BANDA LA KULELEA VIFARANGA
Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufi kirie yafuatayo:-
a) Nyumba ya vifaranga iwe karibu na nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua vifaranga wako mara kwa mara.
b)
Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga
mojawapo ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.
c)
Nyumba ya vifaranga isiruhusu ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu
kuingia. Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.
d) Nyumba iwe na eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.
e)
Ijengwe kwenye sehemu isiyoelekea upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku
wakubwa. Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa
yanayoenezwa na upepo.
Eneo: Vifaranga
hawahitaji eneo kubwa katika muda wa majuma 4 ya kwanza. Nafasi
inayohitajiwa kwa kukadiria ni meta za eneo 1 kwa kila vifaranga 16. Kwa
mfano nyumba yenye Meta 10 za mraba inatosha kulea vifaranga 160 hadi
umri wa majuma 4. Vipimo vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na
hatua 5 kwa hatua 4 au hatua 3 kwa 3.25. Utajenga kutegemea na eneo
ulilonalo. Baada ya majuma 4 ya umri ongeza nafasi na uwape vifaranga
eneo la kuwatosha.
Sakafu: Sakafu
nzuri katika nyumba ya vifaranga ikiwezekana inafaa ijengwe na simenti
iliochanganywa na zege. Ili kupunguza gharama, unaweza kutumia vifaa vya
ujenzi vinavyopatikana kirahisi katika eneo lako vitumikavyo kusiriba
sakafu kama udongo wa kichuguu au unaweza kulainisha kinyesi cha ng’ombe
kwa maji na kusiriba eneo lote la sakafu.
Ukuta: Ingefaa
kuta za nyumba za kulea vifaranga za matofali, udongo, mabati au debe.
Kuta za matofari na udongo zipigwe lipu ili kurahisisha usafishaji wa
nyumba au umwagiaji wa dawa. Urefu wa kuta uwe tangu meta 1.8 – 2.4
(futi 6-8). Sehemu ya kutoka chini ya meta 0.9 – 1.2 (futi 3 – 4) izibwe
na ukuta wa tofali au udongo na sehemu ya juu iliyobakia yenye meta 0.9
– 1.2 (futi) 3-4) ijengwe kwa wavu wa chuma au fito.
Mbao: Nguzo
za miti au mbao zilowekwe dawa ya mbao kama vile “Dudu killer” au oili
chafu ili kuzuia kuoza. Ukitumia miti ni vizuri uondoe magome ambayo
yanaweza kuweka vimelea na wadudu.
Madirisha: Unaweza
kutumia maboksi, mikeka ya magunia, mapazia ya magunia ni rahisi na
yanaweza kuwekwa kwa kupigiliwa misumari kwenye dari na upande wa chini
pazia ipigiliwe misumari kwenye ubao ili ininginie.Unaweza kukunja
mapazia/magunia ili uingize hewa na mwanga wa kutosha katika nyumba ya
vifaranga.
Paa: Mjengo
wa paa uwe unaoweza kuwapatia vifaranga hewa ya kutosha hivyo paa liwe
na tundu la kutoa nje hewa yenye joto. Kwa kadri utakavyoweza, unaweza
kutumia madebe, mabati, makuti au nyasi n.k. kuezeka nyumba ya
vifaranga. Sehemu ya paa ikianza kuvuja iezekwe bila kuchelewa.
Comments
Post a Comment