WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa pamba kutochanganya pamba na mchanga au maji kwa sababu watakosa wanunuzi.
Pia
amesema Serikali itapambana na watu wote wanaotaka kuvuruga zao hilo,
hivyo amewataka wakulima waendelee kuwa na imani na Serikali yao.
Waziri
mkuu alitoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Februari 16, 2018) wakati
akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Kwimba.
“Wakulima
msichezee pamba kwa kuichanganya na chochote ili kuiongezea uzito kwa
sababu mtaharibu sifa nzuri ya pamba ya Tanzania ndani nan je ya nchi.”
Alisema
kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakulima wasiokuwa waaminifu ambao kabla
ya kuipeleka pamba sokoni wanachanganya na maji au mchanga.
Waziri
Mkuu alisema Serikali imeanza kuona tija tangu ilipoagiza Maofisa
Kilimo katika mikoa inayolima pamba wasimamie kilimo hicho kuanzia ngazi
za awali.
Akizungumzia
kuhusu suala la wanunuzi wa pamba, Waziri Mkuu alisema tayari Serikali
imeweka mikakati ya kutosha itakayowezesha pamba yote kununuliwa.
Kuhusu
suala la bei alisema wataangalia katika soko la Dunia na kisha
watawashawishi wanunuzi wanunue kwa bei nzuri itakayowanufaisha
wakulima.
Alisema
Serikali itaendelea kusimamia zao hilo kuanzia hatua za maandalizi ya
shamba kwa kulima kitaalam, upatikanaji wa pembejeo hadi masoko.
Awali,
Waziri Mkuu alitembelea mashamba ya mfano ya pamba katika kijiji cha
Kilyaboya na Igumangobo ambapo alisema ameridhishwa mashamba hayo.
Pia
aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kadashi,
mradi ambao ulioibuliwa na Diwani wa Kata ya Maligisu, Bw. Tabu Mapembe.
Kata
ya Maligisu yenye vijiji vine ina zahanati moja tu, kukamilika kwa
ujenzi wa zahanati hiyo kutasaidia kupunguza tatizo la utoaji wa huduma
za afya.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, FEBRUARI 17, 2018.
No comments:
Post a Comment