazao
ü kuteketeza msalii ya vitunguu baada ya kuvuna
Wasiliana nasi kwa ajili ya ushauri na madawa.
0756483174
No comments:
Post a Comment