
Kuku hupunguza utagaji na hata kuacha kutaga kabisa iwapo:-
- Hawakupewa chakula bora au cha kutosha.
- Hawapewi maji safi ya kutosha.
- Wamebanana, yaani hawakai kwa raha.
- Vyombo vya maji au chakula havitoshi.
- Mwanga hautoshi.
- Majogoo yamezidi katika chumba(weka jogoo 1 kwa mitetea 10)
- Kuku wanaumwa.
- Wana vidusa vya nje na ndani (external and internal parasite).
- Wamezeeka (umri zaidi ya miaka miwili na nusu).
No comments:
Post a Comment