Wednesday, December 20, 2017

NJIA BORA ZA UTUNZAJI WA MAYAI YA KUKU

 
Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.

Hakikisha ya fuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.

UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili

KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo
Yasiwe na uchafu yawe masafi
Yasiwe na nyufa
Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.

KUMTAYARISHA KUKU WA KUATAMIA
Pamoja na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao. Hali hii husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.
Sasa unatakiwa kufanya yafuatayo:-
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu ndani ya kiota
Pia mnyunyuzie dawa kuku anayetarajia kuatamia
Weka mayai kwenye kiota huku mikono yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na harufu kwani kuku anaweza kuyasusa.

Ni vizuri kuifanya kazi hii ya kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku. Pia ifahamike kuwa kwa kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.

PIA JIFUNZE MBINU ZA KUATAMIA MAYAI MENGI KWA NJIA ZA ASILI.
Iwapo una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia na kutotoa pamoja.
Unachotakiwa kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho kutaga.
Unaweza kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na kupata vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia. Mwekee mayai viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa hivyo ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga watoke.

UTEKELEZAJI WAKE.
Kuku anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku anayotaga
Yanapofika mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku ukiendelea kuweka alama mayai yanayotagwa kila siku.
Mara kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10
Fanya hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
Wawekee kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai ya ukweli wakati wa usiku.

MUHIMU.
Mayai ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za mafuta ya taa, manukato n.k.

JIFUNZE PIA KUTAMBUA MAYAI YALIYO NA MBEGU NA YALE YASUYO NA MBEGU.
Mfugaji anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku ya saba baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box lililotengenezwa maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba chenye kiza. Hii itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa chakula cha familia au kuyauza.

MIFUMO MBALIMBALI YA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.

 
Kama nilivoeleza kwenye makalaa iliyopita ya http://mkulimajembemfugaji.blogspot.com/2016/07/njia-tofauti-za-kufuga-kuku-faida-zake_5.html zipo njia(mifumo) tofauti za ufugaji wa kuku hawa
A. MFUMO HURIA
Katika mfumo huu kuku huachiwa wakitembea toka asubuhi wakijitafutia chakula na maji na kufungiwa kwenye vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku. Huu ni mfumo rahisi lakini si nzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi.

FAIDA. 
Mfumo huu una faida za gharama ndogo za uendeshaji kiujumla.

HASARA
Uwezekano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche, kuibiwa mitaani n.k
Kuku huweza kutaga popote na kusababisha upotevu mkubwa wa mayai.
Ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa
Utagaji unakuwa si nzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Uwekaji kumbukumbu si nzuri.
Ni vigumu kugundua kuku wagonjwa hivyo kusababisha ugumu katika utoaji wa tiba.

UTUMIAJI NZURI WA MFUMO HUU
Kuku wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati mwingine wowote hali ya hewa inapokuwa si nzuri.
Kuku wapatiwe chakula cha ziada na maji.
Kuku waandaliwe kwa viota vya kutagia.
Kuku 100 ni vizuri wakitumia eneo la ardhi la ekari 1.
B.MFUMO NUSU HURIA
Huu ni mfumo ambao kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa uzio/ wigo. Mfumo huu ni ghari kiasi ukilinganisha na mfumo huria lakini huweza kumpatia mfugaji faida haraka sana.

FAIDA
Sehemu ndogo ya kufugia hutumika kuliko ufugaji huria, utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na mfumo huria, Ni rahisi kutibu magonjwa ya mlipuka kama mdondo (Newcastle desease), Upotevu wa kuku na mayai ni mdogo sana ukilinganisha na mfumo huria.
C. MFUMO WA NDANI
Kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani. Mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za mbao(randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwa katwa.

FAIDA
Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia, uangalizi mzuri na rahisi wa kuku, Joto litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuua vimelea vya maradhi, kuku wanakingwa na hali ya hewa mbaya na maadui wengine.

HASARA
Uwezekano wa kuku kudonoana ni mkubw na pia Gharama za ujenzi wa mabanda

UTUMIAJI MZURI WA MFUMO HUU.
1. Matandiko yageuzwe kila siku
2. Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha, ambayo yatatoa unyevunyevu hewa chafu ikiwemo ammonia.
4. Mita mraba moja hutosha kuku 5 hadi 8.

BANDA LA KULELEA VIFARANGA

Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufi kirie yafuatayo:-
a)    Nyumba ya vifaranga iwe karibu na nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua vifaranga wako mara kwa mara.
b)   Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga mojawapo ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.
c)     Nyumba ya vifaranga isiruhusu ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu kuingia. Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.
d)    Nyumba iwe na eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.
e)     Ijengwe kwenye sehemu isiyoelekea upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa. Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa na upepo.


Eneo: Vifaranga hawahitaji eneo kubwa katika muda wa majuma 4 ya kwanza. Nafasi inayohitajiwa kwa kukadiria ni meta za eneo 1 kwa kila vifaranga 16. Kwa mfano nyumba yenye Meta 10 za mraba inatosha kulea vifaranga 160 hadi umri wa majuma 4. Vipimo vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa hatua 4 au hatua 3 kwa 3.25. Utajenga kutegemea na eneo ulilonalo. Baada ya majuma 4 ya umri ongeza nafasi na uwape vifaranga eneo la kuwatosha.
Sakafu: Sakafu nzuri katika nyumba ya vifaranga ikiwezekana inafaa ijengwe na simenti iliochanganywa na zege. Ili kupunguza gharama, unaweza kutumia vifaa vya ujenzi vinavyopatikana kirahisi katika eneo lako vitumikavyo kusiriba sakafu kama udongo wa kichuguu au unaweza kulainisha kinyesi cha ng’ombe kwa maji na kusiriba eneo lote la sakafu.
Ukuta: Ingefaa kuta za nyumba za kulea vifaranga za matofali, udongo, mabati au debe. Kuta za matofari na udongo zipigwe lipu ili kurahisisha usafishaji wa nyumba au umwagiaji wa dawa. Urefu wa kuta uwe tangu meta 1.8 – 2.4 (futi 6-8). Sehemu ya kutoka chini ya meta 0.9 – 1.2 (futi 3 – 4) izibwe na ukuta wa tofali au udongo na sehemu ya juu iliyobakia yenye meta 0.9 – 1.2 (futi) 3-4) ijengwe kwa wavu wa chuma au fito.
Mbao: Nguzo za miti au mbao zilowekwe dawa ya mbao kama vile “Dudu killer” au oili chafu ili kuzuia kuoza. Ukitumia miti ni vizuri uondoe magome ambayo yanaweza kuweka vimelea na wadudu.
Madirisha: Unaweza kutumia maboksi, mikeka ya magunia, mapazia ya magunia ni rahisi na yanaweza kuwekwa kwa kupigiliwa misumari kwenye dari na upande wa chini pazia ipigiliwe misumari kwenye ubao ili ininginie.Unaweza kukunja mapazia/magunia ili uingize hewa na mwanga wa kutosha katika nyumba ya vifaranga.
Paa: Mjengo wa paa uwe unaoweza kuwapatia vifaranga hewa ya kutosha hivyo paa liwe na tundu la kutoa nje hewa yenye joto. Kwa kadri utakavyoweza, unaweza kutumia madebe, mabati, makuti au nyasi n.k. kuezeka nyumba ya vifaranga. Sehemu ya paa ikianza kuvuja iezekwe bila kuchelewa.

UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA (BROILER). KATIKA ENEO DOGO LISILOZIDI MITA 1. KWA KUKU 100.




*Eneo linalohitajika ni mita mbili (2), Kwa maana ya Urefu wa mita mbili(2) na Upana wa mita moja(1).
Huu ni ufugaji wenye tija kwa wale wafugaji wenye eneo dogo.

*Kinakachofanyika katika hilo eneo ni ujenzi wa ghorofa/shelves tano(5) kwenda juu kwa ajili ya kufugia kuku.
*Urefu unaoshauriwa wa kila shelf/chumba kimoja ni futi moja na nusu hadi mbili.
*Katika kilachumba/shelf unashauriwa kuweka kuku ishirini, kwa maana ya kuku 10 katika eneo la mita 1.
*Ukichukua idadi ya kuku katika kila chumba (20) mara idadi ya vyumba 5, watapatikana kuku mia(100) katika eneo la mita 2.
*Kumbuka kuwa unaweza kufanya mabadiliko mengine kulingana na eneo utakaloweka ghorofa la kuku.

MRADI WA UFUGAJI SUNGURA KIBIASHARA.

 

KIBANDA CHA KUFUGIA
Tunasaidia kwenye ujenzi wa vibanda bora vya sungura,  kwagharama ya Tshs 65,000/=  tu    kwa kimoja cha  ukubwa  wa  futi 2.53  ,  chenye  uwezo  wa  kufugia  Sungura  mmoja  mkubwa  wakuzalisha  pamoja  na watoto wake kwa mwezi mmoja baada yakuzaliwa yaani kipindi chote cha unyonyeshwaji, na kibanda cha saizi hiyo pia kinaweza kufugia hadi sungura kumi wa umri wa miezi mitatu.
Tunashauri ujenzi wa vibanda vitatu kwa kila jike (kupata nafasi ya watoto wanaomaliza kunyonya kwani jike huzaa kila baada ya miezi 2) na pia kibanda kimoja kwa kila dume.

MBEGU
Tunawataka wakulima wetu kufuga mbegu bora na halisi ya sungura watakaotupa nyama bora kwa soko letu,  na  tunawauzia  kwa  gharama  ya  Tshs  80,000/=  kwa  kila  jike  aliyetayari  kubeba  mimba   na  Tshs 40,000/= kwa kila dume mwenye umri wakuzalisha.

MAFUNZO YETU
Tuna  mafunzo  mara  kwa  mara  pia,  na  zaidi  kuhusu  ujezi  wa  mabanda  bora,  Utunzaji  na  ufugaji  kwa ujumla, na kuhusiana na maswala ya magonjwa na namna yakuzuia.
Tuna  saini  mkataba na mkulima/mfugaji  (kwa  ada  maalum  kila  mwaka)  ambao utamuhakikishia mfugaji/mkulima  soko kwa kipindi chote cha mkataba  pale sungura wake wanapokuwa tayari kwa kuuzwa.
Tunanunua sungura katika umri wa miezi 4-5. Kwa umri huo sungura mwenye afya aliyelishwa vizuri anapaswa kuwa na uzito wa kilo 3-4, na kilo moja ya sungura akiwa hai tunamnunua kwa Tshs 8,000/=.

Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.
http://mkulimajembemfugaji.blogspot.com/p/ontact.html
Tafadhali zingatia mafunzo kwa mtunzaji wa sungura wako/au kama ni wewe mwenyewe ni ya muhimu kujifunza mambo ya msingi unapoanza mradi nasi,
Paleunapohitaji ushauri wa kitaalam utagharimia nauli ya mtaalamu atakufundisha UFUGAJI BORA WAKISASA kwa vitendo.

JINSI YA KUZALISHA AZOLLA KWA CHAKULA CHA KUKU

Habari Ndugu Mfugaji popote pale ulipo, jifunze jinsi ya kuzalisha azolla kwa chakula cha kuku na Mkulimastar.
.
Kwa maeneo mengi sana hapa nchini imekuwa changamoto hupatikanaji pamoja na bei za vyakula vya kuku, na watu wengi wamekuwa wakipata wakati mgumu na kufanya ufugaji kuwa na changamoto nyingi na hata kuhahirisha kufanya ufugaji.
Bali sasa vitambue vyakula ambavyo mfugaji unaweza zalisha katika mazingira yake kwa lengo la kulisha kuku wake.
Vifuatavyo ni vyanzo vya chakula ambavyo vyaweza tumika kulisha kuku.
- MMEA WA AZOLA.
Huu ni mmea ambao hukua ndani ya muda mfupi na uweza lisha mfugo wako wa kuku na kuwapatia chanzo kizuri cha protini pamoja na viini lishe vinginevyo.
MAZINGIRA YA UZALISHAJI
- Eneo ambalo litatumika hakikisha lina funikwa vyema kuweza zuia upotevu mkubwa wa maji, na kuchanganyana na uchafu wa ain ayeyote.
- Eneo lisiwe na shughuli nyingine kuepuka kuchanganyikana na uchafu mwingine pamoja na sumu zingine.
Jinsi ya kuotesha.
1. Andaa bwawa square mita 18 kina futi 1.5   au chombo chochote chenye ukubwa wowote unao endana na ukubwa wa eneo ulilo nalo.
2. Kisha weka nailoni ngumu au turubahi ambalo lituzuia kupotea kwa maji Kunywea chinina  Baada ya hapo weka samadi udongo kilo 27-30  mbichi ya ng`ombe ambayo itachukua eneo la inchi 10, ondoa uchafu wote hutakao jitokeza baada ya kuweka samadi juu ya maji hayo.
3. kisha weka mbegu kiasi cha kilo tatu (3), katika bwawa hilo maalumu.
4. Baada ya azola kuota Subiri kuvuna baada ya siku 15 kwa Mara ya kwanza baada ya hapo utakuwa ukivuna kila baada ya siku 2-3 kwa zaidi ya mwaka anza kuvuna na kuwapatia kuku wako, baada ya hapo anza kulisha kulingana na wingi wa mifugo ulio nao.
NAMNA YA KUWALISHA.
Kuna namna mbili kuu za kuwalisha kuku,
1. Namna  ya kwanza kwa kuwapatia  kwa kuchanganya na vyakula vingine kwa kuweka azolla kilo 50, pumba kilo 25, na kilo 25 za chakula cha madukani/ ulichochanganya mwenyewe ili kupata kilo 100
2. Namna ya pili kwa kuwapatia Chakula cha Azolla tu bila chakula kingine.

Bata Wa Kienyeji Wa Kufugwa (Bata Maji)



 















Kwa mujibu wa Wikipedia, Bata ni ndege wa maji wa familia ya Anatidae wenye mdomo mfupi na mipana na miguu yenye ngozi kati ya vidole. Manyoya yao huwa na uwezo bora wa kufukuza maji kwa msaada wa mafuta maalumu. Bata ndiyo moja ya familia za ndege ambazo spishi zao zina uume.
Mwili wote wa bata kwa ujumla ni mrefu na mpana, na bata wengi kwa wastani wana shingo fupi lakini shingo la bata bukini na bata-maji ni ndefu.
Umbo la mwili la mabata kwa kiasi fulani hutofautiana na hawa kwa kuwa kidogo wa duara kidogo. Miguu yenye magamba ni yenye nguvu na iliyokuwa vizuri, na kwa kawaida, na hurushwa nyuma kabisa ya mwili, hivyo zaidi hasa kwenye spishi za majini.
Mbawa zake ni zenye nguvu na kwa ujumla ni ndogo na zilizochongoka, na kupaa kwa bata kunahitaji mapigo ya haraka bila ya kupumzika, hivyo kuhitaji misuli yenye nguvu sana. Hata hivyo spishi tatu za bata aina ya steamer hawawezi kuruka kabisa.
Spishi nyingi za bata hushindwa kuruka vizuri kipindi cha kupukutisha manyoya ya zamani na kuotesha mapya; hutafuta mazingira salama yenye chakula kingi wakati huo. Hivyo basi kipindi hiki hufuata baada ya kipindi cha kuhama.
Ndege hawa wana rangi mbalimbali. Spishi kubwa hutafuta chakula aghalabu ardhini au kwa maji machache. Spishi ndogo nyingine hula mimea ya maji na huzamia kichwa chao tu, nyingine huzamia kabisa ili kukamata samaki, wanyamakombe au mimea ya maji, lakini spishi kadhaa hutafuta chakula ardhini.
Hujenga matago yao ardhini, juu ya mwamba, ndani ya shimo la miti au ndani ya pango la sungura, mhanga.
Manyoya ya spishi kadhaa hupendwa sana kama kijazo cha mito, mifarishi, mafuko ya kulalia na makoti. Spishi nyingi za mabata hutumika kama chakula.

Matumizi sahihi ya viatilifu

Kila mwaka, viatilifu vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 38
huongezwa katika mazingira kwa makusudi ikiwa ni matumizi ya kawaida ya
binadamu. Katika siku za hivi karibuni, tanzania imekua moja kati ya watumiaji
wanaokua wa viatilifu.

Sehemu kubwa ya viatilifu hivi ni sumu za viwango vya juu na vina madhara ama ya papo kwa papo ama ya muda mrefu kwa afya ya binadamu, wanyama, mimea na wadudu.
Madhara ya muda mrefu ni pamoja na saratani, matatizo ya uzazi, kuharibika kwa homoni na uharibifu wa kinga ya mwili. Madhara haya hutokana na kutumia viatilifu hivi
moja kwa moja, kuvuta wakati wa kupulizia, kuosha nguo zenye sumu baada ya kazi
na kutunza viatilifu katika nyumba za kuishi.


Namna ya kutumia viatilifu kwa usahihi na usalama
1) 
Vaa mavazi sahihi ya kukukinga
Watu wanaofanya kazi ya kupuliza ama kunyunyiza
sawa mashambani ama katika sehemu nyingine wapo katika hatari ya kugusa, kuvuta
hewa, ama kula sumu kwa bahati mbaya ama kwa kuto kujua.
Mavazi yenye kukinga mwili yatumike ilu
kumuepusha mtumiaji wa viatilifu kuathirika na sumu.
Mavazi hayo ni pamoja na:
·        Kofia
·        Shati la mikono mirefu
·        Suruali
·        Buti (gunboot)
·        Soksi na glovu
·        Miwani
·        Kifaa cha kukinga pua
2)    Zuia watu na wanyama kuingia eneo lililopuliziwa viatilifu baada tu ya kutumia
viatilifu
Taasisi ya kulinda mazingira (EPA) imeweka muda kwa kila kiatilifu ambapo binadamu na
wanyama wanaweza kuingia katika eneo lililopuliziwa kwa usalama. Muda wa
kungoja unategemea aina ya sumu iliyotumika.
Ni vema shamba likipuliziwa sumu liwekewe alama ama ishara inayoonesha hakuna
kuingia shambani. 
Kwa kawaida, usiingie shambani wakati majani bado yamelowa sumu japo zipo baadhi ya sumu ambazo hata kama majani yamekausha sumu hutaruhusiwa kuingia.
NB: Taasisi ya kulinda mazingira =The Environmental Protection Agency (EPA)
3) 
Tumia kiatilifu sahihi kwa kupambana na kisumbufu vilivyopo
Visumbufu vipo vya aina mbalimbali kama vile wadudu, fangasi, magugu, wanyama (kama
panya) hivyo ni muhimu kufahamu sumu zipi ni maalumu kwa kundi lipi la
visumbufu. Mfano, kutumia dawa ya wadudu kuangamiza magugu hakutaleta matokeo
kabisa badala yake kutasababisha sumu kutapakaa katika mazingira.
4)    Tumia kiasi sahihi cha sumu
Katika vibandiko (lebo) za viatilifu, watengenezaji hutaja kipimo cha sumu inayotakiwa
kwa ajili ya kuangamiza visumbufu. Mfano, tumia mililita 10 za dawa kwa lita
moja ya maji endapo majani ni machanga na tumia mililita  15 za dawa kwa kila lita ya maji endapo majani yamekaribia kuchanua.
5)    Tumia sumu yako katika mazingira sahihi
Mazingira yanaweza kusababisha sumu inayotumika kuleta madhara. Sma kibandiko cha dawa na utapata maelezo ya katika mazingira gani sumu hiyo inaweza kutumika kwa usalama zaidi. Mfano, usinyunyize sumu wakati wa upepo mkali maana upepo huweza
kuhamisha sumu na kuipeleka mahali kusiko kusudiwa. Pia sumu isitumike wakati
wa joto kali kama vile mchana kwani joto kali huweza kusababisha sumu kuvukizwa
kwa urahisi hivyo kuisambaza katika hewa.
6)    Tumia njia na kifaa sahihi katika kutumia sumu
Vipo vifaa mbalimbali vinavyotumika katika kusambaza viatilifu katika mashamba ama
maeneo lengwa. Watengenezaji wa sumu husika hutoa maelekezo ya namna na vifaa
sahihi vya kutumia. Mfano, changanya na maji safi na nyunyiza au usichanganye
na kitu chochote, itumike kama ilivyo kwa kunyunyiza katika mazao.


Wednesday, October 5, 2016

Uzalishaji wa vitunguu wenye tija, udhibiti wa Wadudu na Magonjwa ya Vitunguu

Zao la vitunguu hulimwa duniani kote kwa ajili ya kutumika kama kiungo cha chakula. Kila familia angalau hutumia kitunguu mara moja klia siku katika chakula chao. Vitunguu hutumika kama dawa katika baadhi ya jamii na wataalamu wanasema hupunguza shinikizo la juu la damu na kupunguza matatizo mengine ya moyo.

Ili uweze kuzalisha mazao ya jamii ya kabichi unahitaji vitu vifuatavyo:

i) Ardhi yenye rutuba.

ii) Mbegu bora ya vitunguu; k.m Red Creole kutoka ktk chanzo cha kuaminika

iii)  Uwezekano wa kupata maji.

iv)  Dawa za kudhibiti magugu, wadudu na magonjwa.
Uchaguzi wa mbegu bora
Mbegu bora ichaguliwe kwa kuzingatia sifa zifuatazo:

1)     Iwe na ustahimilivu dhidi ya magonjwa na wadudu.

2)     Yenye kutoa mavuno mengi.

3)      Inayokomaa mapema ilu kuwahi soko.

4)     Inayoendana na hali ya hewa ya eneo shamba lilipo.

Uchaguzi wa eneo kwa ajili ya kitalu na shamba:
Udongo – vitunguu ni zao la kina kifupi, udongo uwe laini na usio na mawe wala mabonge ili kuruhusu ukuaji wa kitunguu. pH ya 6-7 na usiotuamisha maji.

 Hali ya hewa: joto la sentigredi 15 – 25

Kupanda moja kwa moja shambani
Ingawa zipo baadhi ya faida za kupanda mbegu za vitunguu moja moja kwa moja shambani (direct seeding) kama kuepuka usumbufu wa kutunza kitalu, njia hii sio maarufu sana miongoni mwa wakulima ukilinganisha na ile ya kutumia kitalu. 
Miche ya vitunguu itakua tayari kwa kupandikizwa kati ya wiki 6 hadi 8 baada ya kupanda kitalu. Wakati wa kupandikiza, itawanye mizizi sawasawa kadri ilivyojipanga katika shina kabla ya kufukia na kushindilia kiasi.
Muhimu; wiki mbili kabla ya kuhamisha miche kutoka kwenye kitalu kwenda kuipandikiza shambani, unatakiwa kuipa miche mazingira halisi ya shambani kwamfano kupunguza kiwango cha maji na kuiondolea kivuli. Hii husaidia kupunguza uwezekano wa miche kufa pindi inapo amishiwa kwenye mazingira mapya ya shamba.

Wadudu waharibifu wa vitunguu
Jina la mdudu
Thiripi (Thrips): Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha majani kuwa na doti nyeupe. Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia.
Thrips huudhibitiwa kwa kunyunyuzia dawa iitwayo Protrin 60 EC.
Kimamba: Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.
Wadudu hawa huthibitiwa kwa kunynyuzia dawa Metakan super 350 SE


Sota (Cutworms): Sota au viwavi wa nondo wanasababisha uharibifu mkubwa. Viwavi wanakata mashina ya miche michanga sehemu ya chini ya shina juu ya ardhi. Sota wanapendelea kula wakati wa usiku na mchana kujificha kwenye ardhi karibu sana na sehemu waliokata shina. Uharibifu huu unapunguza sana idadi ya mimea shambani na kuleta upungufu wa mazao.
Wadudu hawa wanadhibitiwa kwa kupulizia dawa kama; PROTRIN 60 EC, Agromectin 1.8 EC ambayo hutumika ndani ya wiki 0-7 na Metakan super 350 EC nayo hutumika ndani ya wiki 8-20.
Utitiri wekundu (Red spider mites)
Hawa ni wadudu wadogo sana, ambao wanajificha upande wa chini wa majani. Wanafyonza maji maji kwenye majani na kusababisha majani kuwa na rangi nyeupe. Wadudu hawa wanatengeneza utando mweupe kuzunguka majani na mashina. Mmea unashindwa kutengeneza chakula na baadaye inakufa.
Njia ya kudhibiti:
kupulizia dawa za wadudu AGROMECTINE 1.8 EC.
 Vipekecha majani (leaf miner)
Hawa ni aina ya inzi wadogo, ambao viwavi wake wanashambulia majani, kwa kupekecha na kutengeneza mitandao wa mitaro kwenye majani. Viwavi wanashambulia majani na kusababisha majani kukauka. Upungufu mkubwa wa mazao hutokea.
Njia ya dhibiti:
kupulizia dawa ya wadudu kama AGROMETHRIN 10 EC 
kuteketeza masalia ya mazao
kutumia mzunguko wa mazao                    

Magonjwa ya vitunguu
Ugonjwa
Dalili za ugonjwa ni:-
Picha
Baka zambarau (Puple Blotch)
Ungonjwa huu unasababishwa na kuvu (fangasi). Chanzo kikubwa cha ugonjwa ni mbegu zenye ugonjwa. Pia ugonjwa unajitokeza wakati kuna ukungu na unyevunyevu mwingi hewani hasa wakati wa masika.
Kiasi cha 60-80 % ya mazao yanaweza kupotea kama ugonjwa hautadhibitiwa.
ü madoa meupe yaliyodidimia kwenye majani na mashina
ü rangi ya zambarau kuwepo katikati ya doa jeupe.
ü majani kuanguka
Kinyausi (Damping – off)
Ugonjwa huu unasababishwa na fangasi na kuenezwa na udongo, mbegu na masalia ya mazao. Ugonjwa unajitokeza hasa kitaluni ikiwa hali ya hewa ina unyevunyevu na udongo una maji maji.
Kudhibiti: mbegu ziwe safi na ziwekwe dawa ya  AGROZEB 80WP
ü mbegu kuoza kabla ya kuota na kunyauka kwa miche baada ya kuota
Virusi njano vya vitunguu (Onion yellow Dwarf virus)
Ugonjwa huu unasababishwa na virusi na kuenezwa na wadudu aina ya vidukari (wadudu -mafuta).
Kudhibiti ugonjwa huu ni:-
Kutumia mbegu safi
Kuweka shamba katika hali ya usafi
Tumia PROTRIN kuua Wadudu wanaosambaza ugonjwa
Mistari ya rangi ya manjano kwenye majani.
Kujikunja kwa majani
Majani kugeuka rangi ya manjano na kuanguka
Mimea mzima kudumaa, kujikunja na kufa.
asteryellows1_600px.jpg
Ukungu mweusi
Onion Black Mold
Kisababishi: Aspergillus niger
Maranyingi hutokea endapo joto litakua kali.
Kudhibiti: mbegu ziwe safi na ziwekwe dawa ya  AGROZEB 80WP
Agromenol 250EC
Utando mweusi katika gamba la kitunguu.
Kuoza shingo na kirungu
Onion Botrytis Neck and Bulb Rot
Kisababishi : Botrytis allii
Japo Ugonjwa huu huonekana wakati vitunguu vimehifadhiwa, maambukizi huanzia shambani.
Tumia Agromenol 250EC
Kudumaa
Sehemu zilizoathirika hukauka na kufa.
Gamba gumu katika shingo ya kitunguu.
Ubwiri unyoya
Onion Downy Mildew
Kisababishi: Peronospora destructor
Kudhibiti: Meronil 720 EC, rudia kila baada ya siku 7
Manyoya ya kijivu-meupe katika majani ya umri mkubwa.
Kutu
Kisababishi: Puccinia porri
Tumia Agromenol 250EC, Meronil 720 EC, Sipron Star 330 EC
Majani yalioathirika huwa na madoa ya rangi ya machungwa
Baadaye hugeuka na kuwa meusi
Majani yaliyoathirika sana huwa ya njano na hatimaye hufa.

ü  kutumia mzunguko wa mazao
ü  kusia mbegu kwa nafasi za kutosha
ü  kuepukana na kubananisha miche kitaluni
ü  Kuepukanana na kumwagilia maji wakati wa jua kali au wakati kuna ukungu.
ü  kupanda mbegu safi
ü  kupanda vitunguu kwa kutumia mzunguko wa mazao
ü  kuteketeza msalii ya vitunguu baada ya kuvuna

Fahamu mbinu za kuongeza thamani nyama

  Safari ya kuongeza thamani nyama ya mifugo huanzia shambani kwa usimamizi wa ufugaji na uzalishaji. Lishe bora ni muhimu kwa wa ufugaji ...