Wednesday, February 18, 2026

Kilimo cha Zao la Pilipili (Chili Pepper)





    Aina za Pilipili

  • Pilipili kali (Bird’s eye / kichaa)
  • Pilipili hoho (Bell pepper)
  • Pilipili ndefu (Cayenne)

Hatua za Kilimo

   Uchaguzi wa Mbegu

  • Tumia mbegu bora zilizoidhinishwa.
  • Chagua aina inayohitajika sokoni (kwa export au soko la ndani).

   Kuandaa Kitalu

  • Panda mbegu kwenye kitalu chenye kivuli.
  • Mwagilia kila siku.
  • Miche huwa tayari kupandikizwa baada ya siku 21–30.

  Maandalizi ya Shamba

  • Udongo tifutifu unaopitisha maji vizuri.
  • Ongeza samadi au mboji.
  • Nafasi: cm 45–60 kati ya mistari na mimea.

  Kupandikiza

  • Fanya asubuhi au jioni.
  • Mwagilia mara baada ya kupandikiza.

  Matunzo

  • Palilia mara kwa mara.
  • Weka mbolea (NPK mwanzoni, CAN au Urea baadaye).
  • Dhibiti wadudu (vidukari, thrips) na magonjwa (ukungu).

  Uvunaji

  • Huanza siku 75–90 baada ya kupandikiza.
  • Vuna mara 2–3 kwa wiki.
  • Kwa export, chagua pilipili zenye ubora na zisizo na doa.

Soko na Faida

  • Soko la ndani: masoko ya mijini, hoteli, viwanda vya chakula.
  • Soko la nje: Kenya, Ulaya, Mashariki ya Kati (hasa pilipili kali).
  • Bei hupanda kipindi cha kiangazi.

Faida za Kiafya

  • Ina Vitamin C nyingi.
  • Husaidia kuongeza kinga ya mwili.
  • Huchochea mmeng’enyo wa chakula.

 Unahitaji Makadirio ya gharama na faida kwa ekari moja pamoja na mbinu za kupata soko la uhakika.wasiliana na Mkula Jembe +255756483174

No comments:

Post a Comment