Skip to main content
Faida za Miparachichi, Miembe na Michungwa
Faida za Miparachichi, Miembe na Michungwa
- Miparachichi imekuwepo nchini kwa miaka mingi. Katika mikoa ya
kaskazini (Kilimanjaro na Arusha) pamoja na kutumika kama matunda,
maparachichi yalibeba jina la chakula cha mbwa kwa kuwa mara nyingi
yalipodondoka kutoka kwenye miti yaliliwa na mbwa. Hata hivyo, mikoa ya
kusini (Mbeya) maparachichi yamekuwa tunda muhimu katika milo yote.
- Utafiti umeonesha kwamba maparachichi yana mafuta muhimu yanayoondoa
mafuta yanayoganda kwenye mishipa ya damu. Pia yana virutubisho
vinavyofanya damu itembee kwa urahisi mwilini. Maparachichi yana
virutubisho vya vitamini E. Kwa sababu hii maparachichiyanatumika katika
kutengeneza vipodozi ya ngozi na nywele.
- Matunda ya parachichi yanaweza kuliwa kwa namna tofauti. Yanaweza
kuliwa kama kituliza njaa wakati ukisubiri chakula kingine au kilainisha
chakula baada ya mlo. Pia parachichi linaweza kuliwa sambamba na
chakula kingine kwa mfano ndizi za kuchoma. Maparachichi yanatumika pia
kutengeneza juisi.
- Matunda machanga yaliyoanguka yanatumika kuharakisha uivishaji wa ndizi kwa kuzifanya ndizi ziive zote kwa pamoja.
- Majani ya miparachichi yanatumika kulishia mifugo kama mbuzi na
ngombe wakati miti yake inatoa mbao nzuri za kutengenezea samani.
- Hivyo miparachichi inaweza kuwa chanzo kizuri cha pesa kwa familia na wajasiliamali soko lake likiboreshwa.
- Miparachichi huweza kustawi sehemu nyingi zenye hali ya hewa ya
kitropiki iliyo na kipindi cha ubaridi, joto kiasi na mvua za kutosha.
- Hivyo, hapa nchini kilimo chake kimeshamiri zaidi kwenye maeneo ya
nyanda za juu mikoa ya Mbeya, Iringa, Morogoro, Kilimajaro na Arusha.
Sehemu nyingine zilizo kwenye miinuko mfano Lushoto mkoani
- Tanga zao hili laweza kulimwa. Hata hivyo kulingana na aina ya
miparachichi, maeneo ya nyanda za chini yasiyo na vipindi virefu vya
ukame yanaweza pia kustawisha zao hili. Kwa vile miparachi ni miti inayo
kua haraka na haipukutishi majani, hivyo ni mti mzuri katika kuhifadhi
mazingira.
- Endapo miti hii itapandwa kwa wingi itakuwa ni kivuto cha ukusanyaji
wa hewa ya ukaa inayotokana na ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi.
1.2 MIEMBE
- Embe ni tunda maarufu na limekuwa likitambulika kama mfalme wa
matunda. Matunda ya embe yanatumika yakiwa mabichi au yameiva. Matunda
yaliyoiva yanaliwa kama tunda au pia yanaweza kutengenezwa juisi na jam.
- Embe mbichi hutumika katika kutengeneza achali. Kama ilivyo kwa
miparachichi, miembe hukua haraka na haipukutishi majani na hivyo ni mti
unaobadilisha mazingira ya mashamba na kuleta hali ya ukijani kwa mwaka mzima.
- Miti ya miembe ikipandwa kwa mpango mzuri mashambani inasaidia
kurekebisha hali ya hewa kwa kupunguza joto, kuvuta mawingu ya mvua,
kupunguza kasi ya upepo, kupunguza mmomonyoko wa ardhi na kufyonza hewa
ya ukaa.
- Hivyo Miembe nayo ni miti mizuri kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
- Miti hii ikipandwa mashambani kwa mpangilio mzuri wakulima wataweza
kulima mazao menginena hivyo kujipatia fedha zaidi, matunda na hata
kuni.
- Miembe hustawi sehemu zenye joto la wastani na lenye maji au mvua za
kutosha, hata hivyo miembe haistawi vizuri katika maeneo yenye baridi
kali na mvua nyingi kwa mwaka kwa kuwa inahitaji kipindi cha ukame cha
miezi isiyopungua miwili hadi mitatu ili kuwezesha kutoa maua. Pia
miembe hihutaji udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi
chumvi.
1.3 MICHUNGWA
- Michungwa pamoja na aina ya matunda yaliyo kwenye jamii yake kama
vile machenza, madaransi, mapomelo, malimau, ndimu n.k. pia ni matunda
maarufu katika sehemu za nchi za joto na zile za joto kiasi.
- Matunda haya hutumika mara nyingi yakiwa yameiva kwa kuyala moja kwa moja au kutengeneza juisi na jam.
- Yana vitamini C nyingi pamoja virutubisho vingine vinavyohitajika kwa mwanadamu.
- Machungwa pamoja na jamii yake huwapa wakulima faida wakati wa mauzo
na pia huongeza thamani ya mashamba yao. Wadau wengi hunufaika kutokana
na kilimo cha matunda haya. Kwa mfano walanguzi na wafanya biashara
wengine kama wale wasafirishaji hujipatia faida.
- Miti ya michungwa kama ilivyo kwa miti mingine, kutumia hewa ya ukaa na hutengeneza kivuli na hivyo kupoza joto.
- Michungwa huweza kustawi kutoka ukanda wa pwani hadi sehemu za
miinuko ya kiasi cha mita 2000 kutoka usawa wa bahari. Pia miembe
hihutaji udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi chumvi.
- Machungwa pia huhitaji kipindi kifupi cha ukame ambapo baada ya kupata maji hutoa maua.
Comments
Post a Comment