![UFAGAJI BORA WA KUKU AINA YA KULOIREL](https://i2.wp.com/farmersmarket.co.tz/wp-content/uploads/2017/09/kuroiler-poultry-farming.jpg?resize=600%2C420)
kuku hawa ni moja kati ya mbegu ambayo inafanya vizuri sana katika nchi nyingi.
SIFA ZA KULOIREL
- Ni aina ya kuku ambao hutumika kwa matumizi ya ani nyama pamoja na mayai
- Kuku mmoja anauwezo wa kutaga mayai 150 hamsini kwa mwaka ukilinganisha na kuku wengine hutoa 40- 50 kwa mwaka.
- Madume ya kuloirel hua yana kilo 3.5 na jike ni kilo 2.5 ukilinganisha na kuku wengine dume hua na kilo 2.5 na jike ni kilo 1.5.
- Pia ni moja kati ya aina ambayo haipati magonjwa kirahisi (disease resistance)
- Kuku hawa hawana gharama sana katika kuwalisha kwa sababu wanauwezo pia wa kula chakula kama kuku wa kienyeji.
BANDA
Kama walivyo kuku wengine banda lazima liwe bora ili kuweza kupata kuku bora pamoja na mayai mengi, ila pia kuku wa aina ya kuroiler sio lazima uwafungie ndani moja kwa moja unaweza kutengeneza sehemu ambayo utawafungulia ili kuweza kujipatia chakulatofauti na kuku wa kisasa.
Lakini pia ni vyema kila wakati ukazingatia usafi ni muhimu hivyo ni vyema kuzingatia hilo
CHAKULA
Chakula ni lazima kiwe bora ili kupata kuku bora pamoja na mayai ya kutosha.
- Kuku jike mmoja anakadiliwa kula kilo 5-8 kabla ya kuanza kutaga.
- muhimu sana kwa mfugaji kujifunza jinsi ya kuchanganya chakula mwenyewe.
- kuanzia siku 1 hadi wiki 4 unatakiwa kuwapa chakula cha kuanzia (chick starter mash)
- kuanzia wiki ya 4 hadi 8 unawapa chakula cha kukuzia (chick grower mash)
- Kuanzia wiki ya kwanza kuanza kutaga hadi mwisho unatakiwa kuwapa chakula(layersmash)
- Lakini pia inakadiliwa kua na drinker 15 na vyombo vya kulia chakula, wastani wa kuku 1000.
Naomba kufahamu wanapatikana vipi Kuku Aina ya kuroiler
ReplyDeleteNipo Tanzania mkoani pwani wilaya ya kibaha, naweza kuwapata wapi Kuku Aina ya kuroiler.
ReplyDeleteHabari yako zoologist,
DeleteLeo shida yako imemalizika.
Karibu Abuychicken ujipatie vifaranga vya kuroiler kwa bei nafuu kabisa , tunapatikana Tanzania mkoa wa pwani wilaya ya kibaha maeneo ya miembe saba B", kuwahi kwako kutoa oder ndyo kuwahi kwako kupata vifaranga.
Wasiliana nasi kupitia no.0657116963