Kilimo cha Kisasa cha Mahindi
Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzoni mwa mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to 15th day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti mwanzoni....
KUANDAA SHAMBA, KUPANDA NA KUPALILIA
Kuandaa Shamba, Kusafisha, Kulima/Kutifua
Ni vyema mashamba yaandaliwe mapema kabla ya msimu wa kupanda haujaanza
ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati unaotakiwa. Kuna njia
mbalimbali zinazotumika kuandaa mashamba. Kati ya njia hizi ni pamoja na
kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
- Jembe la mkono - wengi wanatumia
- Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
- Power tillers
- Matrekta
Matumizi ya trekta, power tillers na jembe la kukokotwa na wanyama
yanapunguza nguvu kazi kwani vinachimbua udongo na kuufanya kuwa
tifutifu (kufanya isiwe na mabonge makubwa, wala isiwe vumbi vumbi). Hii
husaidia:
- Mizizi ya mimea kupenyeza ardhini kirahisi
- Udongo kuweza kuhifadhi maji
- Udongo kuwa na hewa inayohitajika na mimea
- Ukuaji mzuri wa mimea hivyo kuongeza mavuno
Mbegu Bora za mahindi
Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:
- Mbegu za asili: Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo
- Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile zilizoboreshwa kutoka mbegu za asili. Kundi hili linagawanywa kwenye makundi mawili - composite varieties na mbegu chotara (Hybrids).
Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa sababu ya:
- Mwinuko kutoka usawa wa bahari
- Kiasi cha mvua katika eneo husika
- Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa
Mbegu za mahindi zilizoboreshwa ni kama TMV1, TAN 250, TAN 254, Staha,
Situka na zingine zote zinazoanza na herufi “H” kama vile H 250, H 251
na H 615. Pia mbegu mpya zilizotangawa na Kamati ya Taifa ya Mbegu mwaka
huu ni WE4102, WE4106, WE4110, WE4114, WE4115 kutoka ARI ILONGA.
Jinsi Ya Kuweka Mbolea Za Kupandia
Mbolea hizi zinawekwa shambani kabla ya kupanda/kusia mbegu. Zinawekwa
kwa njia mbalimbali kama vile kusambaza kwenye eneo husika na
kuchanganya na udongo, au kuweka kwenye mistari au mashimo ya kupandia.
Ni bora zaidi kuchanganya mbolea za Minjigu Phosphate au Minjingu Mazao
na udongo kuliko kutia kwenye shimo la kupandia. Pia kuchanganya mbolea
na udongo huondoa athari za mbolea kwenye uotaji wa mbegu, hasa kama
kuna uhaba wa unyevunyevu.
Viwango Vya Mbolea Za Kupandia mahindi
Kiwango cha mbolea za kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 fosfati (P)
kwa hektari ambayo ni sawasawa na kiasi cha mifuko 2 ya DAP (= mfuko
mmoja kwa ekari). Ikiwa mbolea ya minjingu phosphate itatumika basi
mifuko mitatu itatosa kwa hekta (= mfuko mmoja na nusu kwa ekari). Na
endapo utaamua kuitumia mbolea ya minjingu mazao basi tumia mifuko minne
na nusu kwenye hekta moja au mifuko miwili kwa ekari moja.
Upandaji wa mahindi
Muda wa kupanda: Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzonimwa
mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to
15th day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili
mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi
wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai
katikati na Agosti mwanzoni. Katika msimu huu utayarishaji wa shamba
hufanyika mwezi wa pili mwanzoni.
Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana
na majira ya mvua. Kwa mfano katika wilaya ya Morogoro tarehe za kupanda
ni kuanzia februari 15 hadi Machi 15. Mkulima anashauriwa afuate
kalenda ya muda wa kupanda kama anavyoshauriwa na bwana shamba wake.
Nafasi ya kupandia mahindi
Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za kilimo inayomwezesha mkulima
kupata mazao bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupanda kwa mistari
na kufuata nafasi zinazoshauriwa na wataalamu wa kilimo. Zifuatazo ni
nafasi za kupanda mahindi na idadi ya mbegu kwa kila shimo na kiasi cha
mbolea (kwa vizibo vya soda) inayotakiwa kuwekwa kwa shimo:
- Kwa nafasi ya 90 sm X 30 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea
- Kwa nafasi ya 90 sm X 25 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea
- Kwa nafasi ya 90 sm X 50 sm, panda mbegu mbili na uweke vizibo viwili vya mbolea
Kupalilia
Ni muhimu shamba lipaliliwe baada ya mimea kuota ili kuondoa magugu.
Magugu ni mimea hivyo hushindana na mimea iliyopandwa na mkulima kwa
kunyonya virutubisho ardhini. Magugu yanaweza pia kuhifadhi wadudu na
magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo kupunguza
mavuno. Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono (yaani) kung’olea
(ikiwa magugu yapo mbali mbali sana) au kulima kwa jembe la mkono au kwa
kutumia dawa/viuagugu (HERBCIDES) hasa 2-4D.
Mbolea za kukuzia mahindi
Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea
ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha
naitrojeni. zifuatazo ni mbolea za kukuzia na kiwango chake cha
naitrojeni:
- UREA: 46% N
- Calcium Ammonium Nitrate, CAN: 23% N
- Sulphate of Ammonia, SA: 21%
Urea inakirutubisho cha naitrojeni (N) kwa kiwango kikubwa na watu wengi
wanauzoefu nayo. Vilevile bei yake ni nafuu ikilinganishwa na mbolea
zingine za kukuzia. Mbolea hii iko katika hali ya chengachenga za
mviringo (granules) za rangi nyeupe. Kiwango cha urea ni nusu kizibo cha
soda kwa kila shina. Mbolea hizi hazidumu kwenye udongo kwa muda mrefu
kwa hiyo huwekwa shambani wakati mimea inapokuwa na mahitaji makubwa ya
kirutubisho cha naitrojeni na wakati udongo una unyevunyevu na shamba
halina magugu.
Pia wakulima hutumia mbolea za kukuzia zinazopatikana kwa bei nafuu kama
vile BOOSTER (foliage nitrogeneous fertilizers) ambayo hupigwa kwa
kunyunyizia katika majani ya mmea kila baada ya wiki 3, kwa mara 2-3
mpaka mahindi kuvunwa. Kiwango cha kupiga ni mchanganyo wa mls 50-80 ktk
lita 15 za maji. Mbolea za kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la
mimea au pande mbili au tatu au nne za kila shina. Cha muhimu ni kwamba
mbolea isirundikwe sehemu mmoja. Minjingu Mazao (kg 50/ekari = gramu
10kwa shimo) pia yaweza tumika kwa kukuzia, hivyo mkulima yko huru
kuchagua kulingana na uwezo na upatikanaji wake.
Viwango Vya Mbolea Za Kukuzia Vinavyoshauriwa
Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni
sawasawa na kiasi cha mifuko miwili ikiwa utatumia UREA. Hata hivyo
mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa.
Hivyo basi utumie mifuko mitatu kwa hekta ambayo ni sawa na mfuko mmoja
kwa ekari. CAN inaweza kutumika kama kuna mahitaji maalum ya nitrate na
ammonium na endapo utaitumia basi mifuko minne na nusu itatosha kwa
hekta, ambapo kwa ekari moja utatumia mifuko miwili tu.
Kwenye mahindi mbolea ya kukuzia inawekwa baada ya palizi ya kwanza
ambayo ni kama wiki tatu mpaka wiki nne baada ya kupanda. Kwa kila mmea
mmoja weka kiasi hiki cha mbolea:
- UREA: kizibo kimoja cha soda
- CAN: vizibo viwili vya soda, na
- SA: kizibo kimoja cha soda
Mambo Muhimu Ya Kuzingatia
Kuweka mbolea: Sehemu za nchi ambazo muda wa kukua mahindi ni
mrefu (zaidi ya miezi mitatu), ni vyema kuweka mbolea za kukuzia mara
mbili, yaani nusu ya kiwango kinachopendekezwa baada ya mwezi mmoja, na
kurudia tena (kutumia nusu iliyosalia) baada ya wiki tatu.
Kupalilia: Katika kilimo cha mahindi, ni muhimu shamba lipaliliwe
siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati
wa kupanda. Wataalamu wanashauri kwamba katika kilimo cha mahindi,
shamba lipaliliwe mara 2-3, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.
- Utafiti unaonyesha kwamba, shamba la mahindi ambalo halijapaliliwa
linaweza kupunguza mavuno kwa asilimia 60 hadi 100 ya mavuno
yanayotarajiwa. Hata kama mkulima atatumia mbegu bora, aina na kiasi cha
mbolea zinazoshauriwa, kupanda kwa mstari pamoja na mbinu nyingine bora
zinazoshauriwa, bila kupalilia hali hii itaathiri mavuno yake.
KUDHIBITI MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA MAHINDI
Magonjwa Yanayoshambulia Mahindi
i) Maize streak virus
Dawa/Kudhibiti: Mbegu bora inayostahimili ugonjwa, kupanda mapema,
kung’oa mimea iliyoathirika ama kunyunyiza dawa za kuua ‘vectors’ kama
vile inzi weupe (white flies).
Maize streak virus |
ii) Smut (Fugwe)
Dawa/Kudhibiti: Tumia Helerat ukifuata maagizo kamili.
Ugonjwa wa fungwe kwenye mahindi |
iii) Cob rot (kuoza kwa mhindi)
Dawa/Kudhibiti: Tumia mbegu zinazostahimili kuoza.
Muhindi uliooza |
Wadudu Na Wanyama Wanaoshambulia Mahindi
a) Viwavi Jeshi
Ni wadudu aina ya funza ambao hutokana na Nondo.Hushambulia mahindi kwa
kula majaniyake pamoja na shina. Wadudu hawa huangamizwa/kudhibitiwa kwa
njia zifuatazo;-
- Kuondoa vichaka karibu na shamba
- Kunyunyizia sumu za asili kama vile Mwarobaini majuma mawili ya mwanzo.
- Kunyunyizia sumu za viwandani endapo wadudu wameanza kuonekana kama vile Karate 1ml/1L
Viwavi jeshi |
b) Funza wa Mabua (Maize Stalk Borer)
Funza wa mabua hutoboa shina la mahindi na kusababisha kudumaa kwa mahindi.
- Matundu, ungaunga kama wa msumeno huonekana kwenye majani yaliyoathiriwa.
- Mashambulizi huanza juma la pili hadi la tatu baada ya mahindi kuota.
- Njia za kudhibiti zinazotumika
- Kuchanganya mahindi na mazao jamii ya mikunde km vile maharagwe
- Kung’oa mahindi yaliyoshambuliwa
- Sumu za asili mwarobaini
- Sumu za viwandani km vile Karate. pia waweza tumia Malathion, sumithion, vumbi ya cymbush au Sevin 5G na ufuate maagizo kamili.
Funza wa mabua |
c) Cutworms (Vikata Shina)
Dawa/Kudhibiti: Tumia Dragnet FT na ufuate maagizo kamili.
d) Wanyama waharibifu
Kudhibiti: Kuwatishia na kuwafukuza wanyama.
Ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora inashauriwa kutumia dawa za
kuzuia magonjwa na wadudu washambuliao mimea na njia zinginezo.
Nyani |
KUVUNA, KUKAUSHA, KUSAFISHA NA KUHIFADIHI
Kuvuna
Mahindi
yako tayari kuvuna wakati kikonyo kimekuwa dhaifu na mahindi yanaangalia
chini. Mahindi yakishakauka vizuri yanatenganishwa na bua halafu majani
ya mhindi kutolewa.
Kukausha
Kama
mahindi hayajakauka vizuri hukaushwa zaidi katika juani siku 3-4 ili
kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni
muhimu mahindi yakauke vizuri ili yasioze yakiwekwa ghalani. Ili
kujua kama mahindi yamekauka vizuri, tia mahindi kadhaa kwenye chupa ya
soda iliyokauka na uongeze kiganja kimoja cha chumvi. Tingisha chupa
halafu uwache itulie kwa dakika tatu. Chumvi ikikwama kando ya chupa,
basi mahindi hayajakauka vizuri.
Kusafisha
Mahindi yaliyokauka vizuri hupepetwa na vilevile mahindi mabovu huondolewa.
Kuhifadhi
Mahindi
huhifadhiwa ghalani baada ya kuwekwa viatilifu vya kuzuia bungua wa
mahindi Njia za kisasa za uhifadhi hutumiwa kama vile matumiz ya
ACTELLIC SUPER DUST katika uwiano wa 1kg kwa gunia 5-10 za ujazo wa
100kg. Kiatilifu kingine ni actellic solution katika rate ya 5mls katika
gunia moja la kg 100. Njia
nyingine ya kienyeji katika kuhifadhi mahindi ni kuweka juu ya ghala
ambalo chini yake kuna jiko la kupikia ambalo hutoa moshi unaotumika
kufukuza na kuua wadudu.
Pia waweza kufahamu:
Tafadhali weka comment yako hapa chini ili kubadilishana uzoefu na wakulima wengine.
Comments
Post a Comment