Washindi wa shindano la ubunifu wa kiteknolojia katika picha ya pamoja na mgeni rasmi baada ya kukabidhiwa zawadi zao
**
Wataalamu
mbalimbali walioudhuria kongamano la The East Africa (EA) Innovation
Event la kampuni mama ya TBL Group ya ABInBev lenye lengo la kuleta
mapinduzi ya kilimo kupitia sayansi na teknolojia lililoandaliwa na
taasisi ya Bits&Bites Technology Convention na kufanyika jijini Dar
es Salaam, wamedhihirisha kuwa mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo
nchini na barani Afrika kwa ujumla yanawezekana kupitia matumizi ya
teknolojia za kisayansi.
Kongamano
hilo ambalo lilijumuisha wataalamu wa fani ya kilimo,watafiti,wahandisi
na wabunifu kutoka kanda ya Afrika Mashariki walijadili jinsi ya kupata
ufumbuzi wa kuinua kilimo cha wakulima wadogo kupitia teknolojia za
kisasa na za gharama nafuu ambapo pia walishiriki shindano la ubunifu wa
nyenzo za kiteknolojia ambapo walipata fursa ya kuwasilisha kazi zao
walizogundua.
Makampuni
ya Imara Tech,Mobisol na Back Save Equipment yaliibuka na ushindi baada
ya jopo la majaji waliokuwa wanasimamia shindano hilo kubainisha kuwa
ugunduzi wao wa nyenzo za kiteknolojia unaweza kusaidia kuinua maisha ya
wakulima wadogo.Kazi zilizowapatia ushindi washiriki zitaanza kufanyiwa
majaribio kabla ya mchakato wa kuzifikisha kwa walengwa ambao ni
wakulima hususani wadogo wadogo.
Akiongea
wakati wa kufunga kongamano hilo, Mkurugenzi wa taasisi ya Tanzania
Private Sector Foundation (TPSF), Godfrey Sembeye, alisema kuwa
kongamano hili limefanyika kwa wakati mwafaka ambapo Tanzania inajipanga
kuingia katika uchumi wa viwanda ambao unaenda sambamba na kufanya
mapinduzi ya kilimo kwa ajili ya kupata malighafi ya viwanda
vitakavyoanzishwa,pia kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha.
Sembeye,
alisema njia pekee ya kuleta mapinduzi ya kilimo ni kupitia matumizi ya
teknolojia ya kisasa na za gharama nafuu ambazo wakulima wengi wa hali
ya chini wanaweza kumudu kuzinunua na kuzitumia kwa ajili ya kuwawezesha
kupata tija na ufanisi katika kazi zao.
“Kutokana
na taarifa za tafiti mbalimbali imebainishwa kuwa bara la Africa lina
hekari 600 milioni ambazo hazitumiki ambazo zikitumika ipasavyo zitaweza
kuzalisha chakula cha kulisha watu wapatao bilioni 9 hadi kufikia mwaka
2050 na ardhi hii haitanufaisha bara la Afrika tu bali dunia nzima,
sekta ya kilimo inaonekana kuwa na fursa kubwa, kinachotakiwa ni
kujipanga kuhakikisha inaenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolia
yanayobadilika kila siku”,alisema Sembeye.
Sembeye
aliipongeza kampuni ya TBL Group na ABInBev kwa kuanzisha mkakati wa
kushirikiana na makampuni ya wasomi wabunifu kutafuta njia ya
kuwawezesha wakulima wadogowadogo kuongeza uzalishaji kupitia matumizi
ya teknolojia za kisasa “Nawaasa mhakikikishe kazi za washindi wa leo na
mawazo mazuri yaliyopatikana kwenye kongamano hilo yafanyiwe kazi kwa
lengo lililokusudiwa la kuongeza uzalishaji kwa wakulima wadogo kupitia
teknolojia za kisasa.
Kwa
upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Mpango wa Kuendeleza
Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGGOT), Geoffrey Kirenga ,alisema
kuwa wakati umefika sasa wa watanzania kuchangamkia fursa zilizopo
kwenye kilimo badala ya kubaki nyuma kama watazamaji.
Aliwataka
pia wasomi wa kitanzania kuendelea kufanya tafiti mbalimbali za
kuboresha sekta ya kilimo sambamba na ubunifu wa nyenzo za kisasa na
kuongeza kuwa vijana ambao ni wengi wasiogope kujiingiza huko kwa kuwa
kuna fursa kubwa “Tunapoongelea kilimo cha kisasa na cha kisayansi
hatupaswi kuwaacha vijana nyuma kwa kuwa ndio watumiaji wakubwa wa vifaa
vya teknolojia za kisasa,wakivitumia kwa shughuli za kilimo wanaweza
kunufaika na kuinua maisha yao”, alisema.
Mkurugenzi
wa kitengo cha sheria na Masuala ya Ndani wa kiwanda cha bia cha
Nile,nchini Uganda kilichopo chini ya kampuni ya ABINBEV,Onapito
Okomoloit,, alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki wapo maelfu ya
wakulima wadogowadogo wa zao la Shahiri na mtama wanaoshirikiana na
kampuni ya ABInBev katika nchi za Tanzania na Uganda kupitia kampuni
zake tanzu za Tanzania Breweries Limited (TBL) na Nile Breweries Limited
(NBL),ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa
mvua,wakiwezeshwa kiteknolojia wataongeza uzalishaji na maisha yao kuwa
bora.
Mwanzilishi
wa taasisi ya Bits&Bytes Convention,Zuweina Farah ,amesema kuwa
kongamano la mwaka huu limepata mafanikio makubwa hususani kwa kutoka na
maazimio ya kupambana na changamoto za wakulima wadogo na kuzitafutia
ufumbuzi lengo kubwa likiwa ni kuwakwamua.
No comments:
Post a Comment