KILIMO BORA CHA MAKAKARA (PASSION FRUITS) : Ni mimea inyotambaa na
kuhimili hali nyingi za hewa (sio ukame). Mmea huu hustawi zaidi ukanda
usio na baridi wastani wa 20c – 30c na kiasi cha mvua 1500mm za ujazo
kwa Mwaka, tunda huwa na ukubwa wa sentimeta 10 kwa kipenyo na uzito
gramu 90.
kuna aina kadhaa za matunda haya lakini yale ya kijani/manjano
hustawi zaidi ukanda wa pwani na yale yenye wekundu fulani hustawi zaidi
maeneo ya misitu, hupendelea udongo wa kichanga wenye mbolea na
usiotuamisha maji, pia udongo usiwe na chumvi nyingi na pia kusiwe na
mwamba chini kasi cha mita moja tu.
Upandaji.
Mbegu zipandwe kwanza kwenye mifuko ya plastiki yenye udongo wenye
rutuba ya kutosha , kiasi cha Mbegu 3 kwa kila mfuko na mara zinapoota
mimea ikingwe na jua kali na ikifikia urefu wa sentimeta 30, huweza
kuhamishiwa shambani
Kwenye shamba lako hakikisha kuna nguzo zenye waya mmoja kwa ajili ya
mimea kutambaa juu yake, sehemu ya juu baada ya nguzo kuzikwa chini
ibakie kama mita mbili na kati ya msatari na mstari iwe ni mita 2
(ukanda wa pwani ) na mita 3 ukanda wa juu kiasi, na umbali kati ya
nguzo na nguzo kwenye mstari ni mita 6, na mimea ipandwe umbali wa mita 3
kati ya nguzo na nguzo kufuata mstari.
Mbolea
Mbolea za viwandani ziwekwe kutokana na hali ya udongo, muone afisa
ugani kilimo ili afanye vipimo kujua mahitaji na upungufu wa udongo,
Magonjwa na madudu.
Wadudu kama chawa wa mimea na mchwa wekundu ndio adui wa makakara,
pia fangasi husshambulia sana maua ya makakara. Dawa za jamii ya kopa
zitumike mara dalili za magonjwa au wadudu kuonekana, kiasi cha kilo 2.8
– 3 hutosha kwa hekta moja au gramu 225 kwa ajili ya dumu moja la lita
20
Magugu.
Makakara yanatakiwa yawe kwenye shamba safi lisilo na majani na
magugu, jembe la Mkono au madawa kama ROUND-UP na GRAMOXONE ynaweza
kutumika mimea ikishaefuka na kuwa juu kwenye waya
Kufundisha matawi ya mimea.
Ni lazima kuyafundisha matawi mawili ya kwanza kwa kuyaelekeza
kutambaa kwenye waya kila moja likielekea upande wake na matawi
yatakayoota kutokana na matawi makuu nayo yaelekezwe juu kwenye waya
yakifikia ukubwa wa sentimeta 30 – 40.
Kupunguza matawi.
Silazima kupunguza matawi kwa sababu mmea mkubwa zaidi ndio hutoa
matunda mengi zaidi, labda kama kuna matatizo katika uchumaji ndio
unaweza kupunguza baadhi ya matawi kiasi.
Uvunaji.
Uvunaji huanza baada ya miezi 8 – 9 baada yam mea kupandwa na matunda
hukusanywa baada ya kudondoka yenyewe chini baada ya kuiva kila baada
ya wiki moja, matunda yahifadhiwe sehemu kavu na isiyo na joto , kiasi
cha tani 5 – 10 huweza kupatikana katika hakta moja kwa msimu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Fahamu mbinu za kuongeza thamani nyama
Safari ya kuongeza thamani nyama ya mifugo huanzia shambani kwa usimamizi wa ufugaji na uzalishaji. Lishe bora ni muhimu kwa wa ufugaji ...
-
Mpenzi msomaji wa blog hii leo napenda nikuletee kitu kingine tofauti kidogo na ambacho blog nyingi za kilimo, ntapenda kukuletea...
-
Karoti ni Nini? Karoti kwa jina la kisayansi inajulikana kama Daucus carota . Ni miongoni mwa mazao kadhaa ya bustani (mbogamboga) yenye ...
hongerakwa kazi nzuri
ReplyDeleteAhsante kwa kazi nzuri
ReplyDeleteHongereni hayo ndo tunayataka siyo kukaa vijiweni kisha unalalamika hali ngumu
ReplyDelete