Friday, April 24, 2026

PONGEZI KWA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KWA KUIMARISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA

 YAH: PONGEZI KWA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KWA KUIMARISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA DRONES KATIKA KILIMO

Uongozi wa MKULIMA JEMBE unapenda kutoa pongezi za dhati kwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa juhudi zake zinazoendelea za kuimarisha matumizi ya teknolojia ya kisasa, hususan ndege nyuki (drones), katika kufundishia na kuendeleza sekta ya kilimo nchini.

Hatua hii ni ya kupongezwa kwa k
uwa inaonesha dhamira ya dhati ya chuo hicho katika kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani, pamoja na kuwajengea wanafunzi ujuzi wa vitendo unaokidhi mahitaji ya soko la ajira la sasa na la baadaye.

Matumizi ya teknolojia ya drones katika kilimo yana mchango mkubwa katika kuongeza tija, kupunguza gharama za uzalishaji, na kuboresha usimamizi wa shughuli za kilimo. Aidha, yanafungua fursa mpya kwa vijana kujiajiri na kuifanya sekta ya kilimo kuwa ya kisasa na yenye mvuto zaidi.

Tunatambua pia jitihada za uongozi wa chuo, wahadhiri pamoja na wadau mbalimbali wanaoshirikiana na SUA kuhakikisha kuwa teknolojia hizi zinafikia wanafunzi na kutumika ipasavyo katika mafunzo ya vitendo.

MKULIMA JEMBE tunaamini kuwa hatua hii italeta mageuzi chanya katika sekta ya kilimo nchini na kuchangia katika kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.

Tunawahimiza wadau wengine wa elimu na kilimo kuiga mfano huu ili kuendelea kuijenga Tanzania yenye kilimo chenye tija na kinachotumia teknolojia ya kisasa.

Imetolewa na:
Uongozi wa MKULIMA JEMBE

Moshi kilimanjaro

No comments:

Post a Comment