KILIMO BORA CHA PILIPILI MANGA: Pilipili mtama au
kwa jina lingine pilipili manga ni kiungo muhimu sana katika mapishi.
Radha yake ya muwasho ndio kitu hasa kinachotafutwa katika vipunje
vidogo vidogo vya zao hili. Pilipili manga husagwa ili kupata ungaunga
kabla ya kutumika ingawa pia inaweza kutumika bila kusagwa.
Jina la kitalaam ni Piper nigram na kwa kiingereza ni black pepper. Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar. Ingawa pia inaweza kukubali katika maeneo ya Kagera
Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki na kwa mapishi mengine mbalimbali. Nchi za magharibi zina matumizi makubwa ya viungo hivi. Aidha pilipili mtama nyeusi ndiyo huzalishwa zaidi hapa nchini.
Namna ya uzalishaji wa pilipili manga.
Kupogolea miche ya pilipili mtama
Mche ukifikia miezi 18 inapaswa kupogolea kwa kukata sehemu ya juu ya mche ili kufanya matawi mengine yachipue chini ya mche. Inashauriwa mche kuwa na urefu wa mita 3-3.5.
Uvunaji
Maua ya kwanza hutoka baada ya miaka miwili. Matunda hukomaa miezi tisa (9) hadi kumi (10). Uvunaji ni mizunguko 5 hadi 6 kwa mwaka. Pilipili mtama inaweza kuvunwa kwa misimu miwili. Mavuno ni kati ya tani 0.35 – 3.75 kwa hekta. Wakati wa uvunaji kishina cha matunda ya kijani hukatwa kutoka kwenye mti kisha mbegu za huchambuliwa kutoka kwenye vishina na kisha huanikwa juani kwa siku 3 hadi 4 ili kuhakikisha zinakauka vizuri kabisa. Kiasi cha unyevu kiwe angalau 13 – 14%.
Kuhifadhi
Pilipili mtama iliyokaushwa vizuri inaweza ikawekwa kwenye chombo kisichopitisha hewa na kudumu kwa miaka hadi 20 bila kuharibika.
Masoko ya pipili mtama
Soko la pilipili matama linapatikana ndani ya nchi na nje pia. Bei ya ndani ni kati ya Sh1,000-1,500. Zao hili huuzwa katika nchi za Uganda, Kenya, Uingereza, Ujerumani, Mashariki ya Kati, n.k. Bei ya Nje ni wastani wa dola za kimarekani 1,985 kwa tani. (Tafadhali fanyia utafiti soko, data hizi ni za siku nyingi)

- Hali ya hewa na udongo
- Uchaguzi wa mbegu
- a) Urefu wa pingili na ukubwa wa majani
- b) Ufupi wa pingili unaoambatana na majani madogo.
- Nafasi ya upandaji
- Mahitaji ya mbolea
- Miti ya kusimikia miche
Kupogolea miche ya pilipili mtama
Mche ukifikia miezi 18 inapaswa kupogolea kwa kukata sehemu ya juu ya mche ili kufanya matawi mengine yachipue chini ya mche. Inashauriwa mche kuwa na urefu wa mita 3-3.5.
Uvunaji
Maua ya kwanza hutoka baada ya miaka miwili. Matunda hukomaa miezi tisa (9) hadi kumi (10). Uvunaji ni mizunguko 5 hadi 6 kwa mwaka. Pilipili mtama inaweza kuvunwa kwa misimu miwili. Mavuno ni kati ya tani 0.35 – 3.75 kwa hekta. Wakati wa uvunaji kishina cha matunda ya kijani hukatwa kutoka kwenye mti kisha mbegu za huchambuliwa kutoka kwenye vishina na kisha huanikwa juani kwa siku 3 hadi 4 ili kuhakikisha zinakauka vizuri kabisa. Kiasi cha unyevu kiwe angalau 13 – 14%.
Kuhifadhi
Pilipili mtama iliyokaushwa vizuri inaweza ikawekwa kwenye chombo kisichopitisha hewa na kudumu kwa miaka hadi 20 bila kuharibika.
Masoko ya pipili mtama
Soko la pilipili matama linapatikana ndani ya nchi na nje pia. Bei ya ndani ni kati ya Sh1,000-1,500. Zao hili huuzwa katika nchi za Uganda, Kenya, Uingereza, Ujerumani, Mashariki ya Kati, n.k. Bei ya Nje ni wastani wa dola za kimarekani 1,985 kwa tani. (Tafadhali fanyia utafiti soko, data hizi ni za siku nyingi)
Samahani nitafute kwa no 0620112019
ReplyDeleteNakupigia haupatikani samahani
DeleteNamba zangu ni 0675607273