MKULIMA JEMBE BLOG

NI JUHUDI ZETU VIJIJI KUWA MIJI

📰 MAKALA MPYA >TARI Seliani Yaelekezwa Kuongeza Tafiti za Mbegu Bora na Kugeuza Utafiti Kuwa Fursa ya Biashara >Miche 5,000 ya Miti Yatolewa Kulinda Mlima Kilimanjaro

Saturday, April 25, 2026

MRADI WA ETHANOL TPC KUCHOCHEA UCHUMI, KUKAMILIKA DESEMBA 2026



 

Mwaka jana, mwezi Novemba 2025, kiwanda cha kuzalisha sukari cha TPC kilitangaza uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Shilingi bilioni 130 katika mradi wa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, ikiwemo Extra Neutral Alcohol (Ethanol).

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Utawala wa TPC, Jafary Ally, mradi huo unaendelea kutekelezwa na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2026. Kukamilika kwake kunatarajiwa kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi wa eneo husika na taifa kwa ujumla.

Mradi huo hautalenga uzalishaji wa ethanol pekee, bali pia utahusisha uzalishaji wa nishati mbadala, mbolea ya potassium, pamoja na hewa ukaa (carbon dioxide) kwa matumizi ya viwandani. Aidha, TPC inapanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati 2 za sasa hadi megawati 7, ambapo sehemu ya umeme huo atauzwa kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Faida nyingine inayotarajiwa ni kuongezeka kwa ajira kwa wananchi, sambamba na kuboresha mazingira kupitia matumizi bora ya rasilimali zilizopo.

Hivyo basi, wadau wa kilimo na viwanda wanashauriwa kufuatilia kwa karibu maendeleo ya mradi huu mkubwa, ambao unatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo cha miwa na viwanda vinavyotegemea mazao yake.

No comments:

Post a Comment