KILIMO BORA CHA PILIPILI MANGAKILIMO BORA CHA PILIPILI MANGA: Pilipili mtama au
kwa jina lingine pilipili manga ni kiungo muhimu sana katika mapishi.
Radha yake ya muwasho ndio kitu hasa kinachotafutwa katika vipunje
vidogo vidogo vya zao hili. Pilipili manga husagwa ili kupata ungaunga
kabla ya kutumika ingawa pia inaweza kutumika bila kusagwa.
Jina la kitalaam ni Piper nigram na kwa kiingereza ni black pepper.
Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika
mkoa wa Tanga na Zanzibar. Ingawa pia inaweza kukubali katika maeneo ya
Kagera
Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki
na kwa mapishi mengine mbalimbali. Nchi za magharibi zina matumizi
makubwa ya viungo hivi. Aidha pilipili mtama nyeusi ndiyo huzalishwa
zaidi hapa nchini.
Namna ya uzalishaji wa pilipili manga.
Hali ya hewa na udongo
Viungo vingi humea katika maeneo yenye joto la wastani kati ya nyuzi
joto 24-26 na huzalishwa maeneo ya mwambao. Udongo wenye rutuba na
unaopitisha maji na wenye uchachu wa kiasi cha pH 6.5. Mahitaji ya mvua
ni mililita 1500-2000 kwa mwaka.
Uchaguzi wa mbegu
Uchaguzi huzingatia mambo yafuatayo:-
a) Urefu wa pingili na ukubwa wa majani
b) Ufupi wa pingili unaoambatana na majani madogo.
Tofauti iko hadi kwenye umbile la matunda. Majani ya mche mama sehemu
kinapokatwa kipando huondolewa wiki mbili kabla ya kukata. Vipando
vyenye macho (nodes) 3-4 humika. Macho mawili huzikwa kwenye udongo na
kipando kiwekewe kivuli. Inashauriwa kuweka mbolea ya samadi wakati wa
kupanda. PILIPILI MANGA
Nafasi ya upandaji
Nafasi ya kupanda ni mita 2-3 kati ya mmea na mmea endapo miche imepandwa na miti inayotakiwa kupogolewa mara kwa mara.
Mahitaji ya mbolea
Matumizi ya mbolea hapa Tanzania si makubwa katika kilimo cha viungo.
Ingawa kiasi cha kilo 0.4 cha Urea, kilo 0.3 cha Superphosphate na kilo
0.3 cha Potash ya Muriate kinaweza kutumika kwa miche mikubwa.
Miti ya kusimikia miche
Miche hupandwa kwa kusimikiwa nguzo ili ikue kwa kujizungusha kwenye
miti kama mijenga ua, n.k. Mti huo wa kusimikia nao pia hupaswa
kupunguziwa majani ili kupunguza giza. Kila kabla ya msimu miti hiyo
hupaswa kupunguziwa matawi (pruning). Kupogolea miche ya pilipili mtama
Mche ukifikia miezi 18 inapaswa kupogolea kwa kukata sehemu ya juu ya
mche ili kufanya matawi mengine yachipue chini ya mche. Inashauriwa
mche kuwa na urefu wa mita 3-3.5.
Uvunaji
Maua ya kwanza hutoka baada ya miaka miwili. Matunda hukomaa miezi
tisa (9) hadi kumi (10). Uvunaji ni mizunguko 5 hadi 6 kwa mwaka.
Pilipili mtama inaweza kuvunwa kwa misimu miwili. Mavuno ni kati ya tani
0.35 – 3.75 kwa hekta. Wakati wa uvunaji kishina cha matunda ya kijani
hukatwa kutoka kwenye mti kisha mbegu za huchambuliwa kutoka kwenye
vishina na kisha huanikwa juani kwa siku 3 hadi 4 ili kuhakikisha
zinakauka vizuri kabisa. Kiasi cha unyevu kiwe angalau 13 – 14%. PILIPILI MTAMAKuhifadhi
Pilipili mtamailiyokaushwa vizuri inaweza ikawekwa kwenye chombo kisichopitisha hewa na kudumu kwa miaka hadi 20 bila kuharibika. Masoko ya pipili mtama
Soko la pilipili matama linapatikana ndani ya nchi na nje pia. Bei ya
ndani ni kati ya Sh1,000-1,500. Zao hili huuzwa katika nchi za Uganda,
Kenya, Uingereza, Ujerumani, Mashariki ya Kati, n.k. Bei ya Nje ni
wastani wa dola za kimarekani 1,985 kwa tani. (Tafadhali fanyia utafiti
soko, data hizi ni za siku nyingi)
KILIMO BORA CHA VITUNGUUKILIMO BORA CHA VITUNGUU:
Hapo awali kitungu kilikuwa ni zao lililokuwa linapatikana porini
katika ukanda wa bahari ya Mediterania. Zao hili hulimwa katika nchi
nyingi za magharibi, nchi za milima zilipo kaskazini mwa dunia, likwemo
bara la Afrika. Vitunguu hustawi katika hali ya hewa ya jotoridi 13°C –
24°C, hali ya hewa inayofaa kwa kuotesha na kukuzia miche kwenye kitalu
ni jotoridi 20°C – 25°C. Kwa kawaida vitunguu huhitaji kiasi cha joto
nyuzi 20°C-25°C ili kuweza kustawi na kukua vizuri. Joto zaidi ya hapo
hufanya vitunguu kudumaa na kutoweza kutengeneza viazi (bulbs).
KILIMO CHA VITUNGUUMatumizi
Kitunguu hutumika kama kiungo cha kuongeza ladha kwenye chakula, na pia hutumika kama dawa ya kansa ya tumbo, vidonda na majipu. Ustawi
Zao la vitunguu hustawi katika udongo wa tifu tifu wenye mbolea ya
kutosha, ukiwa na uchachu wa udongo (PH) kiasi cha 6 – 6.8. Udongo wa
mfinyanzi haufai kwa zao la vitunguu kwa kuwa hauruhusu viazi vya
vitunguu (bulbs) kutanuka. Hivyo uwezekano wa kupata mazao ni mdogo.
Pia udongo wa kichanga haufai kwa zao la kitunguu kwa kuwa hauna mbolea
na hivyo vitunguu huwa vidogo sana, jambo ambalo ni vigumu kupata mazao
yanayofaa kwa soko.
Zao la kitunguu huhitaji unyevu muda wote wa ukuaji wake. Zao hili
lina mizizi mifupi hivyo linahitaji kumwagiliwa maji mara kwa mara. AINA ZA VITUNGUUAINA ZA VITUNGUU
Kuna aina mbili za vitunguu ambazo zimezoeleka:
Vitunguu vya asili kama vile Singida, na Rujewa (aina hii ina rangi ya kahawia iliyopauka).
Chotara: Hii ni aina ya vitunguu inayojulikana kama vitunguu vya
kisasa. Katika kundi hili kuna vitunguu kama Texas grano, Red creole,
Bombay red, White granex, na Super rex.
Mgawanyiko
Zao la vitunguu limegawanyika katika makundi mawili. Hii inatokana na
uhitaji wa mwanga na ukuaji wake. Aina ya kwanza inahitaji mwanga kwa
saa 8-13 ili kuweza kuchanua na kutoa mbegu.
Aina ya pili inahitaji mwanga kwa saa 13-15 kuweza kuchanua na kutoa mbegu. UPANDAJI WA VITUNGUUKupanda
Vitunguu hupandwa kwa kutumia mbegu ambazo husiwa kwenye vitalu. Kitalu
kinaweza kuwa na upana wa mita 1, urefu unategemeana na ukubwa wa eneo
ulilo nalo.
Unaweza kupanda vitunguu kwenye matuta mbonyeo (Sunken bed). Aina hii
ya upandaji hutumika kwenye eneo lenye shida ya maji. Upana wa tuta uwe
mita moja.
Kupanda kwenye matuta mwinuko (Raised bed) upandaji wa iana hii hutu mika sehemu yenye maji mengi au yanayotuama.
Tahadhari: Maji yakituama kwenye vitunguu hufanya vitunguu kuoza, hivyo kuathiri mavuno. Nafasi
Vitunguu vipandwe kwa nafasi ya sentimita 7.5 kutoka mche hadi mche,
sentimita 12.5 kutoka mstari mmoja hadi mwingine kwenye matuta. UDONGO MZURI KWA VITUNGUUMbole ya kupandia
Unaweza kutumia mboji, au samadi iliyo oza vizuri kupandia. Baada ya
hapo unaweza kuongeza mboji baada ya miezi miwili. Endapo unafanya
kilimo kisichozingatia misingi ya kilimo hai, unaweza kupanda kwa
kutumia mbolea aina ya NPK (20:10:10) baada ya mwezi na nusu, unaweka
mbolea ya Urea. Palizi
Vitunguu ni zao lenye uwezo mdogo sana wa kushinda na magugu. Hivyo, inabidi shamba liwe safi muda wote wa ukuaji hadi kuvuna. UVUNAJI VITUNGUUUvunaji
Kwa kawaida, vitunguu huchukua muda wa miezi 5-6 tangu kupandwa hadi
kuvunwa. Unaweza kuanza kuvuna vitunguu baada ya asilimia 75 ya shingo
za vitunguu kuvunjika. Baada ya kuvuna, unaweza kuweka kwenye madaraja
(grades) kwa kufuata ukubwa, rangi na unene wa shingo ya kitunguu.
Vitunguu vyenye shingo nyembamba hudumu zaidi, vyenye shingo nene huoza
haraka. Ukataji
Hakikisha kuwa shingo ya kitunguu inabaki kiasi cha sentimita 2. Hii husaidia kuzuia kuoza haraka. Namna ya kuhifadhi vitunguu
Baada ya kuvuna, hifadhi vitunguu kwenye kichanja chini ya kivuli na
uvitandaze vizuri. Unaweza kuhifadhi vitunguu kwa kufunga kwenye
mafungu na kuvitundika. Vitunguu vikihifadhiwa vizuri vinaweza kukaa
hadi miezi minne bila kuharibika, hii hutegemeana na aina ya uhifadhi.
Wadudu wanaoshambulia vitunguu
Kuna aina nyingi za wadudu wanaoweza kushambulia vitunguu. Hawa
wafuatao ni baadhi ya wadudu waliozoeleka kwenye zao la vitunguu. WADUDU WABAYA
Thiripi (Thrips): Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na
shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na
kusababisha majani kuwa na doti nyeupe.
Madhara: Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia
KITUNGUU
Kimamba: Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza
ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni
hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.
Minyoo fundo (Nematodes): Aina hii ya minyoo hushambulia mizizi ya
vitunguu. Hali hii husababisha kudumaa kwa vitunguu kwa kuwa hushindwa
kufyonza maji na chakula kutoka ardhini.
Vidomozi (Leaf minor): Hushambulia majani kwa kujipenyeza kwenye
ngozi ya jani na kusababisha michoro ambayo huathiri utendaji wa majani.
Utitiri mwekundu (Red spider mites): Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani na kusababisha vitunguu kunyauka.
Funza wakatao miche: Funza hawa hutokana na wadudu wajulikanao kama Nondo, na hushambulia shina na kulikata kabisa. Namna ya kukabiliana na wadudu hawa
Unaweza kukabiliana na wadudu hawa kwa kufanya kilimo cha mzunguko.
Usioteshe vitunguu sehemu moja kwa muda mrefu, au kufuatanisha mazao
jamii ya vitunguu kama vile leaks.
Tumia mbegu bora zilizothibitishwa kutoka kwenye kampuni
zinatambuliwa kisheria na kibiashara. Kupanda kwa wakati unaotakiwa;
vitunguu visipandwe wakati wa kiangazi. Vipandwe wakati wa majira ya
baridi na kuvunwa wakati wa joto. Tumia dawa za asili za kuulia wadudu,
au dawa nyinginezo zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo. UGONJWA KWA VITUNGUU
1. Purple blotch: Ugonjwa huu husababishwa na ukungu (fungus).
Ugonjwa huu husababisha mabaka ya zambarau na meusi katika majani ya
vitunguu. Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu unyevu mwingi.
Madhara: Ugonjwa huu hupunguza mavuno mpaka asilimia hamsini (50%).
2. Stemphylium leaf blight: Hukausha majani kuanzia kwenye ncha hadio
kwenye shina.; Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu na ukungu mwingi.
Madhara: Hupunguza mavuno hadi kwa asilimia sabini na tano (75%).
VITUNGUU
Magonjwa ya virusi (Onion yellow draft virus): Ugonjwa huu
husababisha vitunguu kuwa na rangi iliyochanganyika, kijani na michirizi
myeupe au njano. Vitunguu hudumaa kwa kiasi kikubwa;Ugonjwa huu
husababishwa na kimamba.
Madhara: Huathiri mavuno kwa asilimia 80 mpaka asilimia 100%.
4. Kuoza kwa kiazi (Bulb rot): Husababishwa na fangasi. Ugonjwa huu
hutokea vitunguu vikishakomaa, huku udongo ukiwa na maji maji. Vitunguu
vikishakomaa visimwagiliwe tena. Uharibifu wa vitunguu usiotokana na magonjwa
1. Kuchipua baada ya kuvunwa: Hali hii hutokea endapo vitunguu vitavunwa
kabla ya muda wake. Endapo vitunguu havitakaushwa vizuri baada ya
kuvunwa. Hali hii husababisha uharibifu mpaka asilimia themanini (80%).
Sehemu ya kukaushia vitunguu iwe na hewa inayozunguka na mwanga wa
kutosha. Vitunguu vikiwekwa gizani huchipua kwa urahisi.
2. Muozo laini (Soft rot): Ugonjwa huu hushambulia vitunguu baada ya
kukomaa; husababishwa na vimelea (bacteria). Vitunguu hutoa harufu mbaya
ya uozo. Kuepuka hilo vuna kwa wakati unaofaa, hifadhi sehemu yenye
mwanga na hewa inayozunguka.
MAGONJWA MABAYA KWA VITUNGUUVirusi
Unaweza kuzuia vimamba ambao ndio wanaoeneza virusi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu. Vitunguu vinalipa
“Vitunguu vinatofauti kidogo na mazao mengine ya mboga mboga kwa kuwa
si rahisi kukosa soko, na endapo bei si nzuri unaweza kuhifadhi kwa
muda ili kusubiri bei iwe nzuri.” Ni maneno ya mkulima Peniel Rodrick
(pichani) ambaye amejikita zaidi katika kilimo cha vitunguu kibiashara.
Mkulima huyu kutoka kijiji cha Oloigeruno anasema pamoja na kwamba
anazalisha pia mazao mengine, lakini ameamua kujikita zaidi kwenye
vitunguu baada ya kugundua siri na namna ya kupata faida zaidi.
Toka aanze kilimo cha vitunguu miaka 12 iliyopita, ameweza kuendesha
maisha yake vizuri, ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mingine kama
ufugaji wa ng’ombe, kujenga nyumba ya kisasa na kuitunza familia yake ya
watoto watatu ipasavyo. Pamoja na hayo anasema tatizo kubwa la vitunguu
ni magonjwa na wadudu. Anasema si rahisi sana kugundua mara moja kuwa
kuna ugonjwa unaoshambulia vitunguu, na mara unapogundua unakuwa
umefikia kwenye hali mbaya
KILIMO BORA CHA KABICHIKILIMO BORA CHA KABICHI :
Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika
katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama
malisho ya mifugo
Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha
mimea ya kaulifulawa (cauliflower ), kabichi ya kichina na kale. Kwa
kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa
ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa
sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka.
Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa
baada ya kufunga na kukomaa vizuri.
Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida,
huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa
kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).
Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi.
Hali ya hewa: Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya
baridi, hali ya joto jingi haifai kwa kabichi kwa kuwa huathiri uotaji
na ukuaji wake. Joto jingi pia husababisha kulegea kwa vichwa
vilivyofunga. Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi
ya mita 100 toka usawa wa bahari.
Udongo: Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote
mradi tu udongo huo usiwe na chumvichumvi nyingi na usiotuhamisha maji.
Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi
kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo.
Kitalu: Kitalu ni muhimu katika uzalishji wa zao hili. Ni vema
kutengeneza matuta yenye upana wa mita moja, na urefu wowote kulingana
na matakwa ya mkulima.
Mbolea za samadi na zenye asili ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye
udongo. Kiasi cha gramu 500 za mbegu huhitajika kwa hekta moja. Katika
upandaji kwenye kitalu ni vizuri kutengeneza mistari katika tuta, umbali
toka mstari hadi mstari uwe sentimita ishirini (20). Udongo kiasi
kidogo utumike katika kufunika mbegu.
Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya miche na uwe katika kipimo cha sentimita 2-3 toka mche hadi mche.
Hii itasaidia kuwa na miche mifupi na yenye nguvu. Inafaa kunyeshea
kitalu mara moja au mbili kwa siku na katika sehemu za joto ni vizuri
kuweka kivuli katika matuta. Katika wiki ya tatu, hadi wiki ya nne, ni
vyema kuondoa kivuli kidogo kidogo huku ukipunguza unyeshaji. Hali hii
itasaidia miche isipate mshtuko wa uhamishaji shambani. Kuhamisha na kupanda
Hamisha na kupandikiza miche shambani ikiwa na umri wa wiki nne, wakati
huo miche ikiwa na majani manne ya mwanzoni na urefu wa kiasi cha
sentimita kumi na mbili (12). Wakati wa upandaji, ni vizuri udongo
ukashindiliwa kwenye kila mche. Inafaa upandaji ufanyike mara moja, na
ni vizuri ukafanyika nyakati za jioni au asubuhi sana, na udongo uwe na
unyevu wakati wote. Nafasi kati ya mmea
Katika mstari hadi mstari inatakiwa iwe sentimita 60-75. Kutoka mmea
hadi mmea ni sentimita 30-60. Pia sentimita 75-90 inaweza kutumika kati
ya mstari na mstari.
Mbolea: Ni vizuri kuweka kiasi cha viganja 2-3 vya mbolea ya samadi iliyooza vizuri katika kila shimo.
Palizi: Wakati wa palizi ni vizuri mkulima akawa mwangalifu ili
asiharibu mizizi. Wakati kabichi inapoanza kufunga hufunika ardhi,
hivyo, husaidia kuzuia magugu yasiote, kwa wakati huu hakuna haja ya
kupalilia.
Kuvuna: Kabichi hukomaa katika kipindi cha siku 60-100 tangu
kupandwa. Kwa ajili ya kuuza ni vizuri kuvuna wakati vichwa vinapofunga
vizuri na huwa na uzito wa kutosha kabichi iangaliwe na kutunzwa baada
ya kuvunwa ili isikwaruzwe na kuoza kabla ya kutumiwa. Kwa kawaida hekta
moja hutoa mavuno kiasi cha tani 50-80. Aina za kabichi
Kuna aina nyingi za kabichi na zifuatazo ni miongoni mwa aina hizo: Early Jersey wakefield – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5 Sugar loaf – Aina hii hukomaa mapema sana, kiasi cha miezi 2.5 Glory of enkhuizen – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5 Prize drumhead – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5 F1-High Breed – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 2-4 Duncan – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3
KILIMO BORA CHA NYANYAKILIMO BORA CHA NYANYA : Nyanya ni zao la mboga
ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya
Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama
zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za
ulimwengu. matandazo kwa ajili ya nyanyaUzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania
Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na
Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na
Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo
Kenya, uganda na Tanzania.
Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa
nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa
Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578
ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya
kilimo ya Tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa
Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta),
Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida.
Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji
wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la
uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya
bado ni mdogo sana.
Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi,
upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za
nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu,
magonjwa na magugu. UDONGO KWA AJILI YA NYANYAMazingira
Hali ya Hewa:
Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia
nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa
ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.)
• Udongo:
Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga,
mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya
kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani
yaani pH 6.0 – 7.0.
AINA ZA NYANYA Aina za Nyanya
Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili:
1. Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina hizi
hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni
wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo
miezi 6 ni ya uvunaji.
2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa) Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili:
OPV (Open Pollinated Variety) – Aina za kawaida
Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.
Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na
wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na
zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku
nyingi bila kuharibika mapema.
Kuandaa Kitalu cha Nyanya Mambo muhimu ya kuzingatia:
Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo
ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao
sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo.
Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.)
Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi,
ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia
kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine.
Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za NyanyaKuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya
Aina ya matuta:
matuta ya makingo (sunken seed bed)
matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed)
matuta ya kawaida (flat seed beds)
Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta
Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili
mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila
kukanyaga miche].
Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.
Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.
Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au
mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo.
Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba.
Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia
usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili
kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini
mno kiasi ambacho hazitaota.
Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu
1. Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds);
matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi.
Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi
Matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara.
Hasara:
o Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama hayakutengenezwa vizuri.
2. Matuta ya makingo (sunken seed beds): Faida:
matuta haya ni rahisi kutengeneza
hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
nyevu mdogo unaopatikana ardhini
ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
huzuia mmomonyoka wa ardhi
Hasara:
Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye
mvua nyingi.
Matuta ya kawaida (flat seed beds):
Faida:
ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa
na kusambazwa mbegu huoteshwa
ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu
Hasara:
Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi. Kusia Mbegu
Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test)
Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari
isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha
usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu
kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta.
Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini
zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano.
Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama vile kinyausi (damping
off) au ukungu (blight).
Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa mbegu.
Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini
Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu pamoja na Matunzo Kitaluni
Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo.
Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili
kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi
cha baridi si muhimu sana)
Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo
miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 – 4. Hii itapunguza
magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye
nguvu.
Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani.
Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.
Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani (Transplanting Rules)
Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na udongo.
Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua.
Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa
shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi
iliyostawi vizuri.
Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche
yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa
kupeleka shambani.
Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni.
Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi.
Maandalizi ya Shamba la Nyanya
Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x
(50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha baridi
ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na
kuzuia magonjwa ya fangasi.
Jinsi ya kupanda miche:
Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini.
Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye
udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu
unaosababishwa na mionzi ya jua.
Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani
Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema
Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini.
Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto.
Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye
nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha
mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda
kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.
TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA GREENHOUSETEKNOLOJIA YA KILIMO CHA GREENHOUSE: Kwanza tuanze
kwa kupata tafsiri ya neno lenyewe, Greenhouse imekua ikipatiwa majina
tofauti tofauti, wapo watu wanaiita Nyumba ya Kijani, wengine wanaiita
Banda Kitalu n.k Vyovyote utakavyopenda kuiita teknolojia hii, cha
muhimu ni kuelewa nini hasa maana yake. Greenhouse (Banda Kitalu): ni teknolojia ya
kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea
vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au
nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe
na mazingira haribifu ya hali ya hewa.
Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au
mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na
magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho,
kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo
hayo yaliyotajwa.
Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi baridi, zaidi ya karne
moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi,
mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani
kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la
kuvumbua Greenhouse lilipoibuka.
Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kijani
ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya
ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na
teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini
kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu
wengi. Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna
utofauti kati yake na zile za nchi za ukanda wa baridi
Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kijani
ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya
ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na
teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini
kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu
wengi. Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna
utofauti kati yake na zile za nchi za ukanda wa baridi. GREENHOUSEFaida za Greenhouse
Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi,
ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na
vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya uharibifu wa mazao.
Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
Uwezo wa kupata soko zuri la mazao. Greenhouse itakuwezesha
kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi
hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu, ukiwa na
greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei nzuri
Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti.
Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti wake ni rahisi.
Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone
(drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea pekee.
Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia
ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla
haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa
ajili ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture).
Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama
Nematodes, ndipo uvumbuzi wa teknolojia ya kupanda mimea kwa
kutokutumia udongo ulipotokea
KILIMO NDANI YA GREENHOUSEBaadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha Greenhouse.
Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye
greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri
kupitia teknolojia hii. Tuanze na Marekani, Marekani ina eneo takribani
4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua,
Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni
2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka. Nchini Hispania
inakadiriwa zaidi 25,000hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa
greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe
machanga, pamoja na nyanya.
Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo
hazilimwi kwingine. Mazao maarufu yanayolimwa kwenye Greenhouse za
Canada kama nyanya, matango na hoho.
Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse.
Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi
ndio nchi inayoongoza kwa teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana.
Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi
yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga,
pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower,
Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)
Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua
(cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa nchi ya Israel eneo lake kubwa ni
jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele
katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse.
Balton Tanzania yenye makao yake makuu mjini Arusha, ni moja ya kampuni toka Israel zinazofanya vizuri katika sekta hii.
Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia
teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao ya yanya na
tango yanalimwa kwenye green house.
Misri 10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya
Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote
Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini
mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse. Nchi
nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama Japan (40,000hekta) na
Korea kusini (21,000 hekta). MUUNDO WA GREENHOUSEAina za Greenhouse.
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo: Aina za Greenhouse kwa kigezo cha sura/umbile (shape)
Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu
Quonset Greenhouse
Saw tooth type
Even span type greenhouse
Uneven span type greenhouse
MFANO WA GREENHOUSEAina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi
Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)
Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)
Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)
Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma)
Aina za Greenhouse kwa kigezo cha aina ya zana za ufunikaji (covering types)
Greenhouse zinazofunikwa kwa zana za Vioo (Glass Greenhouse or
Screenhouse) )- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza
joto kwa muda mrefu ndani greenhouse
Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya plaski (plastic film)
KILIMO NDANI YA GREENHOUSEAina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa:
Greenhouse za gharama kubwa (High cost greenhouse) ( Zaidi ya milioni 50)
Greenhouse za gharama za kati (medium cost greenhouse) (milioni 20 hadi 50)
Greenhouse za gharama ndogo (Low cost greenhouse) (chini ya milioni 20)
Greenhouse za gharama ndogo ndio watu wengi wanazitumia sana katika nchi zinazoendelea.
YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI YA MBEGU ZA MPUNGAYAFAHAMU MAKUNDI MAWILI YA MBEGU ZA MPUGA: Je
umekuwa ukijihoji ni vipi utapata mbegu bora za mpunga? Kama jibu ni
ndiyo basi makala haya yanakuhusu sana wewe kwani lengo letu ni kuona
wewe unafanikiwa sana kataika kilimo.
Watu wengi wemekuwa hawafahamu ni mbegu ipi ambayo inafaa katika
upandaji, na kosa hilo ambalo wanalifanya limekuwa likisababisha mazao
nkupatikana kwa uchache zaidi, ila mukweli ni kwamba Matumizi ya mbegu
bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Hivo ili
kuhakikisha unapata mazao mengi Kuna makundi mawili makuu ya mbegu
ambayo ni: 1. Mbegu za asili za mpunga
Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo. Kuna
aina nyingi za mipunga ya asili inayolimwa sehemu mbalimbali hapa nchini
kama Supa, Kahogo, Kula na Bwana, Shingo ya mwali, n.k. Wakulima
wanazipenda mbegu hizi kutokana na kuwa na sifa kama vile ladha nzuri,
uvumilivu wa matatizo mbalimbali ya kimazingira na kwa sababu ya uwezo
wa mbegu hizi kustahimili katika hali mbaya ya hewa na hazihitaji
uangalizi wa hali ya juu.
Sifa hizi ni matokeo ya mbegu hizi kumudu mazingira na uchaguzi wa
mbegu uliofanywa na wakulima kwa miaka mingi. Hata hivyo, nyingi ya
mbegu hizi zina uwezo mdogo wa kuzaa, zinachelewa kukomaa, ni ndefu na
rahisi kuanguka. 2. Mbegu zilizoboreshwa:
Hizi ni zile zilizoboreshwa kutokana na mbegu za asili. Mfano wa mbegu
zilizoboreshwa ni kama vile Katrin, IR54, na IR64. Zinazaa sana hasa kwa
kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, hazikidhi ladha ya walaji na
ukobolekaji wake si mzuri na baadhi hazistahimili kwenye mazingira mengi
ya kawaida. Hii imezifanya mbegu hizi kukubalika na wakulima kwa
kiwango kidogo sana.
Mbegu bora nyingine zilizozalishwa kutoka utafiti na kuonekana
kupendwa kwa ajili ya mavuno mengi na ladha nzuri kama TXD88 na TXD85.
Hivi karibuni imetolewa mbegu nyingine iitwayo TXD306 (SARO5), mbegu hii
hupendwa na wakulima, wafanyabiashara na walaji kutokana na sifa yake
ya mavuno mengi, punje ndefu kiasi na nzito, ladha nzuri na yenye
kunukia pindi ipikwapo na kuliwa.
Hayo ndiyo makundi ya mbegu bora ya mpunga ambayo yatakusaidia kuweza kukua katika kilimo.
UFUGAJI BORA WA NG’OMBEUFUGAJI BORA WA NG’OMBE : Ng’ombe wanafugwa kwa
ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama
ngozi,mbolea na hutumika kama wangyama kazi. Zaidi ya asilimia95 ya
ng,ombe na hutumika kama wanyama kazi. Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe
wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa
kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa. Ng’ombe
walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili, wale wanaofugwa kwa
ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya maziwa. Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa
na ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni
pamoja na:-
Kufuga ng’ombe katika eneo kwa kuzingatia uwianao wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa ufugaji huria.
Kujenga banda au zizi bora.
Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).
Kutunza makundi mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.
Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.
Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifguo.
Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya soko.
Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.
Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.
MIFUMO YA UFUGAJI
Ng’ombe wanaweza kufugwa katika mfumo wa ufugaji huria au kulishwa
katika banda (ufugaji shadidi). Ufugaji huria huhitaji eneo kubwa la
ardhi yenye malisho mazuri na vyanzo vya maji. Pamoja na kuwa na
ufugaji huu, ni muhimu ardhi hiyo itunzwe kwa kuzingatia uwiano wa idadi
ya ng’ombe na malisho. Ufugaji wa shadidi uzingatie uwepo wa banda
bora na lishe sahihi. UFUGAJI KATIKA MFUMO HURIA
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora katika ufugaji huria anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
Atenge eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi ya ng’ombe alionao.
Atunze malisho ili yawe endelevu na yapatikana wakati wote.
Awe na eneo lenye maji ya kutosha na
Atenganishe madume na majike ili kuzuia ng’ombe kuzaa bila mpangilio.
Matunzo mengine ya ng’ombe yazingatie vigezo vingine muhimu kama umri hatua ya uzalishaji na matumizi ya ng’ombe husika. BANDA/ZIZI BORA LA NG’OMBE BANDA BORA.
Band alijengwe sehemu ya mwinuko mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya mvua, upepo, jua kali na baridi.
Kuta imara zenye matunda au madirisha kwa ajili ya kuingiza hewa na mwanga wa kutosha,
Sakafu yenye mwinuko upande mmoja ili isiruhusu maji na uchafu kutuama.
Lijengwe katika hali ya kuruhusu kufanyiwa usafi kwa urahisi kila
siku, na sakafu ngumu ya zege au udongo ulioshindiliwa na kuweka malalo.
Paa lisilovuja na
Aidha kwa wafugaji wanaofuga katika ufugaji huria ambako mazizi hutumika, inashauriwa kuzingatia yafuatayo:-
Zizi likae mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama.
Zizi liweze kukinga mifugo dhidi ya wezi na wanyama hatari.
Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo ng’ombe watengwe kulingana na umri wao.
Zizi lifanyiwe usafi mara kwa mara na
Liwe na sehemu ya kukamulia (kwa ng’ombe wa maziwa), stoo ya
vyakula, sehemu ya kutolea huduma za kinga na tiba, eneo la kulishia na
maji ya kunywa.
ZIZI BORA
Zizi lijengwe sehemu ya mwinuko isiyoruhusu maji kutuama mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-
Liweze kuhakikisha usalama wa ng’ombe.
Ukubwa wa zizi uzingatie idadi ya mifugo.
Liwe na sakafu ya udongo ulioshindiliwa vizuri na kufanyiwa usafi mara kwa mara
Zizi la ndama liwe na paa ma
Lijengwe kwa vifaa madhubuti na visivyoharibu ngozi.
UCHAGUZI WA KOO NA AINA YA NG’OMBE WA KUFUGA
Kwa ufugaji wenye tija, mfugaji anashauriwa kuchagua koo na aina ya ng’ombe kwa kuzingatia malengo ya ufugaji (nyama au maziwa). NG’OMBE WA NYAMA
Ng’ombe wanaofaa kufugwa kwa ajili ya uzalishaji nyama ni wale wanaokua
kwa haraka na kuweka misuli mikubwa iliyojengeka vizuri. Baadhi ya koo
zenye sifa hizo ni pamoja na Boran, Mpwapwa (nyama na maziwa),
Charolais, Aberdeen Angus, pamoja na chotara wao. Hata hivyo, nchini
Tanzania ng’ombe aina ya Zebu (mfano Ufipa,Gofo, Masai, Sukuma, Tarime,
Iringa red), Sanga (Ankole) na chotara wao ndio hutumika kama ng’ombe. NG’OMBE WA MAZIWA.
Sifa za ng’ombe wa maziwa zifuatazo:-
Umbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani.
Mgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani
Miguu ya nyuma mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara.
Kiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu na unene wa wastani
Nafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha na
Endapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa.
Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa kwa wingi nchini ni pamoja na
Friesian, Ayrshire, jersey, Mpwapwa, Simmental na chotara watokanao na
mchangoayiko wa aina hizo na Zebu. UTUNZAJI WA MAKUNDI MABALIMBALI YA NG’OMBE WA MAZIWA KULINGANA NA UMRI NA HATUA YA UZALISHAJI
UTUNZAJI WA NDAMA
Mfugaji anapaswa kutunza ndama vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi
na bora kwa ajili ya maziwa. Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji
wa ndama tangu kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na Kuhakikisha
kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa
kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto (Tincute of Iodine) mara
baada ya kuzaliwa na
Ndama apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrums) mara baada ya
kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Aidha,
aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4.
Endapo jike aliyezaa amekufa au hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa
ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a mbadala, ambayo inaweza
kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo:- Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huohuo.
Lita moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia joto la mwili.
Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver oili).
Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3 na
Yai moja bichi
Koroga mchanganyiko huo, weka katika chupa safi na ndama anyweshwe
kabla haujaopoa. Ndama anyweshwe mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa
muda wa siku 3 mfululizo na kila mara mchanganyiko uwe mpya. Wakati wa
kunywesha chupa iwekwe juu ya kidogo ili asipaliwe.
Endapo ndama hawezi kunyonya ng’o mbe akamuliwe na ndama anyweshwe
maziwa kwa njia ya chupa kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa.
Ndama aendelee kunyweshwa maziwa kwa kiasi kama ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 1
Ndama aanze kuzoeshwa kula nyasi laini, pumba kidogo na maji safi wakti
wote kuanzia wiki ya 2 baada ya kuzaliwa na Ndama aachishwe kunyonya au
kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi 3. Mfugaji ahakikishe kwamba ndama
anayeachishwa kunyonya ana afya nzuri. JEDWALI NA. 1 KIASI CHA MAZIWA NA CHAKULA MAALUMU KWA NDAMA
UMRI (WIKI)
KIASI CHA MAZIWA KWA SIKU (LITA)
KIASI CHA CHAKULA MAALUM CHA NDAMA KWA SIKU (KILO)
1
3.0
0.0
2
3.5
0.0
3
4.0
0.0
4
4.5
0.0
5
5.0
0.1
6
5.0
0.2
7
5.0
0.3
8
4.0
0.4
9
3.0
0.7
10
2.0
1.0
11
1.5
1.25
12 – 16
0.75
1.5
Vyombo vinavyotumika kulishia ndama visafishwe vizuri kwa maji yaliyochemshwa, sabuni na kukaushwa.
Matunzo mengine ya ndani ni pamoja na:-
Kuondoa pembe kati ya siku 3 hadi 14 mara zinapojitokeza ili kuzuia wanyama kuumizana na kuharibu ngozi,
Kukata chuchu za ziada kwa ndama jike
Kuhasi ndama dume wasiozidi umri wa miezi 3 ambao hawatahitajika kwa
ajili kuendeleza kizazi ili wakue hawatajika kwa ajili ya kuendelea
kizazi ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
Kuweka alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya
tano, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio kwa ajili ya urahisi wa
udhiti wa umiliki na utunzaji kumkukumbu na,
Kuwapatia kinga dhidi ya maabukizi na tiba ya magonjwa wanapougua.
Huduma hizi zifanyike chini ya maelekezo ya mtaalam wa mifugo.
UTUNZAJI WA NDAMA BAADA YA KUACHISHWA MAZIWA HADI KUPEVUKA (MIEZI – 18)
Ndama baada ya kuachishwa maziwa apate malisho bora na chakula
mchanganyiko kuanzia kilo 2 4 kwa siku kutegemea umri wake na Ndama
wanapofikia umri wa miezi 18 wachaguliwe wanaofaa kuendeleza kizazi,
wasio na sifa nzuri waondolewe katika kundi.
UTUNZAJI WA MTAMBA
Mtamba ni ng’ombe jike aliyefisha umri wa kupandwa (wastani wa miezi
18) hadi anapozaa kwa mara ya kwanza. Ni muhimu kutunza vizuri mtamba
ili kupata kundi bora la ng’ombe. Miezi 3 kabla ya kupandishwa mtamba
apatiwe:-
Malisho bora
Maji ya kutosha
Madini mchanganyiko na
Chakula cha ziada kiasi cha kilo 2 – 3 kwa siku, ili kuchochea upevukaji na kuongeza uzito wa mwili.
UTUNZAJI WA NG’OMBE WAKUBWA
Kundi hili linajumuisha ng’ombe wenye mimba, wanaokamuliwa na madume.
Mfugaji anapaswa kutunza vizuri ng’ombe wake wakubwa kwa lengo la
kumpatia malisho bora na maji safi ya kutosha kila siku. Mambo muhimu
ya kuzingatia katika utunzaji wa ng’ombe wakubwa ni pamoja na:-
Ng’ombe apatiwe majani makavu (hei) wastani wa kilo 10 au majani
mabichi kilo 40 kwa siku kutegemeana na uzito. Iwapo malisho hayatoshi
hususan wakati wa kiangazi apewe masalia ya mazao (viwandani na
mashambani) kama molasisi, mabua, maharage, mpunga n.k
Ng’ombe apewe vyakula vya ziada (pumba, mashudu, madini
mchanganyiko, unga wa mifupa na chokaa) kulingana na hatua na kiwango
cha uzalishaji na
Ng’ombe apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
UPANDISHAJI
Mfugaji anapaswa kumpandisha ng’ombe kwa umri na wakati muafaka ili
kuepuka matatizo ya uzazi na pia kuhakikisha anapata ndama bora na
maziwa mengi. Mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja na
Mtamba apandishwe akiwa na umri wa miezi 17 -24 na uzito wa kilo 230
– 300 kwa ng’ombe wa kigeni na umri wa miezi 30 – 36 na uzito wa kilo
200 kwa ng’ombe wa asili. (Rejea jedwali Na 2)
Ng’ombe aliyekwisha zaa apandishwe siku 60 baada ya kuzaa na
Siku 18 – 23 baada ya kupandishwa, ng’ombe achunguzwe kama ana
dalili za joto ili apandishwe tena. Iwapo ng’ombe ataendelea kuonyesha
dalili za joto baada ya kupandishwa mara tatu mfugaji apate ushauri wa
mtaalam wa mifugo.
JEDWALI NA.2. UMRI NA UZITO UNAOSHAURIWA KUPANDISHA MTAMBA
AINA YA NG’OMBE
UZITO (KG)
UMRI (MIEZI)
Friesian
240 – 300
18 – 24
Ayrshire
230 – 300
17 – 24
Jersey
200- 250
18 – 20
Mpwapwa
200 – 250
18 – 20
Chotara
230 – 250
18 – 24
Boran
200 – 250
24 – 36
Zebu
200
30 -36
DALILI ZA NG’OMBE ANAYEHITAJI KUPANDWA
Ni muhimu mfugaji akazitambua dalili za ng’ombe anayehitaji kupandwa ili aweze kumpandisha kwa wakati. Dalili hizo ni pamoja na
Kupiga kelele mara kwa mara
Kutotulia/kuhangaika
Kutokwa na ute mweupe usiokatika ukeni
Kupenda kupanda wenzake na husimama akipandwa na wenzake na
Kunusanusa ng’ombe wengine
Ng’ombe akionyesha dalili za joto apandishwe baada ya masaa 12, kwa
kuhimilisha au kwa kutumia dume bora (kwa mfano, akionyesha dalili
asubuhi apandishwe jioni na akionyesha dalili jioni apandishwe asubuhi).
UHIMILISHAJI
Uhimilishaji ni njia ya kupandikiza mbegu kwa ng’ombe jike kwa
kutumia mrija. Faida za uhimilishaji ni pamoja na kusambaza mbegu bora
kwa haraka na kwa gharama nafuu, kupunguza gharama za kutunza dume na
kudhibiti magonjwa ya uzazi.
ILI MFUGAJI ANUFAIKE NA HUDUMA HII ANAPASWA KUFANYA YAFUATAYO:-
Kuchunguza kwa makini ng’ombe mwenye dalili za joto
Kumjulisha mtaalam wa uhimilishaji mapema ili kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa wakati.
Kuchunguza kama ng’ombe atarudi kwenye joto siku ya 18 – 23 baada ya kupandishwa na
Ng’ombe aliyepandishwa apimwe mimba siku 60 hadi 90 baada ya kupandishwa.
MATUNZO YA NG’OMBE MWENYE MIMBA
Ng’ombe mwenye mimba huchukua miezi 9 hadi kuzaa. Katika kipindi
hicho chote anastahili kupatiwa lishe bora na maji ya kutosha ili akidhi
mahitaji ya ndani aliye tumboni na kutoa maziwa mengi baada ya kuzaa.
Mambo ya kuzingatia ni pamoja na
Ng’ombe apewe lishe bora na maji ya kutosha kipindi chote cha mimba
Miezi 2 kabla ya kuzaa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku
Apewe kinga dhidi ya maambukizi na tiba ya magonjwa
Ng’ombe anayekaribia kuzaa, hususani mtamba, azoeshwe kuingia kwenye sehemu ya kukamulia.
DALILI ZA NG’OMBE ANAYEKARIBIA KUZAA
Mfugaji anapaswa kufahamu dalili za ng’ombe anayekaribia kuzaa ili aweze kufanya maandalizi muhimu.
Dalili hizo ni pamoja na Kujitenga kutoka kwa wenzake
Kiwele kuongezeka
Chuchu kutoa maziwa zikikamuliwa
Kutokwa na ute mwekundu na sehemu za uke kuvimba na kulegea
Kuhangaika kulala chini na kusimama na
Kati ya saa moja hadi mbili kabla ya kuzaa sehemu ya uke hutokwa na maji mengi ambayo husaidia kulainisha njia ya ndama kupita.
HUDUMA KWA NG’OMBE ANAYEZAA
Ng’ombe anayezaa anahitaji uangalizi wa karibu ili kuhakikisha
usalama wa ng’ombe na ndama anaezaliwa. Mambo ya kuzingatia ni pamoja
na yafuatayo:-
Sehemu ya kuzalia ng’ombe iandaliwe kwa kuwekwa nyasi kavu na laini na iwe safi.
Ng’ombe ahamishwe sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzaa mara baada ya dalili za kuzaa kuonekana na
Ng’ombe aachwe azae mwenyewe bifa usumbufu
MFUGAJI APATE USHAURI/HUDUMA KUTOKA KWA MTAALAM IWAPO MATATIZO YAFUATAYO YATAJITOKEZA:-
Ng’ombe kushindwa kuzaa kwa masaa mawili hadi matatu baada ya chupa kupasuka
Kondo la nyuma kushindwa kutoka masaa sita baada ya kuzaa
Kizazi kutoka nje na
Ng’ombe kushindwa kusimama baada ya kuzaa
MATUNZO YA NG’OMBE ANAYEKAMULIWA
Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji kupata chakula kwa ajili ya kujikimu
na cha ziada kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa. Ili kukidhi mahitaji ya
uzalishaji wa maziwa ng’ombe
Apewe chakula cha ziada kwa kiwango cha kilo 1 kwa kila lita 2 – 3 za maziwa anayotoa.
Apewe madini na virutubisho vingine kulingan ana mahitaji
Apewe maji mengi kwa vile ni ya muhimu katika kutengeneza maziwa.
Aachwe kukamuliwa siku 60 kabla ya kuzaa. Uachishwaji huu ufanywe
taratibu ili ifikapo siku ya 60 kabla ya kuzaa ukamuaji usitishwe.
Baada ya kusitisha kukamuliwa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku hadi atakapozaa na
Apatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
UZALISHAJI WA MAZIWA
Lengo la ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama pamoja na mazao yatokanayo na maziwa .
Mambo muhimu ya kuzingatia ni:-
Sehemu ya kukkamulia iwe safi na yenye utulivu
Ng’ombe awe na afya nzuri msafi na kiwele kioshwe kwa maji safi ya uvuguvugu.
Mkamuaji awe msafi kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza
Inashauriwa mkamuaji asibadilishwebadilishwe
Vyombo vya kukamulia viwe safi
Muda wa kukamua usibadilishwe na
Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo maalum (strip cup) ili kuchunguza ugonjwa wa kiwele.
UCHAGUZI WA UTUNZAJI WA DUME BORA LA MBEGU
Dume ndilo linalojenga ubora wa kundi la ng’ombe katika masuala ya
uzalishaji kutokana na uwezo wake wa kupanda majike 20 – 25 wakati wa
msimu wa uzalianaji (breeding season).
Ili kundi la ng’ombe liwe bora, mambo yafuatayo yazingatiwe
Chagua dume kutoka kwenye ukoo ulio bora kwa kuzingatia kumbukubu za uzalishaji wa maziwa au nyama za wazazi wake
Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora
Lisha dume malisho bora na maji safi ya kutosha. Pia apatiwe chakula cha ziada.
Katika ufugaji shadidi dume la ng’ombe lifugwe kwenye banda imara lenye sehemu za kuwekea chakula maji na kufanyia mazoezi.
Katika ufugaji huria dume atengewe sehemu na kupatiwa chakula cha ziada.
Dume livalishwe pete puani kwa ajili ya kupunguza ukali na kuwezesha urahisi wa kumshika.
Dume apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingan ana ushauri wa mtaalam wa mifugo na
Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora.
UTUNZAJI WA NG’OMBE WA NYAMA
Ng’ombe wengi wanaofugwa hapa nchini Tanzania ni wa asili ambao kwa
kiwango kikubwa hutumika kwa ajili ya uzalishaji wa nyama. Hata hivyo
uzalishaji wake wa nyama ni mdogo kutokana na kasi ndogo ya kukua na
kuwa na uzito mdogo wakati wanapopevuka. Hali hii husababishwa na
matunzo duni, kwa kuwa huchungwa/hulishwa kwa kutegemea malisho peke
yake ambayo hayawezi kukidhi mahitaji ya viinilishe vinavyohitajika kwa
ng’ombe.
Ili kuongeza kasi ya ukuaji na kuongeza uzalishaji wa nyama, mfugaji anapaswa kufanya mambo yafuatayo:-
UTUNZAJI WA NDAMA
Wajengewe banda/boma imara safi na lisilo na unyevunyevu ili kuepukana na magonjwa kama kichomi na kuhara
Waruhusiwe kunyonya kwa muda usiopungua miezi sita, pia wapatiwe
majani laini kuanzia wanapofikia umri wa wiki mbili ili waanze kula
mapema.
Wapatiwe maji safi na yakutosha
Ndama dume ambao hawatahitajika kwa ajili ya kuendeleza kizazi wahasiwe wakiwa na umri wa wiki mbili ili waanze kula mapema.
Wapatiwe maji safi na yakutosha
Ndama dume ambao hawatahitajika kwa ajili ya kuendeleza kizazi
wahasiwe wakiwa na umri usiozidi miezi 3 ili wakue haraka na kuwa na
nyama nzuri.
Wawekwe alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya
tano kwa ndama wote, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio, kwa ajili
ya urahisi wa udhibiti wa umiliki na utunzaji kumbukumbu.
Ndama wachungwe eneo tofauti na ng’ombe wakubwa kuepuka maambukizi ya minyoo na magonjwa na
UTUNZAJI WA NDAMA BAADA YA KUACHISHWA KUNYONYA HADI KUPEVUKA (MIEZI 6 – 24).
Ndama wa umri huu anatakiwa apatiwe
Malisho bora na maji safi ya kutosha wakati wote
Vyakula vya ziada ili kukidhi mahitaji ya mwili (mifano ya vyakula mchanganyiko imeonyeshwa kwenye jedwali Na. 3 ) na
Tiba na kinga dhidi ya magonjwa hususan kinga ya kutupa mimba (S19) kwa ndama jike watakaotumika kuendeleza kundi.
Katika kipindi cha miezi 6 hadi 24 mfugaji anashauriwa kuchagua ndama
watakaoingizwa katika kundi la wazazi na wanaobaki wawe katika
kunenepesha kwa ajili ya nyama.
UTUNZAJI WA NG’OMBE WA NYAMA
Apatiwe malisho bora na maji safi ya kutosha wakati wote
Vyakula vya ziada (mifano ya vyakula mchanganyiko iliyooneshwa kwenye jedwali Na.3), ili kukidhi mahitaji ya mwili.
Vyakula vya ziada kiasi kisichopungua kilo 2 kila siku miezi 2 kabla ya kuzaa.
Nafasi ya kunyonyesha ndama kwa miezi 6 mfululizo,
Tiba na kinga dhidi ya magonjwa na
Apandishwe kwa kutumia dume bora au kwa kutumia njia ya uhimilishaji siku 60 baada ya kuaa.
UNENEPESHAJI WA NG’OMBE WA NYAMA
Ng’ombe kwa ajili ya nyama anaweza kuchinjwa akiwa na umri wa kuanzia
miezi 3 kulingana na mahitaji ya soko. Kwa kawaida hapa Tanzania
ng’ombe huchinjwa wakiwa na umri wa kuanzia miezi 18 kwa ng’ombe wa
kigeni na zaidi ya miezi 36 kwa ng’ombe wa kigeni na zaidi ya miezi 36
kwa ng’ombe wa asili.
Ili mfugaji aweze kupata faida kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa nyama anapaswa afanye yafuatayo:-
Afuge aina ya ng’ombe wanaokua na kukomaa haraka
Anenepeshe ng’ombe kwa muda wa miezi 3 – 6 kabla ya kuchinjwa. Unenepeshaji huongeza ubora wa nyama na kipato kwa mfugaji.
Awapatie chakula chenye mchanganyiko wenye viinilishe vya kutosha
viinilishe vya kutia nguvu na joto mwilini viwe na uwiano mkubwa kuliko
vingine (Jedwali Na.3), na
Auze ng’ombe mara wanapofikisha umri na uzito unaohitajika katika soko ili kuepuka gharama za ziada.
JEDWALI NA.3. MFANO WA MCHANGANYIKO WA CHAKULA KWA AJILI YA UNENEPESHAJI
AINA YA CHAKULA
KIASI KWA KILO
Majani makavu ya mpunga/NganoHey
23.3
Molasis
44.72
Mahindi yaliyorazwa
18.94
Mashudu ya Alizeti/pamba
11.4
Madini mchanganyiko
0.7
Chumvi
0.47
Urea
0.47
Jumla
100
UZALISHAJI NA UHIFADHI WA MALISHO BORA NA VYAKULA VYA ZIADA
Chakula kikuu cha ng’ombe ni nyasi, vyakula vingine ni pamoja na miti
malisho, mikunde na mabaki ya mazao. Ili kupata malisho misimu yote ya
mwaka ni muhimu kuvuna na kuhifadhi malisho kipindi yanapopatikana kwa
wingi. Inawezekana kupanda malisho mengi kuliko kiasi kinachohitajika
msimu mmoja/wakati wa mvua, kuyavuna yanapofikia hatua ya kutoa maua na
kuyahifadhi (mfano wa malisho yanayoweza kupandwa ni mabingobingo,
Guatemala, African fox-tail, desmodium, centrosema, lukina n.k).
Malisho yakupandwa ni vizuri yawe na mchanganyiko wa jamii ya nyasi,
mikunde na miti malisho.
MASALIA YA MAZAO SHAMBANI
Masalia ya mazao shambani kama vile mabua, magunzi, majani ya
mikunde, viazi, ndizi, mpunga, na mengineyo yanaweza kukusanywa na
kuhifadhiwa vizuri kama chakula cha ng’ombe.
MALISHO YA MITI NA MATUNDA YAKE
Malisho yatokanayo na miti ya malisho na matunda yake yanaweza
kutumika kama malisho ya ng’ombe. Majani na matunda ya miti ya lukina,
sesibania, migunga na mbaazi yanaweza kukaushwa na kuhifadhiwa kwa ajili
ya kulisha ng’ombe.
VYAKULA VYA ZIADA
Ili kukidhi mahitaji ya viinilishwe kulingana na kiwango cha
uzalishaji, ng’ombe anatakiwa kupewa vyakula vya ziada. Vyakula hivyo
vinatokana na mchanganyiko wa vyakula mbalimbali. Michanganyiko hii
inategemeana na upatikanaji wa malighafi katika maeneo husika.
Mifano ya mchanganyiko huo ni kama ifuatavyo:-
EDWALI NA. 4 MFANO WA KWANZA WA CHAKULA CHA ZIADA
AINA YA CHAKULA
KIASI (KILO)
Pumba za mahindi
47
Mahindi yaliyoparazwa
20
Mashudu ya alizeti/pamba
20
Unga wa lukina
10
Chokaa ya mifugo
2
Chumvi
1
Jumla
00
Mfano wa pili wa chakula cha ziada ni tofali la kulamba lenye urea ambalo mchanganyiko wake ni:-
Unga wa mahindi kilo 1
Pumba za mahindi kilo 3
Urea kilo 1
Mashudu ya alizeti kilo 2
Chumvi ya kawaida gramu 200
Unga wa mifupa gramu 200
Chokaa ya mifugo kilo 1.5
saruji kilo 1
mfugaji anatakiwa kuzingatia yafuatayo ili kupata tija katika ufugaji:-
kulisha mchanganyiko wa nyasi, mikunde na mchanganyiko wa madini na vitamin
kutenga maeneo kwa ajili ya kulisha ng’ombe kwa mzunguko pamoja na kupanda malisho katika mfumo huria na nusu huria na
kuvuna nyasi na mikunde inapofikia hatua ya kutoa maua na
kuyahifadhi kwa matumizi wakati wa uhaba wa malisho hususan wakati wa
kiangazi.
NJIA ZA KUHIFADHI MALISHO
Malisho yanaweza kuhifadhiwa kwa kuyakausha (Hei) au kuyavundika (Sileji).
HEI
Hei ni majani yaliyohifadhiwa kwa kukaushwa baada ya kukatwa au
kuachwa kukauka yakiwa shambani kwa matumizi ya baadaye. Katika
kutengeneza hei yafuatayo yazingatiwe:-
vuana malisho yanapoanza kutoa maua
aanikwe kwa siku 3 hadi 6 kutegemea aina ya malisho na hali ya hewa na yageuze mara 1 au 2 kwa siku ili yakauke vizuri.
Yafungwe katika marobota baada ya kukauka inawezekana kutumia kasha
la mbao lenye vipimo vifuatavyo:- Urefu sentimeta 75, upana sentimeta
45 na kina sentimeta 35 au mashine na zana za kufunga marobota ya hei na
Hifadhi marobota juu ya kichanja ili kuzuia maji yasiingie unyevu na kuharibiwa na wadudu.
SILEJI
Sileji ni majani yaliyokatwakatwa na kuvundikwa. Madhumuni ya
kuyavundika ni kuyawezesha kubaki na ubora wake hadi wakati
yatakapotumika katika kutengeneza sileji yafuatayo yazingatiwe:-
Tengeneza sileji kwa kutumia majani yenye sukari nyingi kama mahindi
au mabingobingo na mikunde, mabaki ya viwandani kama molasis,
Andaa shimo au mfuko wa plastiki kulingana na kiasi cha majani yaliyovunwa.
Vuna majani ya kuvundika katika umri wa kuanza kutoa maua. Endapo
majani yaliyovunwa ni teketeke yaachwe kwa siku moja yanyauke kupunguza
kiwango cha maji.
Katakata majani uliyovuna katika vipande vidogovidogo,
Tandaza majani uliyokatakata ndani ya shimo au mfuko katika tabaka nyembamba na kushindilia ili kuondoa hewa yote.
Funika shimo ulilojaza majani kwa plastiki ikifuatiwa na udongo.
Sileji itakuwa tayari kutumika kuanzia siku 21 na
Sileji iliyofunguliwa kwa ajili ya matumizi ifunikwe haraka iwezekanavyo ili kuzuia kuharibika.
Sileji inaweza kubaki na ubora katika shimo kwa muda mrefu kama haitafunguliwa na kuachwa wazi kwa muda mrefu.
UDHIBITI WA MAGONJWA YA NG’OMBE
Magonjwa huweza kusababishwa na matunzo hafifu lishe duni na visababishi vya magonjwa kama vile protozoa bacteria.
Virusi, riketsia na minyoo. Aidha wadudu kama kupe na mbung’o wanasambaza visababishi vya magonjwa.
Afya bora ya ng’ombe inatokana na kuzingatia mambo yafuatayo:-
Ndama apate maziwa ya awali (dang’a) ya kutosha kwa siku 3 – 4 baada ya kuzaliwa ili kuongeza kinga ya magonjwa mwilini.
Chovya kitovu cha ndama ndani ya madini joto (Tincture of Iodine)
mara baada ya kuzaliwa kuzuia kuvimba kitovu kutokauka au kutohudumiwa
ipasavyo mara baada ya ndama kuzaliwa. Kitovu huvimba na kutoa usaha
hukojoakwa shida na wakati mwingine huvimba viungo.
Ndama apewe dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 kama
atakavyoshauri mtaalam wa mifugo. Minyoo huwashambulia ndama zaidi hasa
wale walioana kula majani.
Zingatia usafi wa vyombo na band a epuka kumpa ndama maziwa yaliyopoa na machafu ili kuzuia kuharisha.
Zingatia ujenzi wa mabanda kuruhusu mzunguko wa hewa ili kuzuia
ndama kupata ugonjwa wa vichomi. Vichomi huwapata ndama wa umri wa
miezi 5 au zaidi wanaofugwa ndani katika mabanda machafu yasiyo na
mzunguko wa hewa ya kutosha.
Ogesha ng’ombe kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo ili kuua
kupe wote wanaoleta magonjwa yatokana yo na kupe (ndigana kali na
baridi, kukojoa damu na maji moyo) na mbung’o (ndorobo) na
Ng’ombe wapatiwe chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali chanjo muhimu
ni za ugonjwa wa kutupa mimba, kimeta, ugonjwa wa miguu na midomo na
chambavu.
Mfugaji anashauriwa kutoa taarifa kwa mtaalam wa mifugo anapoona ng’ombe wake ana baadhi ya dalili zifuatazo:-
Joto kali la mwili na manyonya kusimama
Amepunguza hamu ya kula
Amezubaa na kutoa machozi
Anasimama kwa shind ana kusinzia
Anapumua kwa shida na pua kukauka
Anatokwa na kamasi nyingi
Anajitenga na kundi
Anaconda na
Anapunguza utoaji wa maziwa ghafla
KUMBUKUMBU NA TAKWIMU MUHIMU
Kumbukumbu ni taarifa au maelezo sahihi yaliyoandikwa kuhusu matukio
muhimu ya kila ng’ombe na shughuli zote zinazohusiana na ufugaji.
Mfugaji anashauriwa kuweka kumbukumbu na takwimu muhimu katika shughuli
zake za ufugaji wa ng’ombe. Kumbukumbu zinamsaidia mfugaji kujua
mapato na matumizi na kufanya maamuzi sahihi kuhusu mifugo husika na
mifugo husika na mazao yake. Aidha humwezesha kuweka mipango ya
shughuli zake.
Mfugaji anapaswa kuweka kumbukumbu muhimu zifuatazo:-
Uzazi (uhimilishaji na matumizi ya dume, tarehe ya kupandwa, kuzaa kuachisha kunyonya)