JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA KUKU
JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA KUKU : Somo hili ni mahususi kwa ajili
ya wafugaji wote wa kuku, au kwa wale wote ambao wanapenda kufuga kuku.
Kwani mfumo huu ni mzuri na humsaidia mfugaji kuweza kutengeza chakula
ambacho kina virubishio vyote ambavyo ni muhimu kwa kuku.
JINSI KUANDAA CHAKULA CHA KUKU KUANZIA WIKI LA 1- HADI WIKI LA 8. Mahitaji.
Pumba 60kg
Mahind ya kuparaza 10kg
Mashudu alizeti 10kg
Dagaaa 15kg
unga wa mifupa 5kg
Chumvi ½
premix ¼
Mara baada ya kuanda mahitaji hayo changanya vyote ili kupata mchnganyiko wa chakula.
CHAKULA CHA KUKU, KUANZIA WIKI LA NANE NA KUENDELEA. Mahitaji
Pumba ya mahindi yenye chenga- kg 38
Mashudu ya alizeti- kg 7.5
Mabaki ya dagaa – kg 1.5
Chokaa ya kuku – kg 0. 5
Unga wa mifupa – kg 0.5
Lusina – kg 2
Chumvi – kg 0.25
Mara baada ya kuanda mahitaji hayo changanya vyote ili kupata mchnganyiko wa chakula.
No comments:
Post a Comment