Wednesday, February 18, 2026

Kilimo cha Mabiringanya: Kuanzia Kupanda hadi Sokoni



Uchaguzi wa Mbegu

  • Tumia mbegu bora (hybrid au OPV zilizoidhinishwa).
  • Chagua aina inayokubalika sokoni (zambarau ndefu au kijani).

     Kuandaa Kitalu

  • Tengeneza kitalu sehemu yenye kivuli kidogo.
  • Panda mbegu kwa mistari, funika kwa udongo laini.
  • Mwagilia kila siku bila kuzidisha maji.
  • Miche hukua tayari kupandikizwa ndani ya siku 21–30.

   Maandalizi ya Shamba

  • Lima na kulainisha udongo (tifutifu unaopitisha maji).
  • Weka samadi au mboji.
  • Tengeneza matuta kwa nafasi ya cm 60 x 60.

    Kupandikiza

  • Fanya jioni au asubuhi mapema.
  • Mwagilia mara baada ya kupandikiza.
  • Linda miche dhidi ya jua kali siku za mwanzo.

  Matunzo

  • Palilia mara kwa mara.
  • Weka mbolea (NPK au CAN kulingana na hatua ya ukuaji).
  • Dhibiti wadudu kama vidukari na funza.
  • Nyunyizia dawa salama kwa kufuata ushauri wa mtaalam.

  Maua na Matunda

  • Huanza kutoa maua wiki 6–8.
  • Vuna matunda yakiwa bado magumu na yenye kung’aa.

   Uvunaji

  • Huanza siku 70–90 baada ya kupandikiza.
  • Vuna mara 2–3 kwa wiki.
  • Epuka kuvuna matunda yaliyozeeka (huwa machungu).

  Ufungashaji na Soko

  • Panga kwenye kreti au vikapu visivyobanwa.
  • Epuka jua kali baada ya kuvuna.
  • Masoko: masoko ya mijini, hoteli, shule, na wauzaji wa jumla.
  • Bei hubadilika kulingana na msimu—zao la kiangazi huwa na bei nzuri .
  • KAMA UNAITAJI KUJUA  KILIMO CHA BIRINGANYA WASILIANA NA Mkulima Jembe +255756483174

No comments:

Post a Comment