Nakukalibisha mpenzi msomaji wa blog yetu pendwa, nahuu niwakati
mwingine tena wa kuendelea kujifunza mambo mengi zaidi kuhusiana na
kilimo. Na leo nitakuelezea kanuni za kunyunyuzia dawa shambani.
Hawali ya yote nataka kukuelezea maana ya kunyunyuzia dawa au spraying kwa lugha ya kitaalamu.
kunyunyuzia(spraying) nikitendo cha kulinda mazao na wadudu na magonjwa
kwa kusambaza kiasi kidogo cha viwatilifu katika mmea mama.
Chemikali unyunyuziwa kama mchanganyiko kwa kiasi kidogo, kati au
kikubwa juu ya mmea mama ili kuulinda na wadudu au ugonjwa flani kwa
hali ya kimiminika.
UNAWEZA KUTIZAMA KAMA ULIPITWA NA KILIMO BORA CHA MATANGO
VIFAA TOFAUTI TOFAUTI VYA KUNYUNYUZIA DAWA/ VIWATILIFU
Aina tofauti tofauti ya vinyunyuzi hutumiwa kulingana na aina ya zao,
kipata cha mkulimwa na ukubwa wa shamba, vifuatavyo ni vifaa hivyo.
AERIAL SPRAYER; hiki ni kifaa kinacho huusisha ndege katika
kunyunyuzia, ni mahususi katika zao la viazi au mazao mengine ya mboga
mboga ambayo uhitaji kutibiwa katika kipindi ambacho mataili ya trekta
yanaweza kujeruhi mazao hayo
MANUAL KNAPSACK SPRAYER; Hiki ni kifaa ambacho mnyunyuziaji
hukibeba mgongoni na kutumia mkono wake mmoja kupamp na mwingine
kuelekeza nozzle katika mazao, na kifaa hiki hubeba little 5 hadi 15 za
dawa iliyo changanya na maji.
MOTORIZED KNAPSACK SPRAYER; Hiki ni kifaa ambacho pia
kinafanana na nilicho kitaja mara ya pili, tofauti yake hiki kinakua na
engine ambayo huzunguka na kuwezesha dawa kwenda umbali mrefu, kifaa
hiki utumiwa mahali ambapo Manual knapsack sprayer kinakua hakina uwezo
wa kufikisha mfano miti. na kifaa hiku hubeba little 15 hadi 20.
TREE SPRAYER; Hiki kifaa hutumika kunyunyuzia dawa katika miti midogo, mfano miti ya matunda.
BOOM SPRAYER; pia kifaa hiki hutumika kunyunyuzia dawa katika
mashamba makubwa sana, na hufanya kazi kwa kuambatanisha katika trekta.
kifaa hiki ubeba litter tofauti tofauti mfano 4000, 6000 nakadhalika.
KANUNI ZA KUNYUNYUZIA DAWA.
Zifuatazo ni kanunu muhimu ambazo unatakiwa uzingatie wakati wa kunyunyuzia dawa.
angalia uelekeo wa upepo kabla ya kunyunyuzia dawa,
nilazima uvae vifaa vya kukulinda mfano groves na mask
hakikisha kifaa chako kimefungwa vizuri
osha kifaa chako cha kunyunyuzia kabla na baada ya kukitumia
tunza kifaa chako mahali safi na kavu
changanya na koroga dawa yako vizuri kabla ya kunyunyuzia
hakikisha unatumia vipo sahihi.
Bila shaka mpenzi msomache umejifunza mengi zaidi katika somo hili, usiache kujiunga na blog hii na pia katika channel yetu ya youtube ili kujifunza mengi zaidi.
Kamati ya Taifa ya Mbegu (National
Seed Committee) imeidhinisha matumizi ya aina 29 za mbegu mpya za mazao
mbalimbali ya kilimo, mazao hayo ni mahindi,mpuga,alizeti karanga na
chai.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi
Mhe. Mwigulu Nchemba kwa vyombo vya habari, inasema kuidhinishwa kwa
aina hizo za mbegu kunafuatiwa mapendekezo yaliyofanywa na kamati ya
Taifa ya kupitisha aina mpya ya mbegu za mazao (The National variety
Release Committee) katika kikao kilichofanyika kuanzia tarehe 16 – 17
Machi 2016, makao makuu ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Jijini Dar
es salaam.
Aidha, aina hizo mpya za mbegu zimefanyiwa utafiti na kugundulika
kuwa zinasifa mbalimbali ikiwemo kustahimili ukame,kutoa mavuno
mengi,ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu,kukomaa mapema na kupendwa na
wakulima.
Mhe. Nchemba aliongeza kuwa utafiti wa kina ulifanywa na vyuo vya
utafiti vipatavyo12 na kuweza kuzalisha aina mpya za mbegu hivyo
kupatikana aina 16 za mahindi,2 za mpunga, 4 za alizeti, 3 za karanga na
4 za chai.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa aina hizo za mbegu zitaanza kuzalishwa na
makampuni mbalimbali ya uzalishaji mbegu pamoja na Wakala wa Taifa wa
mbegu za kilimo (Agriculture Seeds Agency-ASA), kwa lengo la kuzifikisha
aina hizo mpya za mbegu bora kwa wakulima kuanzia msimu ujao wa kilimo
2017/2018.
“ Hatua hiyo ya kamati inalenga kuongeza tija na kipato kwa mkulima”, iliongeza sehemu ya taarifa hiyo ya Mhe. Nchemba.
Mapapai ni zao moja kati ya mazao ya matunda yenye vitamini A na madini ya kalsiamu kwa
wingi. Inaamanika asili ya papai, ni huko nchi za Amerka ya kati,
(Mexico), ndipo zao ili likasambaa duniani kote. Kwa sasa zao hili
hulimwa karibu kila mahali hapa nchini. Papai ni moja ya mazao yenye
faida kubwa na yenye soko la uhakika. Ekari moja ya papai ikitunzwa
vizuri inaweza kukupatia faida ya zaidi ya milioni 20 kwa kipindi cha
miaka 2 hadi 3.
Kuna aina 3 za mbegu za papai.
1. Mbegu za kienyeji (local varieties). hizi ni aina ya papai za
kienyeji ambazo, mara nyingi hazifahamiki majina yake. Mbegu zake huwezi
zipata kwenye mfumo rasmi wa mbegu (madukani) nk. mara nyingi mbegu
hizi hupatikana kwa kuchukua matunda yaliyoiva na kuchukua mbegu zake..
kiswahili cha mtaani husema mbegu za kukamua..
2. Aina za kawaida (open pollinated varieties kwa kifupi OPV). Mfano wake ni kama Calina nk hizi hua na uzao wa kati.
3. Chotara (hybrid). Mfano Malkia F1, Sinta F1, Red royal mk. Hizi
hufanya vizuri maeneo mengi.. hua na uzao mkubwa kuliko aina nyingine
tulizojifunza hapo juu
MAMBO YA KUZINGATIA WAK ATI WA UZALISHAJI
Ili kupata mazao yenye ubora unaotakiwa ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo bora za uzalishaji
wa mapapai. Ubora wa matunda baada ya kuvunwa hutegemea jinsi yalivyozalishwa. Baadhi
ya kanuni hizo ni kama zifuatazo:
Kuchagua aina bora
Chagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya soko.
Kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu
Mapapi hushambuliwa kwa urahisi na magonjwa na wadudu, hivyo ni muhimu kufanya ukaguzi
wa mara kwa mara ili kugundua dalili za mashambulizi.
Endapo kuna dalili za mashambulizi, dhibiti mapema ili kuzalisha mazao bora yanayoweza
kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Pia hakikisha shamba na barabara zake ni safi wakati wote ili kurahisisha uvunaji na
usafirishaji.
Maandalizi kabla ya kuvuna
Kukagua shamba
Kagua shamba kuona kama kuna mapapai yaliyokomaa
Mapapai hukomaa katika kipindi cha miezi minne hadi mitano kutoka maua yanapochanua.
Dalili za mapapai yaliyokomaa
Tunda hubadilika rangi kutoka kijani kibichi na kuwa ya kijani nyepesi hadi manjano.
Kuandaa vifaa vya kuvunia, kufungashia na kusafirishia
Vifaa vya kuvunia
Vichumio
Mifuko
Ngazi
Vifaa vya kufungashia
Makasha ya mbao/ plasitiki au makaratasi magumu
Vyombo vya kusafirishia
Mikokoteni
Magari
Matela ya matrekta
Kuvuna
Uvunaji bora wa mapapai ni wa kutumia mikono ambapo tunda huchumwa kwa mkono au kwa kutumia vichumio maalumu.
Vuna mapapai yaliyokomaa tu
Vuna mapapai pamoja na vikonyo vyake
Vuna kwa uangalifu ili kuepuka kudondosha matunda
Matunda yakidondoka, huchubuka, hupasuka au hupondeka hivyo husababisha upotevu.
W eka mapapai kivulini mara baada ya kuvuna
Kuchambua, Kusafisha na Kupanga Madaraja
Ni muhimu kuchambua mapapai ili kutenga yaliyooza, kupasuka na yenye
dalili za magonjwa au kubonyea. Lengo la kuchambua ni kupata matunda
yenye ubora kulingana na matumizi , kwa mfano kusindika, kuuza au
kusafirisha.
Matunda yaliyooza na yenye wadudu ni vyema yafukiwe ili kuangamiza wadudu waharibifu
na vimelea vya magonjwa, na pia kuzuia kuenea kwa wadudu na magonjwa hayo.
Matunda yaliyopasuka, kubonyea au kuchubuka kidogo yatumike haraka kwa kuliwa.
Matunda mazuri ambayo hayajapata madhara yoyote yatumike kwa ajili ya kusindika, kuliwa, kuuzwa au kusafirishwa.
Kilimo cha Viazi Vitamu (sweet Potatoes)
Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi
nchini Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja
kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame.
Zao la viazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini.
Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza,
Shinyanga, Dodoma, Morogoro, Kagera, Arusha na Ruvuma. Matumizi
Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia
mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu
hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati, tambi na
Juice. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha
mboji. Aina
Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini
Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C,
Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli,
Sinia,Vumilia, Kabode, na Polista Uzalishaji
Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Viazi hustawi vizuri
katika maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji
kupenya kwa urahisi. Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai
kwani huzuia mizizi kupenya na kupanuka.
Shamba jipya litayarishwe vizuri kwa kufyeka vichaka na kungoa visiki.
Majani yafukiwe wakati wa kutengeneza matuta ili kuongeza rutuba ya
udongo.
Viazi vipandwe kwa kutumia Marando yenye urefu wa sentimita 30 kwa
mavuno bora. Inashauriwa kutumia sehemu ya juu ya shina kwa mavuno
zaidi. Marando yapandwe katika umbali wa sentimita 25 hadi 30 kutoka
mmea hadi mmea na sentimita 60 hadi 75 kutoka tuta hadi tuta. Viazi pia
vyaweza kupandwa kwa kutumia viazi vyenye afya vyenye uzito wa kati ya
gramu 20 hadi 30. Hata hivyo inashauriwa kutumia marando ili kupata
mavuno zaidi na kuepuka kuenea kwa magonjwa. Kutunza shamba
Ni muhimu kupalilia viazi vitamu katika miezi miwili ya mwanzo ili kuupa
mmea nguvu ya kutambaa vizuri. Baada ya muda huo, viazi huweza kufunika
ardhi na hivyo huzuia uotaji wa magugu.
Viazi hushambuliwa na wadudu mbalimbali wakiwemo kipepeo, mbawa kavu,
fukusi na minyoo fundo.Pia hushambuliwa na magonjwa yakiwemo magonjwa
yanayotokana na virusi kama Sweet Potato Chlorotic Stunt virus (SPCSV).
Magonjwa na wadudu yaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia usafi wa shamba,
kubadilisha mazao, na kuzingatia udhibiti sango. Uvunaji
Viazi vitamu huwa tayari kuvunwa miezi mitatu hadi minne tangu kupanda
kutegemea hali ya hewa. Viazi vinaweza kuvunwa kidogo kidogo kwa kutumia
mikono, vijiti, jembe, au rato kadri vinavyohitajika. Aidha inashauriwa
viazi visiachwe ardhini muda mrefu bila kuvunwa kwani vitakomaa sana na
kuwa na nyuzi, na hivyo kuharibu ubora wake. Pia kuacha viazi muda
mrefu hukaribisha mashambulizi ya wadudu kama fukusi na kuoza. Kwa
maeneo makubwa zaidi, inashauriwa kutumia mashine ya kukokotwa na
ngombe. Uvunaji ufanywe kwa uangalifu ili kuhakikisha viazi
visikatwekatwe wala kuchubuliwa wakati wa kuvuna.
Mavuno ya viazi hutofautiana kulingana na aina, hali ya hewa, na udongo. Mavuno ya viazi yanakadiriwa kufikia tani 20 kwa hekta.
Kwa mahitaji ya mbegu za viazi vitamu au ushauri wowote kuhusu kilimo wasiliana nasi kupitia:
simu; 0756 483 174 Email:tupashanehabari@gmail.com
Miparachichi imekuwepo nchini kwa miaka mingi. Katika mikoa ya
kaskazini (Kilimanjaro na Arusha) pamoja na kutumika kama matunda,
maparachichi yalibeba jina la chakula cha mbwa kwa kuwa mara nyingi
yalipodondoka kutoka kwenye miti yaliliwa na mbwa. Hata hivyo, mikoa ya
kusini (Mbeya) maparachichi yamekuwa tunda muhimu katika milo yote.
Utafiti umeonesha kwamba maparachichi yana mafuta muhimu yanayoondoa
mafuta yanayoganda kwenye mishipa ya damu. Pia yana virutubisho
vinavyofanya damu itembee kwa urahisi mwilini. Maparachichi yana
virutubisho vya vitamini E. Kwa sababu hii maparachichiyanatumika katika
kutengeneza vipodozi ya ngozi na nywele.
Matunda ya parachichi yanaweza kuliwa kwa namna tofauti. Yanaweza
kuliwa kama kituliza njaa wakati ukisubiri chakula kingine au kilainisha
chakula baada ya mlo. Pia parachichi linaweza kuliwa sambamba na
chakula kingine kwa mfano ndizi za kuchoma. Maparachichi yanatumika pia
kutengeneza juisi.
Matunda machanga yaliyoanguka yanatumika kuharakisha uivishaji wa ndizi kwa kuzifanya ndizi ziive zote kwa pamoja.
Majani ya miparachichi yanatumika kulishia mifugo kama mbuzi na
ngombe wakati miti yake inatoa mbao nzuri za kutengenezea samani.
Hivyo miparachichi inaweza kuwa chanzo kizuri cha pesa kwa familia na wajasiliamali soko lake likiboreshwa.
Miparachichi huweza kustawi sehemu nyingi zenye hali ya hewa ya
kitropiki iliyo na kipindi cha ubaridi, joto kiasi na mvua za kutosha.
Hivyo, hapa nchini kilimo chake kimeshamiri zaidi kwenye maeneo ya
nyanda za juu mikoa ya Mbeya, Iringa, Morogoro, Kilimajaro na Arusha.
Sehemu nyingine zilizo kwenye miinuko mfano Lushoto mkoani
Tanga zao hili laweza kulimwa. Hata hivyo kulingana na aina ya
miparachichi, maeneo ya nyanda za chini yasiyo na vipindi virefu vya
ukame yanaweza pia kustawisha zao hili. Kwa vile miparachi ni miti inayo
kua haraka na haipukutishi majani, hivyo ni mti mzuri katika kuhifadhi
mazingira.
Endapo miti hii itapandwa kwa wingi itakuwa ni kivuto cha ukusanyaji
wa hewa ya ukaa inayotokana na ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi.
1.2 MIEMBE
Embe ni tunda maarufu na limekuwa likitambulika kama mfalme wa
matunda. Matunda ya embe yanatumika yakiwa mabichi au yameiva. Matunda
yaliyoiva yanaliwa kama tunda au pia yanaweza kutengenezwa juisi na jam.
Embe mbichi hutumika katika kutengeneza achali. Kama ilivyo kwa
miparachichi, miembe hukua haraka na haipukutishi majani na hivyo ni mti
unaobadilisha mazingira ya mashamba na kuleta hali ya ukijani kwa mwaka mzima.
Miti ya miembe ikipandwa kwa mpango mzuri mashambani inasaidia
kurekebisha hali ya hewa kwa kupunguza joto, kuvuta mawingu ya mvua,
kupunguza kasi ya upepo, kupunguza mmomonyoko wa ardhi na kufyonza hewa
ya ukaa.
Hivyo Miembe nayo ni miti mizuri kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Miti hii ikipandwa mashambani kwa mpangilio mzuri wakulima wataweza
kulima mazao menginena hivyo kujipatia fedha zaidi, matunda na hata
kuni.
Miembe hustawi sehemu zenye joto la wastani na lenye maji au mvua za
kutosha, hata hivyo miembe haistawi vizuri katika maeneo yenye baridi
kali na mvua nyingi kwa mwaka kwa kuwa inahitaji kipindi cha ukame cha
miezi isiyopungua miwili hadi mitatu ili kuwezesha kutoa maua. Pia
miembe hihutaji udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi
chumvi.
1.3 MICHUNGWA
Michungwa pamoja na aina ya matunda yaliyo kwenye jamii yake kama
vile machenza, madaransi, mapomelo, malimau, ndimu n.k. pia ni matunda
maarufu katika sehemu za nchi za joto na zile za joto kiasi.
Matunda haya hutumika mara nyingi yakiwa yameiva kwa kuyala moja kwa moja au kutengeneza juisi na jam.
Yana vitamini C nyingi pamoja virutubisho vingine vinavyohitajika kwa mwanadamu.
Machungwa pamoja na jamii yake huwapa wakulima faida wakati wa mauzo
na pia huongeza thamani ya mashamba yao. Wadau wengi hunufaika kutokana
na kilimo cha matunda haya. Kwa mfano walanguzi na wafanya biashara
wengine kama wale wasafirishaji hujipatia faida.
Miti ya michungwa kama ilivyo kwa miti mingine, kutumia hewa ya ukaa na hutengeneza kivuli na hivyo kupoza joto.
Michungwa huweza kustawi kutoka ukanda wa pwani hadi sehemu za
miinuko ya kiasi cha mita 2000 kutoka usawa wa bahari. Pia miembe
hihutaji udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi chumvi.
Machungwa pia huhitaji kipindi kifupi cha ukame ambapo baada ya kupata maji hutoa maua.
Serikali imepanga kuanza matumizi ya vituo maalum vya kuuzia mazao
ili kuwasaidia wakulima kudhibiti ubora wa mazao yao, kupata taarifa za
masoko na kuimarisha ushindani wa bei.
Makubaliano ya matumizi ya vituo hivyo yamefikiwa na Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Bodi ya Usimamizi Stakabadhi za
Ghala na Halmashauri za maeneo yanayotekeleza Mfumo wa stakabadhi.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa
fedha 2017/18, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
amesema kwamba serikali inahamasisha ushindani kwa kutumia vituo maalum
na Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ambao umefanikisha uuzaji wa mazao kwa
uwazi na hivyo kumpatia mkulima bei shindani.
“Utaratibu huo umewezesha bei ya Korosho kupanda na kufikia wastani
wa Shilingi 3,880 kwa kilo msimu wa 2017/2018 ikilinganishwa na Shilingi
3,346 kwa kilo msimu wa 2016/2017 hivyo mfumo huu ni bora ukilinganisha
na utaratibu wa awali” alisema Mwijage.
Aidha, mauzo ya Korosho kupitia Mfumo huo yameongezeka kutoka tani
249,912 msimu wa 2016/2017 hadi tani 291,614 msimu wa 2017/2018 sawa na
ongezeko la asilimia 16.7.
Mwijage amevitaja vituo ambavyo vinaendelea kuboresha utendaji wake
kuwa ni vya mipaka ya Holili/Taveta, Sirari/Isebania, Namanga/Namanga,
Kabanga/Kobero, Rusumo/Rusumo, Mutukula/Mutukula pamoja na
Horohoro/Lungalunga.
Aidha, ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Tunduma/Nakonde
upande wa Tanzania ulioanza mwezi Novemba 2016, unatarajiwa kukamilika
mwezi Mei 2018. Hadi kufikia mwezi Februari 2018 ujenzi wa kituo hicho
umefikia asilimia 75.
Washindi wa shindano la ubunifu wa kiteknolojia katika picha ya pamoja na mgeni rasmi baada ya kukabidhiwa zawadi zao
**
Wataalamu
mbalimbali walioudhuria kongamano la The East Africa (EA) Innovation
Event la kampuni mama ya TBL Group ya ABInBev lenye lengo la kuleta
mapinduzi ya kilimo kupitia sayansi na teknolojia lililoandaliwa na
taasisi ya Bits&Bites Technology Convention na kufanyika jijini Dar
es Salaam, wamedhihirisha kuwa mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo
nchini na barani Afrika kwa ujumla yanawezekana kupitia matumizi ya
teknolojia za kisayansi.
Kongamano
hilo ambalo lilijumuisha wataalamu wa fani ya kilimo,watafiti,wahandisi
na wabunifu kutoka kanda ya Afrika Mashariki walijadili jinsi ya kupata
ufumbuzi wa kuinua kilimo cha wakulima wadogo kupitia teknolojia za
kisasa na za gharama nafuu ambapo pia walishiriki shindano la ubunifu wa
nyenzo za kiteknolojia ambapo walipata fursa ya kuwasilisha kazi zao
walizogundua.
Makampuni
ya Imara Tech,Mobisol na Back Save Equipment yaliibuka na ushindi baada
ya jopo la majaji waliokuwa wanasimamia shindano hilo kubainisha kuwa
ugunduzi wao wa nyenzo za kiteknolojia unaweza kusaidia kuinua maisha ya
wakulima wadogo.Kazi zilizowapatia ushindi washiriki zitaanza kufanyiwa
majaribio kabla ya mchakato wa kuzifikisha kwa walengwa ambao ni
wakulima hususani wadogo wadogo.
Akiongea
wakati wa kufunga kongamano hilo, Mkurugenzi wa taasisi ya Tanzania
Private Sector Foundation (TPSF), Godfrey Sembeye, alisema kuwa
kongamano hili limefanyika kwa wakati mwafaka ambapo Tanzania inajipanga
kuingia katika uchumi wa viwanda ambao unaenda sambamba na kufanya
mapinduzi ya kilimo kwa ajili ya kupata malighafi ya viwanda
vitakavyoanzishwa,pia kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha.
Sembeye,
alisema njia pekee ya kuleta mapinduzi ya kilimo ni kupitia matumizi ya
teknolojia ya kisasa na za gharama nafuu ambazo wakulima wengi wa hali
ya chini wanaweza kumudu kuzinunua na kuzitumia kwa ajili ya kuwawezesha
kupata tija na ufanisi katika kazi zao.
“Kutokana
na taarifa za tafiti mbalimbali imebainishwa kuwa bara la Africa lina
hekari 600 milioni ambazo hazitumiki ambazo zikitumika ipasavyo zitaweza
kuzalisha chakula cha kulisha watu wapatao bilioni 9 hadi kufikia mwaka
2050 na ardhi hii haitanufaisha bara la Afrika tu bali dunia nzima,
sekta ya kilimo inaonekana kuwa na fursa kubwa, kinachotakiwa ni
kujipanga kuhakikisha inaenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolia
yanayobadilika kila siku”,alisema Sembeye.
Sembeye
aliipongeza kampuni ya TBL Group na ABInBev kwa kuanzisha mkakati wa
kushirikiana na makampuni ya wasomi wabunifu kutafuta njia ya
kuwawezesha wakulima wadogowadogo kuongeza uzalishaji kupitia matumizi
ya teknolojia za kisasa “Nawaasa mhakikikishe kazi za washindi wa leo na
mawazo mazuri yaliyopatikana kwenye kongamano hilo yafanyiwe kazi kwa
lengo lililokusudiwa la kuongeza uzalishaji kwa wakulima wadogo kupitia
teknolojia za kisasa.
Kwa
upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Mpango wa Kuendeleza
Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGGOT), Geoffrey Kirenga ,alisema
kuwa wakati umefika sasa wa watanzania kuchangamkia fursa zilizopo
kwenye kilimo badala ya kubaki nyuma kama watazamaji.
Aliwataka
pia wasomi wa kitanzania kuendelea kufanya tafiti mbalimbali za
kuboresha sekta ya kilimo sambamba na ubunifu wa nyenzo za kisasa na
kuongeza kuwa vijana ambao ni wengi wasiogope kujiingiza huko kwa kuwa
kuna fursa kubwa “Tunapoongelea kilimo cha kisasa na cha kisayansi
hatupaswi kuwaacha vijana nyuma kwa kuwa ndio watumiaji wakubwa wa vifaa
vya teknolojia za kisasa,wakivitumia kwa shughuli za kilimo wanaweza
kunufaika na kuinua maisha yao”, alisema.
Mkurugenzi
wa kitengo cha sheria na Masuala ya Ndani wa kiwanda cha bia cha
Nile,nchini Uganda kilichopo chini ya kampuni ya ABINBEV,Onapito
Okomoloit,, alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki wapo maelfu ya
wakulima wadogowadogo wa zao la Shahiri na mtama wanaoshirikiana na
kampuni ya ABInBev katika nchi za Tanzania na Uganda kupitia kampuni
zake tanzu za Tanzania Breweries Limited (TBL) na Nile Breweries Limited
(NBL),ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa
mvua,wakiwezeshwa kiteknolojia wataongeza uzalishaji na maisha yao kuwa
bora.
Mwanzilishi
wa taasisi ya Bits&Bytes Convention,Zuweina Farah ,amesema kuwa
kongamano la mwaka huu limepata mafanikio makubwa hususani kwa kutoka na
maazimio ya kupambana na changamoto za wakulima wadogo na kuzitafutia
ufumbuzi lengo kubwa likiwa ni kuwakwamua.
Serikali itahakikisha kuwa mbolea
inawafikia wakulima kwa wakati katika msimu ujao ili kuchochea ukuaji wa
sekta ya kilimo hapa nchini hali itakayoongeza ari ya utekelezaji wa
dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda. Akizungumza Bungeni mjini Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa katika msimu
ujao, Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mbolea na
pembejeo nyingine katika maeneo yao wakati wote wanapohitaji. “Tutaandaa utaratibu maalum wa
kuwajengea uwezo wabunge wote kuhusu utaratibu mpya wa ununuzi wa mbolea
kwa pamoja ili Waheshimiwa Wabunge waweze kutoa maoni yao hali
itakayosaidia kuboresha mfumo tuliouweka wa uagizaji wa mbolea kwa
pamoja”, alisisitiza Dkt. Tizeba Akifafanua zaidi, Dkt. Tizeba amesema
kuwa ni matumaini yake kuwa baada ya wabunge kujengewa uwezo watakuwa na
uelewa mzuri kuhusu utaratibu huo hali itakayoondoa sintofahamu iliyopo
kuhusu utaratibu mpya wa uagizaji na usambazji wa mbolea kwa pamoja. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa
Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa, akijibu swali la mbunge wa Hanang
Dkt. Mery Nagu aliyetaka kujua ni kwa nini vocha zimepungua na lini
Serikali itaanzisha mfumo mpya wa pembejeo. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa ili
kuboresha usambazaji wa pembejeo kwa wakulima katika msimu wa mwaka
2017/2018 mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement
system- BPS) umeongeza upatikanaji wa mbolea kwa wingi, bei nafuu na
wakati. Aidha, kwa kutumia utaratibu huo bei za mbolea aina ya DAP na UREA zimepungua kwa wastani wa asilimia 30. “Serikali kupitia mfumo wa ununuzi wa
mbolea kwa pamoja hutoa bei elekezi kwa kuzingatia umbali kutoka makao
makuu ya wilaya kwenda Kata na vijiji”, alisisitiza Mhe. Dkt. Mwanjelwa. Akifafanua zaidi, Dkt. Mwanjelwa
alisema kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) inaendelea kufanya
ukaguzi wa mara kwa mara na pindi ukiukwaji wa bei elekezi unapobainika
hatua stahiki zinachukuliwa kwa wahusika. Serikali katika kuimarisha sekta ya
kilimo imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuimarisha kilimo kwa kuwekeza
katika pembejeo, mbolea na zana zinazoweza kuikuza sekta ya kilimo ili
iweze kuchochea uchumi wa viwanda.
Washiriki wa mafunzo kutoka Mikoa 13 Nchini wakifuatilia mada
mada zilizokuwa zikitolewa na makufunzi wa mafunzo ya mfumo wa
uzalishaji mbegu kupitia mradi wa “Mbegu Zetu Haki Zetu” yaliyofanyika
mwishoni mwa wiki Mkoani Morogoro na kuandaliwa na Shirika la PELUM
Tanzania kupitia ufadhili wa Bread for the World
Wadau wa kilimo kutoka katika sekta binafsi nchini wameiomba Serikali
kutunga sheria ya kutambua mfumo usio rasmi wa uzalishaji wa mbegu kwa
kuwa mfumo huo unachagia zaidi ya asilimia 70 ya mbegu za kilimo nchini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki Mkoani Morogoro katika mafunzo ya mfumo wa uzalishaji mbegu kupitia mradi wa “Mbegu Zetu Haki Zetu”
yaliyoandaliwa na Shirika la PELUM Tanzania kupitia ufadhili wa Bread
for the World, Mratibu toka Shirika la TABIO Abdallah Mkindi alisema,
uundaji wa chombo cha kisheria katika mfumo wa mbegu usio rasmi
utasaidia kuleta mageuzi ya haraka katka sekta ya kilimo nchini.
“Mfumo huu wa mbegu usio rasmi unatumiwa na zaidi ya asilimia 70 ya
wakulima wote nchini hivyo basi Serikali inapaswa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa kilimo kuendeleza mfumo huu kuanzia hatua ya uchaguzi wa
mbegu, uhifadhi pamoja na tafiti shirikishi,” alisema Mkindi.
Mkindi alisema ili mfumo huo uweze kuleta tija iliyokusudiwa ni
Serikali pia itapaswa kusimamia uanzishwaji na uimarishwaji wa benki za
mbegu na hasa zile zinazopotea pamoja na kuimarisha mfumo wa usimamizi
katika utafiti wa mbegu za asili zilizopo, zinazopotea na zilizopotea
ili kuweza kuzirudisha.
Kwa mujibu wa Mkindi aliitaka Serikali pia kuongeza nguvu ya
ushirikiano na kituo cha uhifadhi wa nasaba za mimea (NPGRC) ili kujua
nasaba zilizohifadhiwa katika kituo hicho na namna zinavyoweza kuwafikia
wakulima pale zinapohitajika.
Kwa upande wake Afisa kilimo, kutoka Kituo cha Kilimo LAELA la Mkoani
Rukwa, Gaudens Masebe alisema mfumo usio rasmi wa mbegu unapaswa kuwa
na mtaala maalum katika shule za msingi na sekondari pamoja na taasisi
za elimu ya juu nchini kwa kuwa moja ya faida ya mbegu hizi ni kuwa
zinakabaliana na mazingira anayotoka mkulima na ni rahisi kuhifadhi kwa
njia za asili zisizo na gharama.
Naye Herman Hishamu, Meneja Miradi, kutoka Shirika la Island of Peace
la Mkoani Arusha alisema mbegu toka mfumo ulio rasmi zimekuwa na
changamoto nyingi kwa wakulima ikiwemo kutokuwepo na uhakika wa mbegu
hizo kuota jambo ambalo kila mwaka mkulima anabadili mbegu kwenye shamba
moja.
Aidha waalibainisha changamoto nyingine ambazo wakulima wanazipata
wanapotumia mfumo rasmi wa mbegu ambapo pamoja na mkulima kununua mbegu
bado atapaswa kununua mbolea kuweka shambani na pia kunyunyuzia madawa
kwa ajili ya kuulia wadudu na kuzuia magonjwa.
Aidha Francis Mwitumba Meneja Programu kutoka Shirika la Caritas
Mbeya alibainisha kuwa mfumo wa mbegu usio rasmi unamshirikisha moja kwa
moja mkulima toka eneo husika kufahamu hatua zote za uzalishaji mbegu
kupitia mazingira anayoishi, uchaguzi na uhifadhi wa mbegu na kupata
uhakika wa kuvuna mbegu kwa wakati husika na kwa bei nafuu.
Mradi wa “Mbegu zetu Haki zetu” unaotekelezwa na Shirika la PELUM
Tanzania kupitia Masharika wanachama 20 toka Mikoa 13 nchini na
unatarajia kukamilika mwaka 2020. Unasisistiza juu ya mfumo usio rasmi
wa mbegu ambapo kaya 400 (wakulima)toka mashirika wanachama watanufaika
mojamoja na mradi huu.
Mpunga ni miongoni mwa zao muhimu
la chakula nchini Tanzania. Uzalishaji wa mchele nchini kwa takwimu za
mwaka 2016 ni zaidi ya tani milioni 2. Tija ya uzalishaji kwa mkulima ni
wastani wa tani 1.5 -2.5 wakati katika skimu za umwagiliaji uzalishaji
unaweza kufikia hadi tani 6 kwa hekta moja.
Kilimo kilichozoeleka sana cha mpunga ni kile cha mabondeni ambapo
kinahitaji maji mengi. Katika zama hizi za mabadiliko ya tabianchi
ambapo kumekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa mvua na maji kwa
ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na kilimo cha
umwagiliaji, ni muda muafaka kuanza kuhimiza kilimo kinachotumia maji
kwa ufanisi hususan kutumia mbegu za mpunga wa nchi kavu.
Aina ya mbegu
za mpunga wa nchi kavu ni fursa kwa wakulima wengi zaidi kuzalisha
mpunga bila kulazimika kuhitaji maeneo yaliyozoeleka ya mabondeni.
Kilimo mpunga wan chi kavu ni kilimo gani? Bwana Johnson Tillya
ambaye ni Afisa kilimo wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) anasema kuwa,
kilimo cha mpunga wan chi kavu ni kile kinacholimwa maeneo yasiyo ya
mabonde, na kinachotegemea mvua. Ni kilimo kinachoweza kulimwa sawa na
maeneo yanayolimwa mahindi, kwa kifupi ni mpunga wa aina hii hauhitaji
maji mengi.
Katika kuhimiza kilimo cha mpunga cha nchi kavu, ASA imeanzisha
mashamba darasa kwa ajili ya kutambulisha kilimo cha mpunga wa nchi
kavu. Mashamba darasa hayo yalitanguliwa na Mafunzo ya wakulima viongozi
pamoja na wataalam wa kilimo yaliyofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya
Wakulima cha Mkindo.
Wakulima viongozi waliohudhuria mafunzo hayo
walipewa malengo ya kuanzisha vikundi vya wakulima katika vijiji
walivyotoka ambao watalitakiwa kuwahamasisha kuanzisha mashamba ya
vikundi ambayo yatatumika kama mashamba darasa ya kuwafundishia wana
kikundi na wakulima wengine.
Jukumu jingine la kila mwanakikundi baada
ya kupata mafunzo katika shamba darasa ilikuwa ni kueneza elimu
waliyoipata kwa angalau wakulima wengine watano. Kupitia utaratibu huo
wakulima wengi zaidi wanaweza kufikiwa kwa kupewa elimu ya kilimo bora
cha mpunga wan chi kavu kupitia wakulima wenzao waliokwishapatiwa
mafunzo kama hayo awali.
Katika mpango huu wa kuhimiza kilimo bora cha
mpungu wa nchi kavu, ASA imekuwa na jukumu la kutoa mbegu na Kampuni ya
Mbolea Tanzania ilitoa mbolea kwa kila kikundi.
Mbegu za nchi kavu za mpunga ni zipi? Bwana Tillya alisema mbegu
zilizosambazwa kwa wakulima ni NERICA 1, NERICA 2, NERICA 4 na NERICA 7.
Sifa za uzaaji wa aina za mpungu wa nchi kavu ni zipi? Bwana John
Teofili, mkulima mwezeshaji wa kijiji cha Tawa alizitaja aina za mbegu
za mpunga za nchi kavu na uwezo wake wa kuzaa kama ifuatavyo: NETICA 1
ina uwezo wa kutoa mavuno kilo 1,800 kwa eka, NERICA 2 kilo 1,600 kwa
eka, NERICA 4 kilo 2,000 kwa eka, na NERICA 7 kilo 2,000 kwa eka.
Katika ziara ya kutembelea vikundi vya wakulima vinavyoendesha
majaribio ya kilimo cha mpunga wa nchi kavu, vijiji vya Kiloka, Tawa,
Kisaki na Dala vilitembelewa. Vijiji hivyo vinapatikana Morogoro
vijijini katika safu za Milima ya Ulugulu.
Msafara huo ulijumuisha
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, Mkoa wa
Morogoro, Wakala wa Mbegu za Kilimo na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.
Aidha, Waandishi wa habari wa baadhi ya vyombo vya habari walishiriki
ziara hiyo ili kuona mafanikio yaliyopatikana katika kuendesha majaribio
ya aina ya mpunga wan chi kavu.
Serikali
inaendelea na mpango wa kuhamasisha ulimaji wa mazao makuu matano ya
Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa na Chai nchini ili kuongeza uzalishaji
wa mazao hayo.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa ameyasema hayoBungeni Mjini Dodoma wakati wa maswali kwa
Waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sumve Mhe. Richard
Ndassa juu ya namna Serikali ilivyojipanga na utafutaji wa masoko ya
Pamba kutokana na mwitikio mkubwa wa kulima zao hilo mwaka huu.
"Miongoni
mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na
kutafuta masoko ndani na nje ya nchi," alisema Waziri Mkuu.
Amesema,
mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini
ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya
Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.
Pia,
Mhe. Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi
Kuchauka juu ugawaji wa pembejeo za korosho kwa mwaka huu amesema,
Serikali ilitoa pembejeo ya Salfa bure mwaka jana kwa wakulima wa
korosho ili kufanya hamasa kwa zao hilo baada ya wakulima kutelekeza zao
hilo kutokana na kukosa pembejeo hiyo.
"Baada
ya ugawaji wa pembejeo hiyo ya Salfa zao hilo limevunwa kwa kiwango cha
juu kwa mwaka jana, hivyo kutokana na fedha walizozipata wakulima wa
zao hilo watatatikiwa kuchangia gharama za Salfa kwa mwaka huu," alisema
Mhe. Majaliwa.
Wakati huo huo, Mhe.
Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Urambo Mhe.
Margaret Sitta juu ya migogoro ya mipaka ya mapori na misitu, amesema
Serikali imeiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikisha wanavijiji
na viongozi wa kijiji wakati wa uwekaji wa mipaka hiyo.
Hata
hivyo amesema ikiwa kijiji kitaonekana kiko ndani ya mipaka ya msitu au
pori, tathimini itafanyike na baadae watapewa elimu ya kutoingia ndani
ya mipaka ya misitu na mapori ya Serikali Kuu.
Misitu yote ya Serikali Kuu inahifadhiwa kisheria na mipaka hiyo inaonekana ili kuondoa migogoro na wananchi.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa pamba kutochanganya pamba na mchanga au maji kwa sababu watakosa wanunuzi.
Pia
amesema Serikali itapambana na watu wote wanaotaka kuvuruga zao hilo,
hivyo amewataka wakulima waendelee kuwa na imani na Serikali yao.
Waziri
mkuu alitoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Februari 16, 2018) wakati
akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Kwimba.
“Wakulima
msichezee pamba kwa kuichanganya na chochote ili kuiongezea uzito kwa
sababu mtaharibu sifa nzuri ya pamba ya Tanzania ndani nan je ya nchi.”
Alisema
kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakulima wasiokuwa waaminifu ambao kabla
ya kuipeleka pamba sokoni wanachanganya na maji au mchanga.
Waziri
Mkuu alisema Serikali imeanza kuona tija tangu ilipoagiza Maofisa
Kilimo katika mikoa inayolima pamba wasimamie kilimo hicho kuanzia ngazi
za awali.
Akizungumzia
kuhusu suala la wanunuzi wa pamba, Waziri Mkuu alisema tayari Serikali
imeweka mikakati ya kutosha itakayowezesha pamba yote kununuliwa.
Kuhusu
suala la bei alisema wataangalia katika soko la Dunia na kisha
watawashawishi wanunuzi wanunue kwa bei nzuri itakayowanufaisha
wakulima.
Alisema
Serikali itaendelea kusimamia zao hilo kuanzia hatua za maandalizi ya
shamba kwa kulima kitaalam, upatikanaji wa pembejeo hadi masoko.
Awali,
Waziri Mkuu alitembelea mashamba ya mfano ya pamba katika kijiji cha
Kilyaboya na Igumangobo ambapo alisema ameridhishwa mashamba hayo.
Pia
aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kadashi,
mradi ambao ulioibuliwa na Diwani wa Kata ya Maligisu, Bw. Tabu Mapembe.
Kata
ya Maligisu yenye vijiji vine ina zahanati moja tu, kukamilika kwa
ujenzi wa zahanati hiyo kutasaidia kupunguza tatizo la utoaji wa huduma
za afya.
KILIMO BORA CHA PILIPILI MANGAKILIMO BORA CHA PILIPILI MANGA: Pilipili mtama au
kwa jina lingine pilipili manga ni kiungo muhimu sana katika mapishi.
Radha yake ya muwasho ndio kitu hasa kinachotafutwa katika vipunje
vidogo vidogo vya zao hili. Pilipili manga husagwa ili kupata ungaunga
kabla ya kutumika ingawa pia inaweza kutumika bila kusagwa.
Jina la kitalaam ni Piper nigram na kwa kiingereza ni black pepper.
Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika
mkoa wa Tanga na Zanzibar. Ingawa pia inaweza kukubali katika maeneo ya
Kagera
Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki
na kwa mapishi mengine mbalimbali. Nchi za magharibi zina matumizi
makubwa ya viungo hivi. Aidha pilipili mtama nyeusi ndiyo huzalishwa
zaidi hapa nchini.
Namna ya uzalishaji wa pilipili manga.
Hali ya hewa na udongo
Viungo vingi humea katika maeneo yenye joto la wastani kati ya nyuzi
joto 24-26 na huzalishwa maeneo ya mwambao. Udongo wenye rutuba na
unaopitisha maji na wenye uchachu wa kiasi cha pH 6.5. Mahitaji ya mvua
ni mililita 1500-2000 kwa mwaka.
Uchaguzi wa mbegu
Uchaguzi huzingatia mambo yafuatayo:-
a) Urefu wa pingili na ukubwa wa majani
b) Ufupi wa pingili unaoambatana na majani madogo.
Tofauti iko hadi kwenye umbile la matunda. Majani ya mche mama sehemu
kinapokatwa kipando huondolewa wiki mbili kabla ya kukata. Vipando
vyenye macho (nodes) 3-4 humika. Macho mawili huzikwa kwenye udongo na
kipando kiwekewe kivuli. Inashauriwa kuweka mbolea ya samadi wakati wa
kupanda. PILIPILI MANGA
Nafasi ya upandaji
Nafasi ya kupanda ni mita 2-3 kati ya mmea na mmea endapo miche imepandwa na miti inayotakiwa kupogolewa mara kwa mara.
Mahitaji ya mbolea
Matumizi ya mbolea hapa Tanzania si makubwa katika kilimo cha viungo.
Ingawa kiasi cha kilo 0.4 cha Urea, kilo 0.3 cha Superphosphate na kilo
0.3 cha Potash ya Muriate kinaweza kutumika kwa miche mikubwa.
Miti ya kusimikia miche
Miche hupandwa kwa kusimikiwa nguzo ili ikue kwa kujizungusha kwenye
miti kama mijenga ua, n.k. Mti huo wa kusimikia nao pia hupaswa
kupunguziwa majani ili kupunguza giza. Kila kabla ya msimu miti hiyo
hupaswa kupunguziwa matawi (pruning). Kupogolea miche ya pilipili mtama
Mche ukifikia miezi 18 inapaswa kupogolea kwa kukata sehemu ya juu ya
mche ili kufanya matawi mengine yachipue chini ya mche. Inashauriwa
mche kuwa na urefu wa mita 3-3.5.
Uvunaji
Maua ya kwanza hutoka baada ya miaka miwili. Matunda hukomaa miezi
tisa (9) hadi kumi (10). Uvunaji ni mizunguko 5 hadi 6 kwa mwaka.
Pilipili mtama inaweza kuvunwa kwa misimu miwili. Mavuno ni kati ya tani
0.35 – 3.75 kwa hekta. Wakati wa uvunaji kishina cha matunda ya kijani
hukatwa kutoka kwenye mti kisha mbegu za huchambuliwa kutoka kwenye
vishina na kisha huanikwa juani kwa siku 3 hadi 4 ili kuhakikisha
zinakauka vizuri kabisa. Kiasi cha unyevu kiwe angalau 13 – 14%. PILIPILI MTAMAKuhifadhi
Pilipili mtamailiyokaushwa vizuri inaweza ikawekwa kwenye chombo kisichopitisha hewa na kudumu kwa miaka hadi 20 bila kuharibika. Masoko ya pipili mtama
Soko la pilipili matama linapatikana ndani ya nchi na nje pia. Bei ya
ndani ni kati ya Sh1,000-1,500. Zao hili huuzwa katika nchi za Uganda,
Kenya, Uingereza, Ujerumani, Mashariki ya Kati, n.k. Bei ya Nje ni
wastani wa dola za kimarekani 1,985 kwa tani. (Tafadhali fanyia utafiti
soko, data hizi ni za siku nyingi)
KILIMO BORA CHA VITUNGUUKILIMO BORA CHA VITUNGUU:
Hapo awali kitungu kilikuwa ni zao lililokuwa linapatikana porini
katika ukanda wa bahari ya Mediterania. Zao hili hulimwa katika nchi
nyingi za magharibi, nchi za milima zilipo kaskazini mwa dunia, likwemo
bara la Afrika. Vitunguu hustawi katika hali ya hewa ya jotoridi 13°C –
24°C, hali ya hewa inayofaa kwa kuotesha na kukuzia miche kwenye kitalu
ni jotoridi 20°C – 25°C. Kwa kawaida vitunguu huhitaji kiasi cha joto
nyuzi 20°C-25°C ili kuweza kustawi na kukua vizuri. Joto zaidi ya hapo
hufanya vitunguu kudumaa na kutoweza kutengeneza viazi (bulbs).
KILIMO CHA VITUNGUUMatumizi
Kitunguu hutumika kama kiungo cha kuongeza ladha kwenye chakula, na pia hutumika kama dawa ya kansa ya tumbo, vidonda na majipu. Ustawi
Zao la vitunguu hustawi katika udongo wa tifu tifu wenye mbolea ya
kutosha, ukiwa na uchachu wa udongo (PH) kiasi cha 6 – 6.8. Udongo wa
mfinyanzi haufai kwa zao la vitunguu kwa kuwa hauruhusu viazi vya
vitunguu (bulbs) kutanuka. Hivyo uwezekano wa kupata mazao ni mdogo.
Pia udongo wa kichanga haufai kwa zao la kitunguu kwa kuwa hauna mbolea
na hivyo vitunguu huwa vidogo sana, jambo ambalo ni vigumu kupata mazao
yanayofaa kwa soko.
Zao la kitunguu huhitaji unyevu muda wote wa ukuaji wake. Zao hili
lina mizizi mifupi hivyo linahitaji kumwagiliwa maji mara kwa mara. AINA ZA VITUNGUUAINA ZA VITUNGUU
Kuna aina mbili za vitunguu ambazo zimezoeleka:
Vitunguu vya asili kama vile Singida, na Rujewa (aina hii ina rangi ya kahawia iliyopauka).
Chotara: Hii ni aina ya vitunguu inayojulikana kama vitunguu vya
kisasa. Katika kundi hili kuna vitunguu kama Texas grano, Red creole,
Bombay red, White granex, na Super rex.
Mgawanyiko
Zao la vitunguu limegawanyika katika makundi mawili. Hii inatokana na
uhitaji wa mwanga na ukuaji wake. Aina ya kwanza inahitaji mwanga kwa
saa 8-13 ili kuweza kuchanua na kutoa mbegu.
Aina ya pili inahitaji mwanga kwa saa 13-15 kuweza kuchanua na kutoa mbegu. UPANDAJI WA VITUNGUUKupanda
Vitunguu hupandwa kwa kutumia mbegu ambazo husiwa kwenye vitalu. Kitalu
kinaweza kuwa na upana wa mita 1, urefu unategemeana na ukubwa wa eneo
ulilo nalo.
Unaweza kupanda vitunguu kwenye matuta mbonyeo (Sunken bed). Aina hii
ya upandaji hutumika kwenye eneo lenye shida ya maji. Upana wa tuta uwe
mita moja.
Kupanda kwenye matuta mwinuko (Raised bed) upandaji wa iana hii hutu mika sehemu yenye maji mengi au yanayotuama.
Tahadhari: Maji yakituama kwenye vitunguu hufanya vitunguu kuoza, hivyo kuathiri mavuno. Nafasi
Vitunguu vipandwe kwa nafasi ya sentimita 7.5 kutoka mche hadi mche,
sentimita 12.5 kutoka mstari mmoja hadi mwingine kwenye matuta. UDONGO MZURI KWA VITUNGUUMbole ya kupandia
Unaweza kutumia mboji, au samadi iliyo oza vizuri kupandia. Baada ya
hapo unaweza kuongeza mboji baada ya miezi miwili. Endapo unafanya
kilimo kisichozingatia misingi ya kilimo hai, unaweza kupanda kwa
kutumia mbolea aina ya NPK (20:10:10) baada ya mwezi na nusu, unaweka
mbolea ya Urea. Palizi
Vitunguu ni zao lenye uwezo mdogo sana wa kushinda na magugu. Hivyo, inabidi shamba liwe safi muda wote wa ukuaji hadi kuvuna. UVUNAJI VITUNGUUUvunaji
Kwa kawaida, vitunguu huchukua muda wa miezi 5-6 tangu kupandwa hadi
kuvunwa. Unaweza kuanza kuvuna vitunguu baada ya asilimia 75 ya shingo
za vitunguu kuvunjika. Baada ya kuvuna, unaweza kuweka kwenye madaraja
(grades) kwa kufuata ukubwa, rangi na unene wa shingo ya kitunguu.
Vitunguu vyenye shingo nyembamba hudumu zaidi, vyenye shingo nene huoza
haraka. Ukataji
Hakikisha kuwa shingo ya kitunguu inabaki kiasi cha sentimita 2. Hii husaidia kuzuia kuoza haraka. Namna ya kuhifadhi vitunguu
Baada ya kuvuna, hifadhi vitunguu kwenye kichanja chini ya kivuli na
uvitandaze vizuri. Unaweza kuhifadhi vitunguu kwa kufunga kwenye
mafungu na kuvitundika. Vitunguu vikihifadhiwa vizuri vinaweza kukaa
hadi miezi minne bila kuharibika, hii hutegemeana na aina ya uhifadhi.
Wadudu wanaoshambulia vitunguu
Kuna aina nyingi za wadudu wanaoweza kushambulia vitunguu. Hawa
wafuatao ni baadhi ya wadudu waliozoeleka kwenye zao la vitunguu. WADUDU WABAYA
Thiripi (Thrips): Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na
shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na
kusababisha majani kuwa na doti nyeupe.
Madhara: Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia
KITUNGUU
Kimamba: Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza
ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni
hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.
Minyoo fundo (Nematodes): Aina hii ya minyoo hushambulia mizizi ya
vitunguu. Hali hii husababisha kudumaa kwa vitunguu kwa kuwa hushindwa
kufyonza maji na chakula kutoka ardhini.
Vidomozi (Leaf minor): Hushambulia majani kwa kujipenyeza kwenye
ngozi ya jani na kusababisha michoro ambayo huathiri utendaji wa majani.
Utitiri mwekundu (Red spider mites): Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani na kusababisha vitunguu kunyauka.
Funza wakatao miche: Funza hawa hutokana na wadudu wajulikanao kama Nondo, na hushambulia shina na kulikata kabisa. Namna ya kukabiliana na wadudu hawa
Unaweza kukabiliana na wadudu hawa kwa kufanya kilimo cha mzunguko.
Usioteshe vitunguu sehemu moja kwa muda mrefu, au kufuatanisha mazao
jamii ya vitunguu kama vile leaks.
Tumia mbegu bora zilizothibitishwa kutoka kwenye kampuni
zinatambuliwa kisheria na kibiashara. Kupanda kwa wakati unaotakiwa;
vitunguu visipandwe wakati wa kiangazi. Vipandwe wakati wa majira ya
baridi na kuvunwa wakati wa joto. Tumia dawa za asili za kuulia wadudu,
au dawa nyinginezo zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo. UGONJWA KWA VITUNGUU
1. Purple blotch: Ugonjwa huu husababishwa na ukungu (fungus).
Ugonjwa huu husababisha mabaka ya zambarau na meusi katika majani ya
vitunguu. Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu unyevu mwingi.
Madhara: Ugonjwa huu hupunguza mavuno mpaka asilimia hamsini (50%).
2. Stemphylium leaf blight: Hukausha majani kuanzia kwenye ncha hadio
kwenye shina.; Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu na ukungu mwingi.
Madhara: Hupunguza mavuno hadi kwa asilimia sabini na tano (75%).
VITUNGUU
Magonjwa ya virusi (Onion yellow draft virus): Ugonjwa huu
husababisha vitunguu kuwa na rangi iliyochanganyika, kijani na michirizi
myeupe au njano. Vitunguu hudumaa kwa kiasi kikubwa;Ugonjwa huu
husababishwa na kimamba.
Madhara: Huathiri mavuno kwa asilimia 80 mpaka asilimia 100%.
4. Kuoza kwa kiazi (Bulb rot): Husababishwa na fangasi. Ugonjwa huu
hutokea vitunguu vikishakomaa, huku udongo ukiwa na maji maji. Vitunguu
vikishakomaa visimwagiliwe tena. Uharibifu wa vitunguu usiotokana na magonjwa
1. Kuchipua baada ya kuvunwa: Hali hii hutokea endapo vitunguu vitavunwa
kabla ya muda wake. Endapo vitunguu havitakaushwa vizuri baada ya
kuvunwa. Hali hii husababisha uharibifu mpaka asilimia themanini (80%).
Sehemu ya kukaushia vitunguu iwe na hewa inayozunguka na mwanga wa
kutosha. Vitunguu vikiwekwa gizani huchipua kwa urahisi.
2. Muozo laini (Soft rot): Ugonjwa huu hushambulia vitunguu baada ya
kukomaa; husababishwa na vimelea (bacteria). Vitunguu hutoa harufu mbaya
ya uozo. Kuepuka hilo vuna kwa wakati unaofaa, hifadhi sehemu yenye
mwanga na hewa inayozunguka.
MAGONJWA MABAYA KWA VITUNGUUVirusi
Unaweza kuzuia vimamba ambao ndio wanaoeneza virusi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu. Vitunguu vinalipa
“Vitunguu vinatofauti kidogo na mazao mengine ya mboga mboga kwa kuwa
si rahisi kukosa soko, na endapo bei si nzuri unaweza kuhifadhi kwa
muda ili kusubiri bei iwe nzuri.” Ni maneno ya mkulima Peniel Rodrick
(pichani) ambaye amejikita zaidi katika kilimo cha vitunguu kibiashara.
Mkulima huyu kutoka kijiji cha Oloigeruno anasema pamoja na kwamba
anazalisha pia mazao mengine, lakini ameamua kujikita zaidi kwenye
vitunguu baada ya kugundua siri na namna ya kupata faida zaidi.
Toka aanze kilimo cha vitunguu miaka 12 iliyopita, ameweza kuendesha
maisha yake vizuri, ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mingine kama
ufugaji wa ng’ombe, kujenga nyumba ya kisasa na kuitunza familia yake ya
watoto watatu ipasavyo. Pamoja na hayo anasema tatizo kubwa la vitunguu
ni magonjwa na wadudu. Anasema si rahisi sana kugundua mara moja kuwa
kuna ugonjwa unaoshambulia vitunguu, na mara unapogundua unakuwa
umefikia kwenye hali mbaya
KILIMO BORA CHA KABICHIKILIMO BORA CHA KABICHI :
Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika
katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama
malisho ya mifugo
Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha
mimea ya kaulifulawa (cauliflower ), kabichi ya kichina na kale. Kwa
kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa
ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa
sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka.
Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa
baada ya kufunga na kukomaa vizuri.
Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida,
huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa
kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).
Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi.
Hali ya hewa: Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya
baridi, hali ya joto jingi haifai kwa kabichi kwa kuwa huathiri uotaji
na ukuaji wake. Joto jingi pia husababisha kulegea kwa vichwa
vilivyofunga. Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi
ya mita 100 toka usawa wa bahari.
Udongo: Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote
mradi tu udongo huo usiwe na chumvichumvi nyingi na usiotuhamisha maji.
Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi
kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo.
Kitalu: Kitalu ni muhimu katika uzalishji wa zao hili. Ni vema
kutengeneza matuta yenye upana wa mita moja, na urefu wowote kulingana
na matakwa ya mkulima.
Mbolea za samadi na zenye asili ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye
udongo. Kiasi cha gramu 500 za mbegu huhitajika kwa hekta moja. Katika
upandaji kwenye kitalu ni vizuri kutengeneza mistari katika tuta, umbali
toka mstari hadi mstari uwe sentimita ishirini (20). Udongo kiasi
kidogo utumike katika kufunika mbegu.
Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya miche na uwe katika kipimo cha sentimita 2-3 toka mche hadi mche.
Hii itasaidia kuwa na miche mifupi na yenye nguvu. Inafaa kunyeshea
kitalu mara moja au mbili kwa siku na katika sehemu za joto ni vizuri
kuweka kivuli katika matuta. Katika wiki ya tatu, hadi wiki ya nne, ni
vyema kuondoa kivuli kidogo kidogo huku ukipunguza unyeshaji. Hali hii
itasaidia miche isipate mshtuko wa uhamishaji shambani. Kuhamisha na kupanda
Hamisha na kupandikiza miche shambani ikiwa na umri wa wiki nne, wakati
huo miche ikiwa na majani manne ya mwanzoni na urefu wa kiasi cha
sentimita kumi na mbili (12). Wakati wa upandaji, ni vizuri udongo
ukashindiliwa kwenye kila mche. Inafaa upandaji ufanyike mara moja, na
ni vizuri ukafanyika nyakati za jioni au asubuhi sana, na udongo uwe na
unyevu wakati wote. Nafasi kati ya mmea
Katika mstari hadi mstari inatakiwa iwe sentimita 60-75. Kutoka mmea
hadi mmea ni sentimita 30-60. Pia sentimita 75-90 inaweza kutumika kati
ya mstari na mstari.
Mbolea: Ni vizuri kuweka kiasi cha viganja 2-3 vya mbolea ya samadi iliyooza vizuri katika kila shimo.
Palizi: Wakati wa palizi ni vizuri mkulima akawa mwangalifu ili
asiharibu mizizi. Wakati kabichi inapoanza kufunga hufunika ardhi,
hivyo, husaidia kuzuia magugu yasiote, kwa wakati huu hakuna haja ya
kupalilia.
Kuvuna: Kabichi hukomaa katika kipindi cha siku 60-100 tangu
kupandwa. Kwa ajili ya kuuza ni vizuri kuvuna wakati vichwa vinapofunga
vizuri na huwa na uzito wa kutosha kabichi iangaliwe na kutunzwa baada
ya kuvunwa ili isikwaruzwe na kuoza kabla ya kutumiwa. Kwa kawaida hekta
moja hutoa mavuno kiasi cha tani 50-80. Aina za kabichi
Kuna aina nyingi za kabichi na zifuatazo ni miongoni mwa aina hizo: Early Jersey wakefield – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5 Sugar loaf – Aina hii hukomaa mapema sana, kiasi cha miezi 2.5 Glory of enkhuizen – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5 Prize drumhead – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5 F1-High Breed – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 2-4 Duncan – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3